Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, April 24, 2022

UJUMBE WA NENO LA MUNGU LEO JUMAPILI YA APRIL 24.



 


 

“Basi wekeni Mbali Uovu  wote na hila yote na unafiki na husuda na Masingizio yote.  

 

Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa  yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu” Maneno Matakatifu kutoka 1Petro 2. 1-2.

 

Neno hilo la Mungu linatufundisha yafuatayo,tuache Uovu, Pili tudumu kwenye Wokovu tutakapoimaliza safari yetu ya hapa duniani.

 

Kumbe basi tunakumbushwa kwamba Pesa zetu, Mali zile watoto wetu au ndoa zetu haziwezi kutupeleka Peponi bali Wokovu ndio pekee utakao tupeleka Peponi.

 

 

Usijidanganye kwamba Kuishi nyumba Moja na Askofu, Padri au Mchungaji kutakupa tiketi ya kufika Pepoli ‘No’, Matendo yako mema ndio yatakayokupa kibali cha kufika Peponi.

 

Pia usijidanganye kwamba  kuolewa na Askofu au Mchungaji ndoa hiyo itakupa kibali cha kufika Peponi hapana, nakukumbusha matendo yako Mema ndiyo pekee yatakayo kufikisha kwenye Pepo ya Mwenyezi Mungu. 

 

Hali kadharika Kuwa kiongozi wa dini Askofu, Padri, Mchungaji, Mwinjilisti, Kasisi, Katekista au Palishiweka cheo hicho hakikupi tiketi ya kufika Peponi Matendo yako Meme ndio pekee yatakayofikisha kwenye Uzima wa Milele.

 

 

Tena nyinyi viongozi wa dini mkienda kinyume na Wokovu mtahukumiwa zaidi mtaingizwa Jehanamu na kutupwa kwenye moto mkali Biblia ilionya.

’Ole wao  watakao kuwa Vugu vugu Moto si Moto baridi si baridi.’

 

Ninayo yakemea kwa wenzangu nayakemia pia kwenye nafsi yangu, nami najichana ‘Live’ najipiga ngumi kwenye mshono.

 

 

 Shekidele nisijidanganye kwamba kitendo  cha kuruhusu kanisa kujengwa  eneo la nyumba yangu kitanipa  tiketi ya kufika Peponi hapana.

 

 Japo namini hilo  nalo ni jambo jema laki Pekee  haliwezi kunipa kibari cha kufika Peponi natakiwa kuendeleza mema zaidi siku zote za maisha yangu mpaka hapo Mungu atakapo kata punzi yangu ya kuishi hapa chini ya jua.

 

Miaka ya hivi karibuni Uongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God’T.A.G Jimbo la Morogoro walifika nyumbani na kuomba kujenga Kanisa nje ya nyumba yangu na mimi bila kinyongo niliwakubaria kwa moyo mmoja ambapo mpaka sasa huduma inaendelea kwenye kanisa hilo.

 Wiki iliyopita kulifanyika Mkutano Mkubwa wa lnjiri nje ya kanisani hilo ambapo kuna uwanja mkubwa.

Mungu atusaidie tusitumie nguvu na akili nyingi  kuyatafuta na kuyatamani Maisha ya dunia.

 Kwa Neema zake atuongoze tutumie akili na nguvu nyingi kuyatafuta  Maisha ya Mbinguni ambayo tunaamini ndio maisha marefu zaidi tofauti na maisha ya hapa duniali  yaliyojaa shida na damu nyingi.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...