Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, January 31, 2022

TANZIA. YALIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI, MMENGUAJI WA BAND YA MAISHA MAPYA AFARIKI DUNIA.

                                Tatu Bongo enzi za Uhai wake
Kiongozi wa Maisha Mapya Pugi’Kushoto’ akimtambulisha Tatu Mach 11 2021 kwenye ukumbi mmoja uliopo pande za Kichangani.


Agost 8 Pugi alifanya sherehe ua kumbikizi yake ya kuzaliwa wakati band hiyo inapafoni. Pichani Pugi kushoto akimrisha keki Tatu Bongo.


          Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.

Kama kawaida mwishoni mwa wiki Mlala nje  alizunguka  kumbi mbali mbali za Starehe Mkoani Morogoro kusaka Matukio.

Kwa masikitiko Makubwa Mlala nje akiwa kwenye shoo ya Band ya Maisha Mapya  maeneo ya Mazimbu, Kiongozi wa band hiyo Abubakar Pugi akiwatangazia Mashabiki  Kifo cha Mnenguaji Mahiri wa kike wa band hiyo Tatu Bauka Maarufu ‘Tatu Bongo’.

 

Taarifa za kifo hicho ziliwastua mashabiki wa band hiyo ambapo wengi wao walipanda jukwaani na kutoa pesa kama Rambi rambi zao kwa familia ya Marehemu.

 

Baada ya tangazo hilo Mlala nje alizungumza na Kiongozi wa band hiyo Pugi ambapo alisema Mnenguaji wake alifariki dunia Alhamis iliyopita  nyumbani kwake Dar na kuzikwa siku iliyofuta’ljumaa’ Makaburi ya Mburahati Dar.

”Sisi kama Maisha Mapya kupitia Group letu la Whatsap ambalo hata wewe Shekidele ni Mwanachama tumechanga pesa, tunashukuru mashabiki nao wameguswa amechangia hivyo tutakusanya pesa hizi na sisi viongozi tutazipeleka Dar kwa familia ya Tatu ambaye ameacha Mtoto mmoja”alisema Pugi ambaye ni miongoni mwa wamiliki wa band hiyo Pendwa Mkoani Morogoro.

 

 Marehemu Tatu alitamburishwa rasmi kujiunga na band hiyo Mach 11- 2021 akitokea band ya FM Academia ya Jijini Dar.

Akizungumza na Mlala Nje muda mfupi baada ya kutambulishwa, Tatu alisema katika Maisha yake ya Muziki amezitumikia band nyingi kubwa za jijini Dar.

”Nimeamua kubadili upepo wa Maisha nimekuja kujiunga na bend ya Maisha Mapya nikitokea AF Academia”alisema Mnenguaji huyo aliyeacha Mtoto mmoja wa kike.

“Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimidiwe. Umemaliza Mwendo Mpambanaji  Tatu Bongo tutaonana badae”

 

                    

 

Thursday, January 27, 2022

GARI LASAFIRISHWA KWENYE MKOKOTENE.


 


 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Mwenyendesha Mkokotene alinaswa hivi karibuni alisafirisha gari bovu kutoka kwenye Magereji yaliyopo maeneo ya barabara ya Tumbaku akilipeleka kata ya Mji Mpya Mkoani hapa, kwa lengo la kwenda kuuzwa kama Chuma Chakavu.

 

Kuna taarifa zinadai kwamba kufuatia kukidhiri kwa wizi wa mara kwa Mara kwenye Miundombinu ya serikali, Kama Vile alama za barabaranai, Kingo za Madaraja,na Taa za barabarani.biashara ya Vyuma chakavu imepigwa marufuku kwa lengo la kulinda Miundombinu hiyo.

Siku za hivi karibuni Vibaka walivamia nyumbani kwa Mlemavu Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo Majira ya Usiku na kuiba baiskeli yake ya mataili 3.   Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mlemavu huyo wa Miguu [jina linahifadhiwa kwa sababu za kiuwanaume]alisema.

 

”Kama unavyoona Mlango wa chumba changu ninachoishi na mke wangu ni Mwembemba baiskeli  haikuweza kupita hivyo Miaka yote nilikuwa nailaza hapa nje ya Mlango wa chumba changu”alisema Mlemavu huyo na kuongeza.

