“Basi wekeni Mbali Uovu
wote na hila yote na unafiki na husuda na Masingizio yote.
Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa ili
kwa hayo mpate kuukulia wokovu” Maneno Matakatifu kutoka 1Petro 2. 1-2.
Neno hilo la Mungu linatufundisha yafuatayo,tuache Uovu, Pili
tudumu kwenye Wokovu tutakapoimaliza safari yetu ya hapa duniani.
Kumbe basi tunakumbushwa kwamba Pesa zetu, Mali zile watoto
wetu au ndoa zetu haziwezi kutupeleka Peponi bali Wokovu ndio pekee utakao
tupeleka Peponi.
Usijidanganye kwamba Kuishi nyumba Moja na Askofu,
Padri au Mchungaji kutakupa tiketi ya kufika Pepoli ‘No’, Matendo yako mema
ndio yatakayokupa kibali cha kufika Peponi.
Pia usijidanganye kwamba kuolewa na Askofu au Mchungaji ndoa hiyo
itakupa kibali cha kufika Peponi hapana, nakukumbusha matendo yako Mema ndiyo
pekee yatakayo kufikisha kwenye Pepo ya Mwenyezi Mungu.
Hali kadharika Kuwa kiongozi wa dini Askofu, Padri,
Mchungaji, Mwinjilisti, Kasisi, Katekista au Palishiweka cheo hicho hakikupi
tiketi ya kufika Peponi Matendo yako Meme ndio pekee yatakayofikisha kwenye
Uzima wa Milele.
Tena nyinyi viongozi wa dini mkienda kinyume na
Wokovu mtahukumiwa zaidi mtaingizwa Jehanamu na kutupwa kwenye moto mkali
Biblia ilionya.
’Ole wao watakao
kuwa Vugu vugu Moto si Moto baridi si baridi.’
Ninayo yakemea kwa wenzangu nayakemia pia kwenye nafsi yangu,
nami najichana ‘Live’ najipiga ngumi kwenye mshono.
Shekidele
nisijidanganye kwamba kitendo cha
kuruhusu kanisa kujengwa eneo la nyumba
yangu kitanipa tiketi ya kufika Peponi
hapana.
Japo namini
hilo nalo ni jambo jema laki Pekee haliwezi kunipa kibari cha kufika Peponi
natakiwa kuendeleza mema zaidi siku zote za maisha yangu mpaka hapo Mungu
atakapo kata punzi yangu ya kuishi hapa chini ya jua.
Miaka ya hivi karibuni Uongozi wa Kanisa la Tanzania
Assemblies Of God’T.A.G Jimbo la Morogoro walifika nyumbani na kuomba kujenga
Kanisa nje ya nyumba yangu na mimi bila kinyongo niliwakubaria kwa moyo mmoja
ambapo mpaka sasa huduma inaendelea kwenye kanisa hilo.
Wiki
iliyopita kulifanyika Mkutano Mkubwa wa lnjiri nje ya kanisani hilo ambapo kuna
uwanja mkubwa.
Mungu atusaidie tusitumie nguvu na akili nyingi kuyatafuta na kuyatamani Maisha ya dunia.
Kwa Neema
zake atuongoze tutumie akili na nguvu nyingi kuyatafuta Maisha ya Mbinguni ambayo tunaamini ndio
maisha marefu zaidi tofauti na maisha ya hapa duniali yaliyojaa shida na damu nyingi.