WAGALATIA 5-17
“Kwa sababu Mwili hutamani,ukishindana na roho na roho kushindana na mwili,kwa Maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya Mnayotaka” Hilo ndilo neno letu la leo Jumapili ya Julai 31.
Ujumbe huyo wa Mungu unatufundisha kwamba kuna vita kubwa ya matamanio kati ya Mwili na Roho.
Tunapaswa kuyashinda matamanio ya Mwili ili tubaki kuwa na roho safi jambo ambalo litatupa tiketi ya kufika Peponi.
Kuna baadhi ya watu wanakosema wakisema nafanya mema ili niende mbinguni nawakumbusha kwamba sote tutakwenda mbinguni sisi wenye dhambi na tusio na dhambi.
Tukifika huko matendo yetu ndio yatakayotuingia Peponi au Jehanamu ya Milele,hukumu hiyo itatenganisha, Mafuta na Maji, Magugu na Ngano, wenye dhambi na wasio na dhambi.
Kumbe basi matendo yetu ndio yatakayotupeleka Peponi au Motoni hivyo hata uzikwe na jeneza la dhahabu kama matendo yako yatakuwa ya dhambi hilo jeneza au wengi wawatu waliokuja kukuzika hayo hayata badilisha hukumu ya Mungu juu ya matendo yako uliyoyafanya ukiwa hai.
Baada ya kupita hukumu hiyo isiyo na upendeleo wenye dhambi tutatupa jehanamu kwenye hukumu ya Milele na wenye haki tutaweka Poponi kwenye raha za Milele.
Natambua roho iradhi kuyashinda matamanio lakini Mwili ni dhaifu, hivyo nakusia na kuihusisi pia nafsi yangu tusikubali tushindwa na matamanio ya Mwili yatakayotuingia kwenye hukumu ya Milele.
Tamaa zinazo zungumzia hapo ni pamoja na tama za mwili, Mali na dhuruma
No comments:
Post a Comment