Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, April 29, 2023

AJARI. DEREVA, ABIRIA WANUSURIKA KIFO MORO.




 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Dereva wa gari ndogo aina ya Toyota Previs akiwa na abiria wake mmoja wamenusurika kifo baada ya gari hiyo iliyokuwa mwendo kasi kugonga kigo ya barabara na kuruka juu kabla ya kutua chini na kusota umbari wa takribani mita 50.

 

Tukio hilo lililoshuhudiwa ‘Live’ na Mwandishi wa habari hizi limetokea Mwishoni mwa wiki barabara kuu ya Morogoro-lringa eneo la Mataa ya Tumbaku.

Mwandishi wa Mtandao huu ambaye ndiye shuhuda pekee aliyeshuhudia tukio hilo  anauhabarisha umma A-Z.

 

”ljumaa majira ya saa 7 usiku wakati natokea kwenye shughuri zangu za Mlala Nnje kwenye moja ya ukumbi uliopo Mazimbu nikirejea nyumbani nilipofika kwenye Mtaa hayo kama ilivyo ada unapotokea upande wa Mazingu kuingia lringa Road kuelekea Msamvu kuna njia ya kuchepuka hunahaja ya kusubiri taa.

 

Hivyo nikiwa na Pikipiki licha ya taa nyekundu kuwaka Upande wangu nilichepuka kwenye njia hiyo, Kama inavyofahamika usiku huo Mnene mara nyingi gari sio mengi hivyo ile naikamata lringa Road tu niliona gari  hiyo yenye rangi ya ‘Dack Bluu’ikitokea upande wa Msamvu dereva huyo aliyekuwa akitokea Dar es salaam akielekea Upande wa lringa aliongeza mwendo kwa lengo la kuwahi taa ya Kijani iliyokaribika kuzima.

 

Hivyo dereva huyo ambaye ni mgeni Mkoani Morogoro hakujua kwamba eneo hilo la Mtaa kuna kigo ya matofari yaliyotumbukia ndani ya barabara, akili  na macho yake vyote vilikuwa kwenye Mataa hayo.

 

Alipofika eneo hilo huku akiwa mwendo kasi gari  iligonga kigo  ikaruka juu na kutua kwenye kitu cha mafuta ikilalia ubavu wa dereva.

Nilisimamisha Pikipiki yangu nikiangalia gari hiyo iliyokuwa mbele yangu ikipaa juu kama ndege.

 

Dakika chache niliona kundi la boda boda Kama Kunguru wa Zanzibar walioona mzoga, likiibuka eneo hilo ikiwemo boda boda ya Mwandishi wa Mtandao huu.

 

Kila boda boda alikuwa na malengo yake kwenye tukio  hilo wengine walifika  kwa lengo la kuwaibia wahanga wa tukio hilo, wengine walifika kwa lengo la kutoa Msaada kwa wahanga na mimi nilifika eneo hilo kwa lengo la kuchukua habari.

 

Waliokuwa na lengo la kuwaibia marehemu niliwashuhudia wakizungu nyuma wakifunua bodeni wakisaka mabegi huku wakipekua pekea vitu kama kuku Jalalani.

 

 Wale wenye mapenzi mema walifungua mlango wa dereva kwa lengo la kujua hali za waliondani,Wakiongozwa na mimi tulipofungua Mlango tuliona watu wawili wanaume dereva na abiria wake walikuwa salama baada ya kufunga mikanda hivyo gari ilivyo paa angani  kama ‘chopa’hawa kuhama hama baada ya kuzuiwa na hiyo mikanda ya usalama.

 

Baada ya kutoka kwenye gari hiyo nilipoinua uso nimewaona walinzi wenye silaha wa kituo hicho cha mafuta ambao waliwatawanya boda boda wote na kutoa ulinzi kwa wahanga hao si pati picha kama tukio hilo lingetokea vichakani.

 

Baada ya Walinzi hao kufika niliwaamulu dereva na abiri watoke kwenye gari hiyo iliyokuuwa imebonde huku taili ya kulia lililogonga kingo hiyo likiwa kule kule barabarani.

 

 Dereva huyo alipotoka alionekana kama kuchanganyikiwa ambapo alisema jambo moja kwamba kama hakugona mtu wala gari nyingine ameomba atafutiwe Winji ya kuinyanyua gari lake kwa lengo la kulirejesha Dar baada ya safari yake kuishia hapo.