 

 “Nyumba hii haina uzio iko wazi Jamaa wamekuja usiku wameichukua baiskeli yangu wameenda hapo Mtoni wakaikata kata na msumeno wakaenda kuuza Vyuma Chakavu kulipokucha nilipofungua Mlango sikuiona baiskeli Majirani wakaniambia walipoenda kuchota Maji mtoni wameona mabaki ya vyuma eneo hilo la Mtoni ndio hivyo tena wamechukua miguu yangu kwa sasa niko tu ndani sitembei ndio Maana hunioni Mjini”alisema Mlemavu huyo.

 

Kufutaia hali hiyo Mwandishi wa Mtandao huu aliguswa na kuamua kuendesha harambee kwenye Mtandao huu na kufanikiiwa kupata pesa za kumnunulia  baiskeli nyingine ingawa ilikuwa imetumika.

Mtandao huu unawashukuru wote waliojitolea kufanikisha zoezi hilo, Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema atawalipa Mara dufu pale mlipopunguza.

Monday, January 24, 2022

KUMBUKIZI.


 


Matajiri wa Mkoa wa Morogoro, Kulia Mh Abdulaziz Mohamed Abood ambaye anamiliki Mabasi ya Kampuni ya Abood, akisalimiana na  Mohamed Hood ambaye anamiliki Kampuni ya Mabasi ya Hood.

 

Makada hao wa CCM walinaswa na Kamera za Mtandao huu kwenye Moja ya Mikutano ya Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’ iliyofanyika eneo la Maskani Manispaa ya Morogoro.

 

Abood  ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kupitia CCM huku  Mzee Hood akiwa  diwani Mstaafu wa Kata ya Mji Mkuu Kwa leseni ya CCM.

 

Waarabu hawa Wazaliwa wa Mkoa wa Morogoro enzi hizo walikuwa na Upinzani Mkali wa Kibiashara, kabla ya Upinzania huo kufa baada ya Mabasi ya Hood kutoonekana barabarani huku yale ya Abood ‘King Of The Road’ yaliendelea kusambaa kwa kasi Mikoa mbali mbali ya Tanzania.

Thursday, January 20, 2022

UTALII WA NDANI.

Nimetembelea Jumba la makumbusho ya Azimio la Arusha ambalo liko eneo la Kaloleni Jijini Arusha.
....Niko kwenye Mnara  uliopo jirani na Jengo hilo la Makumbusho ya Azimio la  Arusha nikijianda kuingia kwe nye Mjengo huo

 ....Hili ndio jumba ambalo ndani yake kuna Makumbusho mbali mbali yakiyemo ya Azimo la Arusha



Wednesday, January 19, 2022

UDAKUZ SPESHO. BODA BODA ACHEKEZWA NA POLISI HOJA ZAKE NZITO ZA MUWEKA HURU


 Hii ni Pikipiki ya Mdakuz wa Mtandao huu aliinunua June 8 2021 ikiwa na namba aligoma kununua Pikipiki bila kupewa Document.

.

                       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nikiwatakia Kheri ya Mwaka Mpya 2022.

 

Kama kawaida Mdau wa Mtandao Pendwa wa Shekidele tunakutana tena leo January 19 2022 kwenye kipengele chetu cha Udakuz wa Kitaa kinachoruka hewani kila wiki.

 

Wiki iliyopita Mdakuz  akiwa Mtaa wa Makongoro  katikati ya Mji wa Morogoro akisaka Matukio, alinasa tukio la Polisi wa doria wanaotumia  Pikipiki Maarufu ‘Foda Fasta’ wakimchekecha kwa Maneno dereva wa Pikipiki Maarufu ‘boda boda’.

Baada ya kuona tukio hilo Mdakuz wa Mtandao huu akiwa na Pikipiki yake alisogea eneo la tukio na kutega Msikio y kama Antena za King’amuzi cha Wasambaa Tv.

               MSALA WEMYEWE ULIKUWA HIVI.

Boda boda huyo ambaye kwa maelezo yake alidai kwamba muda huo alitoka dukani kununua Pikipiki hiyo alikamatwa  kwa kosa la kuendesha Pikipiki bila kuwa na namba ya Usajiri’Pret Number’.

