Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, November 29, 2021

WANANCHI MORO WAVUTANA JUU YA MAREHEMU KUPEWA JINA LA HAYATI


 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Wiki iliyopita Mwandishi wa wa Mtandao huu akiwa mitaani akisaka matukio aliwashuhudia wananchi wakiwa kwenye mvutano makali juu ya Marehemu kuitwa hayati.
Upande mmoja alisema Marehemu kuitwa Hayati ni kiswahiri fasaha huku Upande wa pili ukidai kwamba Marehemu kuitwa hayati ni makosa makubwa.
Mvutano huo ulikamilika huku kila upande ukishikilia Msimamo wake, ili kupata majawabu ya uvutano huo Mwandishi wa habari hizi aliamua kumtafuta Mwenyekiti wa Usanifu wa Lugha na Ushahiri Tanzania’UKUTA’ Mkoa wa Morogoro Shehe Twaha Kiobya,[Pichani akihojiwa na Mtandao huu] alitoa jibu sahihi la jambo hilo huku akilitaja Baraza la Kiswahiri Tanzania’BAKITA’.
Clip Video ya mahojiano hayo yenye majibu ya swali hilo itaruka hewani hivi Punde hivyo nakusihi utembelea Mtandao huu muda wote.

Thursday, November 25, 2021

KUMBUKIZI YA MIAKA 5 YA KIFO CHA WAKALLA MAARUFU WA GLOBAL PUBLISHERS.

                     Marehemu Nasibu enzi za Uhai wake
Meneja Mkuu wa Global Abdallah Mrisho akizungumza kwenye mziba huo
Meneja Masoko wa Global Kivea akizungumza mbele ya jenera lililobeba mwili wa Marehemu
Vigogo hao wa Global waliofunga safari kutoka Dar Mpaka Moro kushiriki mazishi hayo wakiingia kwenye Noa yao wakirejea Dar
Kutoka Kushoto ni Laurence Kapande Mhasibu Mkuu wa Kampuni ya Global, Siafael Paulo Mhariri Mkuu wa gazeti la Ijumaa wikienda, Oscar Ndauka Mhariri Mtendaji Global na Abdallah Mrisho Meneja Mkuu Global Publishers
Mh Abbdas Mtemvu aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Dar

                                           Hussein Ngurungu


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.  Novembar 25 -2016 aliyekuwa wakalla Maarufu wa Magazeti ya Kampuni Pendwa ya Global Pubrishers Mkoani Morogoro Nassib Nassoro alifariki dunia.

 

Hivyo jana November 25 2021 Mpendwa wetu huyo ametimiza miaka 5 toka alivyoiaga dunia. 

 

Hayati Nassib ambaye pia alikuwa Mhasibu Mkuu wa Msikiti Mkuu wa ljumaa wa Kata ya Mwembesongo na Mjumbe wa kamati ya Ujenzi wa shule ya Msingi na Sekondari inayomilikiwa na Msikiti huo alizikwa katika Makaburi  ya Familia yao yaliyopo Kingolwira Manispaa ya Morogoro.

Kwenye Mazishi hayo watu wengi maarufu walishiriki akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke  Mh Abas Mtemvu, Mchezaji wa zamani wa Pan Afrika Hussein Ngurungu ambaye rekodi yake ya kuitumika timu ya taifa ya Tanzania’Taifa Star’ kwa miaka 10 mfurulizo haijavunjwa na mchezaji yoyote mpaka sasa.  

Tutakukumbuka daima Mpendwa wetu Nassib Mungu akupunguzie adhabu ya kabri na akupokee na kukuweka unapostahiri kulingana na maisha uliyoishi hapa ulimwengungu.

 

                         

BABA NA MWANA WASHINDWA KUINUSURU TIMU YAO KUSHUKA DARAJA.

Yohana Semkia kushoto akitoa maelekezo kwa wachezaji wa Pam Fc. Kulia ni kocha kuu wa timu hiyo Lulusi  Yohana Semkiwa



 

 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

BEKI Kisiki wa zamani wa timu ya Reli ya Morogoro’Kiboko ya Vigogo’ Yohana Semkiwa’Mgosi’ wiki iliyopita aliradhimika kuacha shughuri zake binafsi na kumsaidia Mtoto wake Lulusi Semkiwa kuinusuru timu  ya Pam Fc isishuke daraja.

 

Lilusi ni kocha Mkuu wa timu ya Pam Fc iliyoshiriki ligi daraja la Tatu Mkoa wa Morogoro na kujikuta ikifanya vibaya na kuangukia kwenye Play Off ya kupigania kutoshuka daraja.

 

Timu nyingine zilizoangukia  Play Off ni Eleven Killer na New Kings, huku timu za Mkundi United, Kihonda United, Moro Youths.

 

Tanzanite Academy,Lukobe Fc na Mgude Worries zenyewe zikisonga hatua inayofuata kungana na timu kutoka vituo vingine,timu za Kihonda Maghorofani. John  Bosco na Kinonko zewenye zikisubiri msimu ujao.

