Watoto wa Marehemu Emma wa kwanza kushoto na wapili kulia huyo wa kati ni mtoto wa dada yake Doris
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
INAUMA SANA.
Kama nilivyoripoti juzi Mjane wa Mtangazaji mahari wa Abood Media Hayati Emmanuel Victor Mdoe Bi. Doris Bonifas Luhanga alikuwa na siku nne toka alipojifungua Mtoto wa kike kwa uparesheni.
Kwa ushauri wa Madaktari ili kulinda mshono huo mbicho usipasuke hakupaswa kulilia Mpendwa Mume wake kwa sauti. Hivyo wakati wa kuaga mwili wa mpendwa Mume wake.
Mjane huyo wa Marehemu alikusanya watoto zake wawili na yule mtoto wa dada yake aliyekuwa akiishia naye kwa pamoja waliinamisha michwa kwenye jeneza na mpendwa baba yao bila kutoa machozi huku Mama yao akiangusha maombi mazito. Sehemu ya maombi hayo yaliyonaswa na Mwandishi wa habari hizi ni haya
” Baba umeondoka ghafla huku tukiwa bado tunakupenda lakini Mungu amekupenda Zaidi, hivyo tunamuomba Mungu akusamehe makosa yako n akupokea, binafsi umeniachia malezi ya watoto namuomba Mungu anipe nguvu na hekima ya kutimiza jukumu hiyo zito la malezi.
” Maombi hayo yaligusa watu wengi wakiwemo viongozi wa dini waliokuwa eneo la tukio. Mtandao huu unamuomba Mwenyezi Mungu azidi kumpe nguvu Mjane huyo wa marehemu kwenye kipindi hiki kigumu anachokipitia.
Marehemu Emma ameacha Mjane Doris Bonifas Lulanga ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Tomondo iliyopo Halmashauri ya Morogoro Vijijini[DC] na watoto 3 wakwanza Victor, wapili Dailan wakiume.na watatu ni wakike ambaye hadi baba yake anafariki dunia alikuwa na umri wa siku 4 hivyo hataji jina alikuwa haja pewa.
Pichani wa kati ni mtoto wa dada yake Doris ambaye toka akiwa mdogo familia hiyo ya Emmanuel Victor ilimchukua na kuishi naye hapo nyumbani.
Kwenye tukio hilo la kuaga mtoto huyo mchanga hakuweza kumuaga baba yake kutokana uchanga wake wa siku 4 toka aje hapa duniani.
Swali kwako msomaji wa habari hii ya kuumiza moyo,mtoto huyo Mchange hajapewa jina je kama ukipewa nafasi ya kutoa jina kwa mtoto huyo aliyezaliwa katika mazingia ya uparesheni na baada ya kuzaliwa siku 4 mbele baba yake amefariki dunia ungempa jina gani la faraja katika maisha yake?
No comments:
Post a Comment