Kiongozi wa Maisha Mapya Pugi’Kushoto’ akimtambulisha Tatu Mach 11 2021 kwenye ukumbi mmoja uliopo pande za Kichangani.
Agost 8 Pugi alifanya sherehe ua kumbikizi yake ya kuzaliwa wakati band hiyo inapafoni. Pichani Pugi kushoto akimrisha keki Tatu Bongo.
Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.
Kama kawaida mwishoni mwa wiki Mlala nje alizunguka kumbi mbali mbali za Starehe Mkoani Morogoro kusaka Matukio.
Kwa masikitiko Makubwa Mlala nje akiwa kwenye shoo ya Band ya Maisha Mapya maeneo ya Mazimbu, Kiongozi wa band hiyo Abubakar Pugi akiwatangazia Mashabiki Kifo cha Mnenguaji Mahiri wa kike wa band hiyo Tatu Bauka Maarufu ‘Tatu Bongo’.
Taarifa za kifo hicho ziliwastua mashabiki wa band hiyo ambapo wengi wao walipanda jukwaani na kutoa pesa kama Rambi rambi zao kwa familia ya Marehemu.
Baada ya tangazo hilo Mlala nje alizungumza na Kiongozi wa band hiyo Pugi ambapo alisema Mnenguaji wake alifariki dunia Alhamis iliyopita nyumbani kwake Dar na kuzikwa siku iliyofuta’ljumaa’ Makaburi ya Mburahati Dar.
”Sisi kama Maisha Mapya kupitia Group letu la Whatsap ambalo hata wewe Shekidele ni Mwanachama tumechanga pesa, tunashukuru mashabiki nao wameguswa amechangia hivyo tutakusanya pesa hizi na sisi viongozi tutazipeleka Dar kwa familia ya Tatu ambaye ameacha Mtoto mmoja”alisema Pugi ambaye ni miongoni mwa wamiliki wa band hiyo Pendwa Mkoani Morogoro.
Marehemu Tatu alitamburishwa rasmi kujiunga na band hiyo Mach 11- 2021 akitokea band ya FM Academia ya Jijini Dar.
Akizungumza na Mlala Nje muda mfupi baada ya kutambulishwa, Tatu alisema katika Maisha yake ya Muziki amezitumikia band nyingi kubwa za jijini Dar.
”Nimeamua kubadili upepo wa Maisha nimekuja kujiunga na bend ya Maisha Mapya nikitokea AF Academia”alisema Mnenguaji huyo aliyeacha Mtoto mmoja wa kike.
“Bwana ametoa na Bwana ametwa jina lake lihimidiwe. Umemaliza Mwendo Mpambanaji Tatu Bongo tutaonana badae”
No comments:
Post a Comment