Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, April 26, 2022

WAMASAI WADAI HAJI MANARA AMEVAA VAZI LA KIMASAI LA KIKE.


Mwandishi wa Mtandao huu[kushoto] akimpongeza Kiongozi Mkuu wa Kabila la Wamasai anayeongoza wamasai wa Mikoa ya Morogoro. Dodoama. Singida, Manyara na lringa Mara.

 

 Shughuri hiyo ya kumsimika Kiongozi huyo Mkuu wa kabila la Wamasai mwenye cheo cha ‘Raibon’ alifanyika Wilayani Kilosa.

Hafra  hiyo ilifanyika kwenye zizi la Ng’ombe ilihudhuriwa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Serikali ya Mkoa wa Morogoro.

 

Akiwemo Mkuu wa Mkoa na aliyekuwa katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka.  A. Shaka ambaye kwa sasa ni Katibu Mwenyezi wa CCM Taifa.

 

Mara baada ya kusimikwa kiongozi huyo alipewa ulinzi Mkali wa Jeshi la Polisi chini ya OCD wa Kilosa kulia aliyevaa Kaunda Suti.



 ....Mwandishi wa Mtandao huu kushoto akisalimiana na baba yoyo


 

Na Dunstan Sherkidele,Morogoro.

 

BAADHI ya Wamasai wameibuka na kudai  vazi la Kimasai ambalo Msemaji machachari wa Yanga Haji Manara alilivaa jana ni la Kike.

 

Wakati Mwandishi wa Mtandao huu anamsikiliza Haji Kupitia Luninga kwenye baa moja aliyopo pande a Mji Mpya ambayo inamilikiwa na Mmasai akihamasisha mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kwenye gemu yao dhidi ya Simba itakayopigwa Jumamosi  Saa 11 jioni.

 

Alijitokeza Kijana mmoja wa kimasai  akidai vazi la kimasai alilovaa Haji ni la Kike, baada ya kusikia hivyo Mwandishi wa habari hizi alimsogelea Kijana huyo alipotakiwa kuthibisha jambo hilo alisema.

 

“Mimi ni Yanga damu siwezi kumnanga msemaji wa timu yangu lakini ukweli ni kwamba Vazi hili alilovaa Haji ni la Kike na sehemu kumbwa ya mapambo hasa hilo la kichwani na shingoni ni mapambo ya Mama yoyo labda hilo Pambo la mkononi pekee ndio  la Kiume kama huamini Shekidele mulize Mmasai yoyote atakuthibitishia hilo”alisema Kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina Moja la Moses.

 

 

 Juhudi za Mwandishi wa Mtandao huu za kumpata Haji Manasa kuzungumzia jambo hilo ziligonga Mwamba ingawa juhuzi za kumtafuta bado zinaendelea ili tupate ufafanuzi kutoka kwake.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...