Mfadhiri wa Coastal Union Tajiri Nassoro Salum Binslum[kushoto] akimkabidha mkataba Marcello mara baada ya kusainiwa na pande zote mbili Marcello akiambaa ambaa na Mpira na guu lake la shoto
Na Dunstana
Shekidele,Morogoro.
Wakati dirisha kubwa la Usajiri likielekea Ukingoni
timu kongwe nchini Coastal Union ya Jijini Tanga’ Wanamangushi’ a.k.a Wagosi wa
Kaya’ wiki end iliyopita wamefanikiwa kumsajiri
beki chipukizi Omary Mbaruku Maarufu Marcello kutoka timu ya daraja la kwanza
ya Fountain Gate ya Jijini Dodoma.
lfahamike Marcello kabla
ya kujiunga na Fountain Gate Miaka miwili iliyopita alikuwa akiitumikia timu ya
Mawenzi Market ya Mkoani Morogoro iliyokuwa akishiriki pia ligi daraja la
kwanza, hivyo wadau wa soka Mkoani Morogoro akiwemo Mwandishi wa habari hizi
wanamfahamu vizuri Mchezaji huyo.
Hivyo kwa kinywa kipana pasina shaka yoyote Coastal
kunasa saini ya mchezaji huyo Mwenyeji wa Visiwa vya Pemba Zanzibar anayemudu
vyema kucheza beki ya kushoto wameramba dume.
Wakati akiwa Mawenzi Mwandishi wa Mtandao huu
alimfuatilia mchezaji huyo anayetumia
mguu wa kushoto,mwenye kasi ya ajabu ya kupanda na kushuka huku akimwaga Krosi kali
kwenye lango la wapinzani.
Kufuatia hali hiyo Mashabiki wa Mawenzi walimpachika
jina la Marcello wakimlinganisha na aliyekuwa beki kisiki wa Real Madrid ya Hispani anayecheza beki ya
kushoto anayetumia pia mguu wa kushoto Marcello Vieira Da Salva Raia wa Brazil.
Baada ya kujiunga na Coatal Union Jumapili
iliyopita siku iliyofuata [Jumatatu] Mwandishi wa Mtandao huu alimtwangia simu
Marcello.
“ Shekidele ni kweli jana nimejiunga na Coastal kwa Mkataba wa Miaka 2 kwa sasa niko Kambini Tanga na timu yangu hiyo
Mpya”alisema mchezaji huo na kuendelea kufunguka.
“Kwa mafanikio haya ya kusajiriwa na timu kubwa ya
Coastal inayocheza ligi kuu, kipekee
namshukuru Mwenyezi Mungu, Ndugu zangu,
Mkurugenzi wangu wa Fountain Gate Jaftet
Makau na Viongozi wa Mawenzi Market, wachezaji wenzangi wa Mawenzi na mashabiki
wote wa Mawenzi.
Kipekee nivishukulu vitu vya soka vilivyoibua Kipaji changu
toka nikiwa mdogo.
Vituo hivyo ni Kisa cha nyumbani Pemba na Taasisi ya Mseti
Foundation ya Jijini Dar.
Nitakuwa mchoyo wa
fadhira nisipokushukuru wewe Shekidele Mwandishi bora wa habari za michezo
umekuwa karibu sana na mimi licha ya kuhama Morogoro ubarikiwe sana”alisema Marcello.
Ahadi yangu kwa umma
wawatanzania ndani ya miaka hiyo 2 Coastal watamuuza beki huyo kwa pesa
ndefu kwa timu kubwa nchini, hilo
linaweza kushindikana kama Omary Marcello anabadilika kitabia na kulewa sifa za
mafanikio.
Na amini hilo haliwezi kutokea kwa sababu namfahamu Omary ni Mcha mungu Mzuri mwenye
hofu na Allah, si Mjivumi na wala sio mlevi, hana Mambo Mengi ya tamaa za Mali
na Mapenzi ni Mtu Smart.
Mtandao huu unamuombe kila lenye kheri kwenye mafanikio yake
ya kucheza ligi kuu kwa mara ya kwanza kwenye histori ya maisha yake.
Dirisha kubwa la Usajri nchini lilifunguliwa Julai
1 na linafungwa Julai 31 huku pazia la ligi kuu likirajiwa kuzinduliwa Agost 13
kwa mchezo wa ngao ya Jamii kwa mpambano wa watani wa Jadi Simba na Yanga. huku
ligi hiyo ikitarajiwa kuanza Agost 17.