Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, April 29, 2023

AJARI. DEREVA, ABIRIA WANUSURIKA KIFO MORO.




 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

Dereva wa gari ndogo aina ya Toyota Previs akiwa na abiria wake mmoja wamenusurika kifo baada ya gari hiyo iliyokuwa mwendo kasi kugonga kigo ya barabara na kuruka juu kabla ya kutua chini na kusota umbari wa takribani mita 50.

 

Tukio hilo lililoshuhudiwa ‘Live’ na Mwandishi wa habari hizi limetokea Mwishoni mwa wiki barabara kuu ya Morogoro-lringa eneo la Mataa ya Tumbaku.

Mwandishi wa Mtandao huu ambaye ndiye shuhuda pekee aliyeshuhudia tukio hilo  anauhabarisha umma A-Z.

 

”ljumaa majira ya saa 7 usiku wakati natokea kwenye shughuri zangu za Mlala Nnje kwenye moja ya ukumbi uliopo Mazimbu nikirejea nyumbani nilipofika kwenye Mtaa hayo kama ilivyo ada unapotokea upande wa Mazingu kuingia lringa Road kuelekea Msamvu kuna njia ya kuchepuka hunahaja ya kusubiri taa.

 

Hivyo nikiwa na Pikipiki licha ya taa nyekundu kuwaka Upande wangu nilichepuka kwenye njia hiyo, Kama inavyofahamika usiku huo Mnene mara nyingi gari sio mengi hivyo ile naikamata lringa Road tu niliona gari  hiyo yenye rangi ya ‘Dack Bluu’ikitokea upande wa Msamvu dereva huyo aliyekuwa akitokea Dar es salaam akielekea Upande wa lringa aliongeza mwendo kwa lengo la kuwahi taa ya Kijani iliyokaribika kuzima.

 

Hivyo dereva huyo ambaye ni mgeni Mkoani Morogoro hakujua kwamba eneo hilo la Mtaa kuna kigo ya matofari yaliyotumbukia ndani ya barabara, akili  na macho yake vyote vilikuwa kwenye Mataa hayo.

 

Alipofika eneo hilo huku akiwa mwendo kasi gari  iligonga kigo  ikaruka juu na kutua kwenye kitu cha mafuta ikilalia ubavu wa dereva.

Nilisimamisha Pikipiki yangu nikiangalia gari hiyo iliyokuwa mbele yangu ikipaa juu kama ndege.

 

Dakika chache niliona kundi la boda boda Kama Kunguru wa Zanzibar walioona mzoga, likiibuka eneo hilo ikiwemo boda boda ya Mwandishi wa Mtandao huu.

 

Kila boda boda alikuwa na malengo yake kwenye tukio  hilo wengine walifika  kwa lengo la kuwaibia wahanga wa tukio hilo, wengine walifika kwa lengo la kutoa Msaada kwa wahanga na mimi nilifika eneo hilo kwa lengo la kuchukua habari.

 

Waliokuwa na lengo la kuwaibia marehemu niliwashuhudia wakizungu nyuma wakifunua bodeni wakisaka mabegi huku wakipekua pekea vitu kama kuku Jalalani.

 

 Wale wenye mapenzi mema walifungua mlango wa dereva kwa lengo la kujua hali za waliondani,Wakiongozwa na mimi tulipofungua Mlango tuliona watu wawili wanaume dereva na abiria wake walikuwa salama baada ya kufunga mikanda hivyo gari ilivyo paa angani  kama ‘chopa’hawa kuhama hama baada ya kuzuiwa na hiyo mikanda ya usalama.

 

Baada ya kutoka kwenye gari hiyo nilipoinua uso nimewaona walinzi wenye silaha wa kituo hicho cha mafuta ambao waliwatawanya boda boda wote na kutoa ulinzi kwa wahanga hao si pati picha kama tukio hilo lingetokea vichakani.

 

Baada ya Walinzi hao kufika niliwaamulu dereva na abiri watoke kwenye gari hiyo iliyokuuwa imebonde huku taili ya kulia lililogonga kingo hiyo likiwa kule kule barabarani.

 

 Dereva huyo alipotoka alionekana kama kuchanganyikiwa ambapo alisema jambo moja kwamba kama hakugona mtu wala gari nyingine ameomba atafutiwe Winji ya kuinyanyua gari lake kwa lengo la kulirejesha Dar baada ya safari yake kuishia hapo.

 

Niliwashauri hayo yafanyike asubuhi kwa vile gari ipo kwenye ulinzi salama hapo kituo cha mafuta wao watafute usafiri waende hospital kucheki afya zao, walikubari ushauri huo. 

        WAHUSIKA WA BARABARA HIYO.

Kama ni TANROARD AU TARURUA hebu ondoeni hilo tumbo la tunda lililoingia ndani ya barabara bila sababau yoyote ambapo uwepo wake unachangia  kusababisha ajari kwa ndugu zetu wageni wanaotumia barabara hiyo sisi wenyeji tunalijua eneo hilo  je kwa ndugu zetu wageni?.

 Na kwenu Trafick mnakamata magari Mabovu mkidai yanasababisha ajari kwa nini msiikamate na hii barabara inayosababisha ajari na kuharibu maliza za watu mkiwashauri wa husika kuondoka tunda hilo kama mnavyotushauri sisi kutengeneza magari yetu mabovu? angalieni wenyewe hilo tumbo lililoingia barabarani madereva wageni nyakati za usiku wakifika eneo hilo  akili na macho yao  yana kuwa kwenye hayo mataa na sio kuangalia tumbo hilo la barabara ambalo limewekwa katikati.

 Na nyinyi madereva Mnapofika kwenye maeneo ya watu zingatieni ile spindi 50 au taha chini ya hapo kwa vile maeneo ya makazi ya watu kuna hatari nyingi.

 

 Mimi kama Mwandishi wa habari nimetimiza jukumu langu la kukosoa na kushauri Shekidele hana hatia Naamini viongozi wetu ni wasikivu watalifanyia kazi jambo hili.

1 comment:

  1. Thanks for the taarifa chief.... Hapo linatakiwa kupigwa rangi ama kuwekwa reflactor ambapo yeyote ataliona kwa urahisi. Nawasilisha hoja to Tanroad.. road signs no muhimu ajali ztapungua👍

    ReplyDelete

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...