Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, July 27, 2022

KWA USAJIRI HUU WA MARCELO COASTAL UNION WAMERAMBA DUME.

Mfadhiri wa Coastal Union Tajiri Nassoro Salum Binslum[kushoto] akimkabidha mkataba  Marcello mara baada ya kusainiwa na pande zote mbili

 Marcello akiambaa ambaa na Mpira na guu lake la shoto


 

 Na Dunstana Shekidele,Morogoro.

 

 

Wakati dirisha kubwa la Usajiri likielekea Ukingoni timu kongwe nchini Coastal Union ya Jijini Tanga’ Wanamangushi’ a.k.a Wagosi wa Kaya’  wiki end iliyopita wamefanikiwa kumsajiri beki chipukizi Omary Mbaruku Maarufu Marcello kutoka timu ya daraja la kwanza ya Fountain Gate ya Jijini Dodoma.

 

 lfahamike Marcello kabla ya kujiunga na Fountain Gate Miaka miwili iliyopita alikuwa akiitumikia timu ya Mawenzi Market ya Mkoani Morogoro iliyokuwa akishiriki pia ligi daraja la kwanza, hivyo wadau wa soka Mkoani Morogoro akiwemo Mwandishi wa habari hizi wanamfahamu vizuri Mchezaji huyo.

 

 

Hivyo kwa kinywa kipana pasina shaka yoyote Coastal kunasa saini ya mchezaji huyo Mwenyeji wa Visiwa vya Pemba Zanzibar anayemudu vyema kucheza beki ya kushoto wameramba dume.

 

Wakati akiwa Mawenzi Mwandishi wa Mtandao huu alimfuatilia  mchezaji huyo anayetumia mguu  wa kushoto,mwenye  kasi ya ajabu ya  kupanda na kushuka huku akimwaga Krosi kali kwenye lango la wapinzani.

 

 

 

 

Kufuatia hali hiyo Mashabiki wa Mawenzi walimpachika jina la Marcello wakimlinganisha na aliyekuwa beki kisiki  wa Real Madrid ya Hispani anayecheza beki ya kushoto anayetumia pia mguu wa kushoto Marcello Vieira Da Salva Raia wa Brazil.

 

 

Baada ya kujiunga na Coatal Union Jumapili iliyopita siku iliyofuata [Jumatatu] Mwandishi wa Mtandao huu alimtwangia simu Marcello.

 

 

“ Shekidele ni kweli jana nimejiunga na Coastal  kwa Mkataba wa Miaka 2  kwa sasa niko Kambini Tanga na timu yangu hiyo Mpya”alisema mchezaji huo na kuendelea kufunguka.

 

 

“Kwa mafanikio haya ya kusajiriwa na timu kubwa ya Coastal  inayocheza ligi kuu, kipekee namshukuru Mwenyezi Mungu, Ndugu  zangu, Mkurugenzi wangu wa Fountain Gate  Jaftet Makau na Viongozi wa Mawenzi Market, wachezaji wenzangi wa Mawenzi na mashabiki wote wa Mawenzi.

 

     

Kipekee nivishukulu vitu vya soka vilivyoibua Kipaji changu toka nikiwa mdogo.

 

Vituo hivyo ni Kisa cha nyumbani Pemba na Taasisi ya Mseti Foundation ya Jijini Dar.

 

  Nitakuwa mchoyo wa fadhira nisipokushukuru wewe Shekidele Mwandishi bora wa habari za michezo umekuwa karibu sana na mimi licha ya kuhama Morogoro ubarikiwe sana”alisema  Marcello.

 

 Ahadi yangu kwa umma wawatanzania ndani ya miaka hiyo 2 Coastal watamuuza beki huyo kwa pesa ndefu  kwa timu kubwa nchini, hilo linaweza kushindikana kama Omary Marcello anabadilika kitabia na kulewa sifa za mafanikio.

 

 

Na amini hilo haliwezi kutokea kwa sababu  namfahamu Omary ni Mcha mungu Mzuri mwenye hofu na Allah, si Mjivumi na wala sio mlevi, hana Mambo Mengi ya tamaa za Mali na Mapenzi ni Mtu Smart.

 

Mtandao huu unamuombe kila lenye kheri kwenye mafanikio yake ya kucheza ligi kuu kwa mara ya kwanza kwenye histori ya maisha yake.

 

 

Dirisha kubwa la Usajri nchini lilifunguliwa Julai 1 na linafungwa Julai 31 huku pazia la ligi kuu likirajiwa kuzinduliwa Agost 13 kwa mchezo wa ngao ya Jamii kwa mpambano wa watani wa Jadi Simba na Yanga. huku ligi hiyo ikitarajiwa kuanza Agost 17.

              

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...