 

Niliwashauri hayo yafanyike asubuhi kwa vile gari ipo kwenye ulinzi salama hapo kituo cha mafuta wao watafute usafiri waende hospital kucheki afya zao, walikubari ushauri huo. 

        WAHUSIKA WA BARABARA HIYO.

Kama ni TANROARD AU TARURUA hebu ondoeni hilo tumbo la tunda lililoingia ndani ya barabara bila sababau yoyote ambapo uwepo wake unachangia  kusababisha ajari kwa ndugu zetu wageni wanaotumia barabara hiyo sisi wenyeji tunalijua eneo hilo  je kwa ndugu zetu wageni?.

 Na kwenu Trafick mnakamata magari Mabovu mkidai yanasababisha ajari kwa nini msiikamate na hii barabara inayosababisha ajari na kuharibu maliza za watu mkiwashauri wa husika kuondoka tunda hilo kama mnavyotushauri sisi kutengeneza magari yetu mabovu? angalieni wenyewe hilo tumbo lililoingia barabarani madereva wageni nyakati za usiku wakifika eneo hilo  akili na macho yao  yana kuwa kwenye hayo mataa na sio kuangalia tumbo hilo la barabara ambalo limewekwa katikati.

 Na nyinyi madereva Mnapofika kwenye maeneo ya watu zingatieni ile spindi 50 au taha chini ya hapo kwa vile maeneo ya makazi ya watu kuna hatari nyingi.

 

 Mimi kama Mwandishi wa habari nimetimiza jukumu langu la kukosoa na kushauri Shekidele hana hatia Naamini viongozi wetu ni wasikivu watalifanyia kazi jambo hili.

Thursday, April 27, 2023

WATU MAARUFU WALIOSHIRIKI MSIBA WA MTANGZAJI ABOOD MEDIA HAWA HAPA

              Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Fatma Mwassa
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma Mh Divah Mathaman
Mbunge wa Viti Maalumu kwa lesen ya CCM akiwakilisha Mkoa wa Morogoro Mh Christina lshengoma
Mstahiki Meya wa Mji wa Morogoro ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro'MRFA Mhe Pascal Kihanga. kwenye maelezo Yake Kihanga alisema.

" Kijana huyu namfahamu vizrui kwenye harudi yake mimi likkuwa mwenyekiti wa kamati. Mimi pia ni Mwenyekiti wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro na Emma alikuwa Afissa habari wa chama hicho"aliseme Kihanga ambaye pia ni diwani wa kata ya Mazimbu na Mfanyabiashara maarufu wa wa mbao

Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Morogoro Vijijini[D.C] M h Rehema Said Bwassi
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Komredi Fikiri Juma
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mh Aziz Abood  Bw Morris akimwakilisha Mbunge huyu.

 lfahamike Mh Abood toka mziba wa Emma unatokea tulikuwa naye Mochwari akilipita gharama zote,siku moja kabla ya lbada hiyo ya kumuombea Mpendwa wetu Emma Mh Abood ambaye pia anamiliki Viwanda, Mabasi, Malori, Vituo vya Mafuta na Vyombo vya habari'Abood Media alipokea taarifa ya Mama yake aliyekuwa anaumwa hali yake kubadilika ghafla hivyo ilimradhimi kukimbia Dar kumjulia hali mzazi wake huyo. 

 

Mara zote akiwa huko Dar Abood alipiga simu kujua kinachoendelea kwenye lbada hiyo ya kumuombea Emma.

Mchungaji wa kanisa la Anglikana Paleshi ya Kingolwira Magereza Jonas Mshomi aliongoza lbada hiyo nyumbani kw amarehemu Mkambarani nyuma ya baa ya Moseka.
Mwenyekiti wa chama cha Waandoshi wa habari Mkoa wa Morogoro Nickson Mkilanya. lkumbukwe Hayati Emma alikuwa Mwanachama hai wa chama hicho
Kujisifu sio dhambi ila dhambi ni kuziendekeza hizo sifa.

 Mwamba Dustan Shekidele'Mkude Simba' na mimi nilikuwepo kwenye msiba huo wa Mwanachama mwenzangu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro

                 Mwamba  Emmanuel Victor Mdoe
 

Tuesday, April 25, 2023

MKE WA HAYATI EMMA AFANYA USHUJAA KWENYE JENEZA LA MUME WAKE.





Watoto wa Marehemu Emma wa kwanza kushoto na wapili kulia huyo wa kati ni mtoto wa dada yake Doris
 

          Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

INAUMA SANA.