 

Boda  huyo aliyekuwa na mwenzake kwa pamoja waligoma kukamatwa kwa maana ya kuwakabidhi Pikipiki hiyo Wanausalama hao kwa lengo la kuipeleka kituoni kwa hoja kwamba hawana kosa.

 

Wakidai kwamba Muda huo walitoka dukani kununua Pikipiki hiyo wakielekea nyumbani kuihifadhi mpaka watakapopewa   kadi ya Pikipiki na Pret Number kwenye duka walilonunua chombo hicho cha Moto.  

 

Maafande hao wakawaeleza kwamba ni kosa kisheria kuendesha chombo cha Moto kisichokuwa na namba.

“Pia sisi Polisi jukumu letu ni kulinda raia na Mali zao hivyo ikitokea Pikipiki yako imeibiwa ukaja kuripoti Polisi tutaitafutaje wakati utakuwa huna alama yoyote itakayotupa wepesi wa kuitambua”walisema Maafande hao

 

Maafande hao baada ya kuona watu wanazidi kujaa eneo hilo huku Mwandishi wa Mtandao huu naye akizidi kutega Antena zake waliamua kuwaachia  kwa sharti kwamba wasiendelee kuitumia Pikipiki hiyo mpaka watakapo pata namba.

 

Kabla Mapolisi hao wajaondoka  Mdakuzi  alifanikiwa kuzungumza nao kuhusiana na tukio hilo.

 

” lko hivi  kila siku tunakamata hizi Pikipiki mpya zinazotembea barabarani bila namba ni makosa  kisheria wanatakiwa wakaiweke ndani mpaka watakapo pata hizo Document”walisema Wanausalama hao na kuondoka zao.

 

Kwa Upande wao boda boda hao walipohojiwa  walisema”Sio kama tumegoma kukamatwa hapana yule afande baada ya kuongea sana tena kwa jazba nikamueleza kwa upole anipe na mimi nafasi  ya kujieleza aliponipa nafasi nikamueleza kwamba tumetoka dukani muda huu kununua hii pikipiki  kama inavyoonekana hata manaironi hayajabanduliwa.

Pret Number na Kadi tumeambiwa tukachukue baada ya wiki moja nikamuonyesha risti ya manunuzi na siku ya kwenda kuchukua hiyo kadi na namba.

 

Akasema pikipiki nimenunua toka juzi nikamwambia aje kwenye Dash Bord angaliye  haijatembea hata kilometa Moja alipoangalia akaamini na kutuachia”alisema boda huyo na kuongeza.

 

Hoja kwamba Pikipiki haikupaswa kutembea bila namba sasa niliponunua ningeibeba kichwani mpaka nyumbani?. Muda huu tunaenda nyumbani kuhifadhi mpaka tutakapo pata namba kama walivyotuamulu”walisema boda boda huyo.

 

 Uchunguzi uliofanywa na Mdakuzi umebaini kwamba Maafande hao walikuwa sahihi kuwachekecha boda boda huyo kwani ni kweli kwa sasa ukinunua Pikipiki Docoment unakabidhiwa  baada ya wiki moja au mbili  

 

 Kwa ukali wa Maisha  baadhi ya madereva wa boda boda huwa hawasuburi mpaka wapate namba hufanya kazi bila namba jambo ambalo ni kinyume cha sheria za Usalama barabarani.

                           USHAURI KWA MAMLAKA HUSIKA

 Hivi sharia zinasemaje kwenye hilo mtu anaweza kuza chombo cha Moto bila kutoa Docoment Muhimu kwa mteja ambaye ambaye ni lazima baada ya kununua chombo hicho lazima asafiri nacho. Wateja wengi wa Pikipiki hutoka Wilayani hivyo Mteja ananunua Pikipiki hapa Mjini anasafiri nayo Mpaka mvomero au Kisaki umbali wa takribani kilometa 90 mpaka 100 bila Pikipiki kuwa na Namber ya Usajiri wala Kadi.

 

 Ushauri kwa Mamlaka husika wajaribu kuongea na wenye maduka yanayouza Pikipiki kama Pikipiki haina Docoment wasiruhusiwe kuziuza kwa wateja ili kuondoa kadhia hiyo Mtaani.

               


AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...