Katibu
Mkuu wa MRFA Mch Kimbawala akizungumza na timu shirikia mara baada ya
kuzindua mashindano hayo. Picha no 3 ni Makundi 4 ya timu shiriki
wenyeji na waalikwa.
Baadae
Picha za matukio ya gemu ya ufunguzi kati ya Moro Kids na Black Viba
zitaruka hewani hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa’MRFA’ Mch. Emmanuel Kimbawala ameupongeza Uongozi wa Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro’MDFA’ kwa kutii maagizo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF’ ya kuzitaka wilaya zote nchini kuandaa michuano ya Vijana na Soka la Wanawake kwenye Maeneo yao.
Akizungumza kwenye Ufunguzi wa Michuano hiyo inayofanyika uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro Mchungaji Kimbawala alisema.
“Naupongeza Uongozi wa Chama cha Soka Wilaya ya Morogoro kuandaa mashindano haya ambayo ni maagizo kutoka TFF waliotupatia sisi Viongozi wa Mkoa na sisi tukatoa maagizo kwa wachini yetu kwa maana ya Wilaya”alisema Kimbawala na kuongeza.
“ Kwa upande wenu nyinyi Vijana hii ni fursa ya kuibua Vipaji vyenu kwa sasa mpira unalipa vizuri na niwaibie siri kuna mawakala kibao wanafuatilia mashindo haya”alisema Katibu huyo ambaye kitaaluma ni Mwalimu.
Michuano hiyo ya Vijana chini ya Miaka 20 inayojulikana kwa jina la ‘Under Twenty Legue’ inashirikisha timu 25 huku timu 4 zikitoka Wilaya nyingine baada ya maombi yao kuomba kushiriki ligi hiyo kukubaliwa na kamati ya ligi.
Timu hizo ni Pwani Sporty Foundation na Ruvu Shooting kutoka Mkoa wa Pwania. Kilombero Soccer Net kutoka Wilaya ya Kilombero na Mtibwa Sugar Kutoka Wilaya ya Mvomero.
No comments:
Post a Comment