Kama nilivyoripoti juzi Mjane wa Mtangazaji mahari wa Abood Media Hayati Emmanuel Victor Mdoe Bi. Doris Bonifas Luhanga alikuwa na siku nne toka alipojifungua Mtoto wa kike kwa uparesheni.

Kwa ushauri wa Madaktari ili kulinda mshono huo mbicho usipasuke hakupaswa kulilia Mpendwa Mume wake kwa sauti. Hivyo wakati wa kuaga mwili wa mpendwa Mume wake.

 

 

 Mjane huyo wa Marehemu alikusanya watoto zake wawili na yule mtoto wa dada yake aliyekuwa akiishia naye kwa pamoja waliinamisha michwa kwenye jeneza na mpendwa baba yao bila kutoa machozi huku Mama yao akiangusha maombi mazito. Sehemu ya maombi hayo yaliyonaswa na Mwandishi wa habari hizi ni haya

” Baba umeondoka ghafla huku tukiwa bado tunakupenda lakini Mungu amekupenda Zaidi, hivyo tunamuomba Mungu akusamehe makosa yako n akupokea, binafsi umeniachia malezi ya watoto namuomba Mungu anipe nguvu na hekima ya kutimiza jukumu hiyo zito la malezi.

 

” Maombi hayo yaligusa watu wengi wakiwemo viongozi wa dini waliokuwa eneo la tukio. Mtandao huu unamuomba Mwenyezi Mungu azidi kumpe nguvu Mjane huyo wa marehemu kwenye kipindi hiki kigumu anachokipitia.

 

Marehemu Emma ameacha Mjane Doris Bonifas Lulanga ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Tomondo iliyopo Halmashauri ya Morogoro Vijijini[DC] na watoto 3 wakwanza Victor, wapili Dailan wakiume.na watatu ni wakike ambaye hadi baba yake anafariki dunia alikuwa na umri wa siku 4 hivyo hataji jina alikuwa haja pewa.

 

Pichani wa kati ni mtoto wa dada yake Doris ambaye toka akiwa mdogo familia hiyo ya Emmanuel Victor ilimchukua na kuishi naye hapo nyumbani.

 

Kwenye tukio hilo la kuaga mtoto huyo mchanga hakuweza kumuaga baba yake kutokana uchanga wake wa siku 4 toka aje hapa duniani.

 

Swali kwako msomaji wa habari hii ya kuumiza moyo,mtoto huyo Mchange hajapewa jina je kama ukipewa nafasi ya kutoa jina kwa mtoto huyo aliyezaliwa katika mazingia ya  uparesheni na baada ya kuzaliwa siku 4 mbele baba yake amefariki dunia ungempa jina gani la faraja katika maisha yake?

Sunday, April 23, 2023

MKUU WA MKOA, WAKUU WA WILAYA, WABUNGE NA WAKURUGENZI JANA WAMESHIRIKI IBADA YA KUMUOMBEA MWANDISHI WA HABARI.

                             Mkuu wa Mkoa akiwasili msibani

Kigogo wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro akitoa salama za Jeshi hilo
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro Nick son Mkilanya akitoa salama za rambi rambi .lfahamike marehemu Emma alikuwa Mwanachama hai wa Chama hicho
Mtangazaji wa Abood Media Yahaya Limangwa ambaye ndiye wa kwanza kufika eneo la tukio majira ya saa 11 alfajiri akieleza tukio hilo A-Z
Mratibu wa Makapuni ya Abood Group Morris akitoa salama za salambi rambi kwa mfanyakazi wake
Jenere lililobebe mwili wa mpendwa wetu Emma likiwa ndani ya nyumba yake kabla ya kutokewa nje kwa lbada
Mkuu wa mkoa wa morogoro Fatma Mwassa[kulia] akimpa mkono wa pole Mjane wa Marehemu


Meneja wa Abood Media Abed Dogori akiongoza mamia ya wananchi kutoa mwili wa marehemu Nnje

