Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, January 19, 2022

UDAKUZ SPESHO. BODA BODA ACHEKEZWA NA POLISI HOJA ZAKE NZITO ZA MUWEKA HURU


 Hii ni Pikipiki ya Mdakuz wa Mtandao huu aliinunua June 8 2021 ikiwa na namba aligoma kununua Pikipiki bila kupewa Document.

.

                       Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nikiwatakia Kheri ya Mwaka Mpya 2022.

 

Kama kawaida Mdau wa Mtandao Pendwa wa Shekidele tunakutana tena leo January 19 2022 kwenye kipengele chetu cha Udakuz wa Kitaa kinachoruka hewani kila wiki.

 

Wiki iliyopita Mdakuz  akiwa Mtaa wa Makongoro  katikati ya Mji wa Morogoro akisaka Matukio, alinasa tukio la Polisi wa doria wanaotumia  Pikipiki Maarufu ‘Foda Fasta’ wakimchekecha kwa Maneno dereva wa Pikipiki Maarufu ‘boda boda’.

Baada ya kuona tukio hilo Mdakuz wa Mtandao huu akiwa na Pikipiki yake alisogea eneo la tukio na kutega Msikio y kama Antena za King’amuzi cha Wasambaa Tv.

               MSALA WEMYEWE ULIKUWA HIVI.

Boda boda huyo ambaye kwa maelezo yake alidai kwamba muda huo alitoka dukani kununua Pikipiki hiyo alikamatwa  kwa kosa la kuendesha Pikipiki bila kuwa na namba ya Usajiri’Pret Number’.

 

Boda  huyo aliyekuwa na mwenzake kwa pamoja waligoma kukamatwa kwa maana ya kuwakabidhi Pikipiki hiyo Wanausalama hao kwa lengo la kuipeleka kituoni kwa hoja kwamba hawana kosa.

 

Wakidai kwamba Muda huo walitoka dukani kununua Pikipiki hiyo wakielekea nyumbani kuihifadhi mpaka watakapopewa   kadi ya Pikipiki na Pret Number kwenye duka walilonunua chombo hicho cha Moto.  

 

Maafande hao wakawaeleza kwamba ni kosa kisheria kuendesha chombo cha Moto kisichokuwa na namba.

“Pia sisi Polisi jukumu letu ni kulinda raia na Mali zao hivyo ikitokea Pikipiki yako imeibiwa ukaja kuripoti Polisi tutaitafutaje wakati utakuwa huna alama yoyote itakayotupa wepesi wa kuitambua”walisema Maafande hao

 

Maafande hao baada ya kuona watu wanazidi kujaa eneo hilo huku Mwandishi wa Mtandao huu naye akizidi kutega Antena zake waliamua kuwaachia  kwa sharti kwamba wasiendelee kuitumia Pikipiki hiyo mpaka watakapo pata namba.

 

Kabla Mapolisi hao wajaondoka  Mdakuzi  alifanikiwa kuzungumza nao kuhusiana na tukio hilo.

 

” lko hivi  kila siku tunakamata hizi Pikipiki mpya zinazotembea barabarani bila namba ni makosa  kisheria wanatakiwa wakaiweke ndani mpaka watakapo pata hizo Document”walisema Wanausalama hao na kuondoka zao.

 

Kwa Upande wao boda boda hao walipohojiwa  walisema”Sio kama tumegoma kukamatwa hapana yule afande baada ya kuongea sana tena kwa jazba nikamueleza kwa upole anipe na mimi nafasi  ya kujieleza aliponipa nafasi nikamueleza kwamba tumetoka dukani muda huu kununua hii pikipiki  kama inavyoonekana hata manaironi hayajabanduliwa.

Pret Number na Kadi tumeambiwa tukachukue baada ya wiki moja nikamuonyesha risti ya manunuzi na siku ya kwenda kuchukua hiyo kadi na namba.

 

Akasema pikipiki nimenunua toka juzi nikamwambia aje kwenye Dash Bord angaliye  haijatembea hata kilometa Moja alipoangalia akaamini na kutuachia”alisema boda huyo na kuongeza.

 

Hoja kwamba Pikipiki haikupaswa kutembea bila namba sasa niliponunua ningeibeba kichwani mpaka nyumbani?. Muda huu tunaenda nyumbani kuhifadhi mpaka tutakapo pata namba kama walivyotuamulu”walisema boda boda huyo.

 

 Uchunguzi uliofanywa na Mdakuzi umebaini kwamba Maafande hao walikuwa sahihi kuwachekecha boda boda huyo kwani ni kweli kwa sasa ukinunua Pikipiki Docoment unakabidhiwa  baada ya wiki moja au mbili  

 

 Kwa ukali wa Maisha  baadhi ya madereva wa boda boda huwa hawasuburi mpaka wapate namba hufanya kazi bila namba jambo ambalo ni kinyume cha sheria za Usalama barabarani.

                           USHAURI KWA MAMLAKA HUSIKA

 Hivi sharia zinasemaje kwenye hilo mtu anaweza kuza chombo cha Moto bila kutoa Docoment Muhimu kwa mteja ambaye ambaye ni lazima baada ya kununua chombo hicho lazima asafiri nacho. Wateja wengi wa Pikipiki hutoka Wilayani hivyo Mteja ananunua Pikipiki hapa Mjini anasafiri nayo Mpaka mvomero au Kisaki umbali wa takribani kilometa 90 mpaka 100 bila Pikipiki kuwa na Namber ya Usajiri wala Kadi.

 

 Ushauri kwa Mamlaka husika wajaribu kuongea na wenye maduka yanayouza Pikipiki kama Pikipiki haina Docoment wasiruhusiwe kuziuza kwa wateja ili kuondoa kadhia hiyo Mtaani.

               


No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...