Kigogo wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro akitoa salama za Jeshi hilo
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro Nick son Mkilanya akitoa salama za rambi rambi .lfahamike marehemu Emma alikuwa Mwanachama hai wa Chama hicho
Mtangazaji wa Abood Media Yahaya Limangwa ambaye ndiye wa kwanza kufika eneo la tukio majira ya saa 11 alfajiri akieleza tukio hilo A-Z
Mratibu wa Makapuni ya Abood Group Morris akitoa salama za salambi rambi kwa mfanyakazi wake
Jenere lililobebe mwili wa mpendwa wetu Emma likiwa ndani ya nyumba yake kabla ya kutokewa nje kwa lbada
Mkuu wa mkoa wa morogoro Fatma Mwassa[kulia] akimpa mkono wa pole Mjane wa Marehemu
Meneja wa Abood Media Abed Dogori akiongoza mamia ya wananchi kutoa mwili wa marehemu Nnje
Projuza wa Abood Media Modest Modest [Mr Ujembe] akishikilia msalama wa marehemu
Mjane wa Marehemu akiwa na maumivu mawili ya kufiwa na mumewe na yale ya mshono
Mchungaji akiongoza lbada hiyo jana mchana
Afande Bitrisi Lyamuya akimuaha marehemu Emma
Mratibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Thadei Hafigwa'Komredi' akimuaga Mwanachama wake huku akiwa na begi mgongoni tayari kwa safari ya kuelekea Handeni kwa mazishi
Mchezaji wa Moro Veterani Afande Mstaafu Mzee Kondo naye akimuaha marehemu Emma
Mmoja wawanakamati wa msiba huo Peter Kimath akitoa heshima zake za mwisho kwa Mwandishi mwenzake, wa nyuma yake ni Meneja wa SUA Media Gerard Lomile'Mtu kazi'
Mratibu Mkuu wa kamati ya Msiba huo Mh Ratifa Ganzel akitoa sadaka mara baada ya kumuaga mwandishi mwenzia. lfahamike Mh Ratifa pia ni diwani wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro Mh Fatma Mwassa, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mh Divah Mathaman, Mbunge wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM kutoka Mkoa wa Morogoro Mh Christina lshengoma, Meya Manispaa ya Morogoro Mh Pascal Kihanga,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini[DC] Mh Rehema Bwassi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mh Firiki Juma,Madiwani na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Morogoro kwa pamoja jana mchana wameshiriki lbada ya kumuombea Mtangazaji wa Abood Media Hayati Emmanuel Victor Mdoe[41].
lbada hiyo iliyoongozwa na Mchungaji kiongozi wa kanisa la Anglikana Paleshi ya Kingolwira Magereza Mch. Jonas Mshomi imefanyika nyumbani kwa Marehemu Mkambarani nyuma ya baa ya Moseka inayomilikiwa na aliyekuwa Mkuu wa Polisi Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es salaam R.C.O Zombe.
Katika Mahuburi yake Mchungaji Mshomi alisema Marehemu Emma aliwekeza kwa Mungu.
” Marehemu Emma alikuwa akisali kwenye kanisa letu hapa Magereza, pia kabla ya kuhamia hapa kwenye nyumbani yake awari alikuwa akiishi Msamvu na Viongozi wenzangu wa kanisa la Msamvu wamsema Marehemu Emma alijitolea kujenga Madhabahu kwenye kanisa lile hivyo tutaendelea kumkumbuka kwa hilo pia”alisema Kasisi huyo.
Pia Viongozi niliyowataja hapo juu baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na Mc wa shughuli hiyo Antony Muhanda ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Morogoro, kila mmoja alitoa ashuhuda alivyofanya kazi vizuri na marehemu Emma.
Hayati Emma alifariki dunia Jumatano Usiku wakati akitoka Mjini kwenye shughuri zake akireja nyumbani kwake Kijiji cha Mkambarani kilichopo umbali wa kilometa 15 kutoka Mjini amabapo kipo kando kando ya barabara kuu ya Moro -Dar gari yake aliyokuwa akiendesha Toyota IST iliacha njia na kupinduka umbali wa mita 100 kutoka barabarani.
Marehemu Emma ameacha Mjane Doris Bonifas Lulanga ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Tomondo iliyopo Halmashauri ya Morogoro Vijijini[DC] na watoto 3 wakwanza Victor, wapili Dailan wakiume.
Kwa mujibu wa Mjane huyo mtoto wao 3 ni wakike hajapewa jina kwani amezaliwa kwa uparesheni siku 4 zilizopita.
lnauma sana Mke akiwa na mshono mbichi tumboni anapokeka taarifa za kifo cha Mpendwa Mumewe wake aliyezimika kama mshumaa.
Wakati wa kuaga mwili wa mpendwa mume wake Mjane huyo aliwakusanya watoto zake na kufanya tukio la kishujaa. tukio hilo lililonaswa live na Mtandao huu litaruka hewani hivi punde Pamoja na Picha za viongozi wote walishiriki lbada hiyo hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
Mara baada ya lbada hiyo iliyokuwa na baraka ya Mvua kukamilika Majira ya saa 8 mchana Msafara wa kuelekea Kijijini cha Kibeleke Handeni Mkoani Tanga kumpunzisha mependwa wetu kwenye nyumba yake ya Milele ilianza kwa maombi ya watumishi wa mungu 3.
No comments:
Post a Comment