Projuza wa Abood Media Modest Modest [Mr Ujembe] akishikilia msalama wa marehemu
Mjane wa Marehemu akiwa na maumivu mawili ya kufiwa na mumewe na yale ya mshono
Mchungaji  akiongoza lbada hiyo jana mchana
Afande Bitrisi Lyamuya akimuaha marehemu Emma
Mratibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Thadei Hafigwa'Komredi' akimuaga Mwanachama wake huku akiwa na begi mgongoni tayari kwa safari ya kuelekea Handeni kwa mazishi
Mchezaji wa Moro Veterani Afande Mstaafu Mzee Kondo naye akimuaha marehemu Emma
Mmoja wawanakamati wa msiba huo Peter Kimath akitoa heshima zake za mwisho kwa Mwandishi mwenzake, wa nyuma yake ni Meneja wa SUA Media Gerard Lomile'Mtu kazi'
Mratibu Mkuu wa kamati ya Msiba huo Mh Ratifa Ganzel akitoa sadaka mara baada ya kumuaga mwandishi mwenzia. lfahamike Mh Ratifa pia ni diwani wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM
 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

MKUU wa Mkoa wa Morogoro Mh Fatma Mwassa, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mh Divah Mathaman, Mbunge wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM kutoka Mkoa wa Morogoro Mh Christina lshengoma, Meya Manispaa ya Morogoro Mh Pascal Kihanga,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini[DC] Mh Rehema Bwassi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mh Firiki Juma,Madiwani na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Morogoro kwa pamoja jana mchana wameshiriki lbada ya kumuombea Mtangazaji wa Abood Media Hayati Emmanuel Victor Mdoe[41].
 
lbada hiyo iliyoongozwa na Mchungaji kiongozi wa kanisa la Anglikana Paleshi ya Kingolwira Magereza Mch. Jonas Mshomi imefanyika nyumbani kwa Marehemu Mkambarani nyuma ya baa ya Moseka inayomilikiwa na aliyekuwa Mkuu wa Polisi Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es salaam R.C.O Zombe.
 
Katika Mahuburi yake Mchungaji Mshomi alisema Marehemu Emma aliwekeza kwa Mungu.
 
” Marehemu Emma alikuwa akisali kwenye kanisa letu hapa Magereza, pia kabla ya kuhamia hapa kwenye nyumbani yake awari alikuwa akiishi Msamvu na Viongozi wenzangu wa kanisa la Msamvu wamsema Marehemu Emma alijitolea kujenga Madhabahu kwenye kanisa lile hivyo tutaendelea kumkumbuka kwa hilo pia”alisema Kasisi huyo. 
 
Pia Viongozi niliyowataja hapo juu baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na Mc wa shughuli hiyo Antony Muhanda ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Morogoro, kila mmoja alitoa ashuhuda alivyofanya kazi vizuri na marehemu Emma.
 
Hayati Emma alifariki dunia Jumatano Usiku wakati akitoka Mjini kwenye shughuri zake akireja nyumbani kwake Kijiji cha Mkambarani kilichopo umbali wa kilometa 15 kutoka Mjini amabapo kipo kando kando ya barabara kuu ya Moro -Dar gari yake aliyokuwa akiendesha Toyota IST iliacha njia na kupinduka umbali wa mita 100 kutoka barabarani. 
 
Marehemu Emma ameacha Mjane Doris Bonifas Lulanga ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Tomondo iliyopo Halmashauri ya Morogoro Vijijini[DC] na watoto 3 wakwanza Victor, wapili Dailan wakiume.
 
Kwa mujibu wa Mjane huyo mtoto wao 3 ni wakike hajapewa jina kwani amezaliwa kwa uparesheni siku 4 zilizopita.
lnauma sana Mke akiwa na mshono mbichi tumboni anapokeka taarifa za kifo cha Mpendwa Mumewe wake aliyezimika kama mshumaa.
 
Wakati wa kuaga mwili wa mpendwa mume wake Mjane huyo aliwakusanya watoto zake na kufanya tukio la kishujaa. tukio hilo lililonaswa live na Mtandao huu litaruka hewani hivi punde Pamoja na Picha za viongozi wote walishiriki lbada hiyo hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
 
Mara baada ya lbada hiyo iliyokuwa na baraka ya Mvua kukamilika Majira ya saa 8 mchana Msafara wa kuelekea Kijijini cha Kibeleke Handeni Mkoani Tanga kumpunzisha mependwa wetu kwenye nyumba yake ya Milele ilianza kwa maombi ya watumishi wa mungu 3.

Saturday, April 22, 2023

MKUU WA MKOA MORO ANGOZA MAMIA YA WANANCHI KUMUAGA MWANDISHI WA HABARI



 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro leo Mchana ameongoza Mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro kumuaga Mtangazaji wa Abood Media Hayati Emmanuel Victor Mdoe. Habari kamili na matukio kibao endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...