 

Toka mashindano hayo yalipoanza mwanzoni mwa mwezi huu Uwanja wa Saba Saba kituo cha Morogoro Mjini, Mwandishi wa Mtandao huu alihudhuria michuano hiyo na hajawahi kumuona Yohaya Semkia uwajani hapo.

 Majuzi ndipo alipomuona kwenye hatua ya Play Off akiwa kwenye benchi la Pam Fc iliyokipiga na New Kings akiwa bize kutoa maelekezo kwa wachezaji na mwisho wa mchezo huu Pam alinyukwa bao 2-1.

Wachambuzi wa Mambo walisikika wakisema Semkiwa aliamua kumsapoti Mtoto wake kuliokoa Jahazi la Pam lisizame.

 

Hata hivyo licha ya Mzee Semkiwa Kumsapote Mwanaye lakini bado timu hiyo ya Pam yenye Maskani yake Kata ya Kichangani iliendelea kufanya vibaya kwa kufungwa michezo yote 2 ya Play Off na kujikuta ikikata tiketi ya kuelekea ligi daraja la Nne msimu ujao.

 

Mara baa ya  timu hiyo kushuka daraja Mwandishi wa Mtandao huu alimfuta Mzee Semkiwa na alipohojiwa alikiri kufika kwenye michezo hiyo 2 ya Play Off kwa lengo la kumsapoti Mtoto wake.

”Mgos Shekidele ni kweli nimeonekana kwenye michezo hii ya Play Off lengo kuu ni kumsaidi Mtoto wangu ili timu yake isishuke daraja lakini kwa bahati mbaya licha ya kucheza vizuri kwenye michezo yote 2  bahati haikuwa yetu tumefungwa na kushuka daraja”alisema Semkiwa ambaye alikuwa beki wa kulia wa Reli ya Morogoro.

Alipoulizwa mtoto wake huyo ni wangapi kwenye uzao wake alisema ni  wanne akitanguliwa na wakubwa zake 3.

 

Kwa Mijibu wa taarifa zilizopo kwenye Group la Chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro ambalo Mwandishi wa Mtandao huu yumo,Kupitia Viongozi wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro kwenye ligi hiyo timu moja ya mwisho kwenye Play Off itashuka daraja hivyo baada ya michezo hiyo ya Play Off kutamatika jana kwa Pam kufungwa na Eleven Killer ni rasm timu hiyo imeshuka daraja.

                    

Sunday, November 21, 2021

NYUMBA YA MFANYABIASHARA MAARUFU MORO YATEKETEA KWA MOTO.

Mjengo huo wa kifahari ukiendelea kuteketea kwa Moto
Wananchi wakishuhudia tukio hilo kwa hudhuni kunbwa

Mmilkki wa Nyumba hiyi Yakuti Maiza azungumza na Mwandishi wa habari hizi eneo la tukio

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood kulia mwenye barakoa na diwani wa Kata ya Mji Mpya Mh Emmy Kiula  kwa pamoja wakimfariji Yakuti Maiza  mwenye Flana nyeuri kati


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 MJENGO wa kisasa wa Mfanyabiashara Maarufu Mkoani Morogoro Yakuti Maiza uliopo Mtaa wa Fumilwa B Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro umeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea jana Majira ya Mchana na kwamba hakuna mtu aliyepoteza Maisha wala kujeruhiwa ingawa sehemu kubwa ya Mali zilizomo ndani ya nyumba hiyo ziliteketea kwa Moto.

 

Akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu Mmiliki wa nyumba hiyo  Bw Maiza alisema Chanzo cha Moto huyo ni hitirafu ya Umeme iliyotokea kwenye moja ya chumba.  

“Shekidele kama unavyoona nyumba yangu inaungua na mpaka sasa watu wa faya wala Tanesco hawajafika licha ya kuwapa taarifa Mapema ofisi za Tanesco ziko hapo jirani hali kadharika Ofisi za Faya nazo haziko mbali sana na hapa kwangu”alisema Maiza Pichani mwenye flana nyeusi.

Alipoulziwa kama kuna mtu amejeruhiwa au kupoteza maisha kwenye tukio hilo  alijibu

 

”Tuna mshukuru Mungu hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa ingawa sehemu kubwa ya vitu vyangu vya thamani zilivyomo ndani zinaendelea kuteketea kwa Moto kama unavyoshuhudia”alisema Mfanyabiashara huyo huku akiwa na hudhuni kubwa. Wakati Mtandao huu ukiendelea kuwahoji watu mbali mbali Maafande wa  Kikosi cha Zima Moto na Mafundi wa Tanesco walifika eneo la tukio na kila mmoja walitimiza majukumu yake huku mafundi wa Tanesco wakipanga juu ya nguzo na kukata mawasiliano ya umeme yaliyoelekea kwenye nyumba hiyo.

 

Katika hatua nyingine mara baada ya kikosi cha Zima Moto na Uokoaji kufika eneo la tukio baadhi ya wananchi wakiongozwa na Abdallah Maiza ambaye ni mdogo wa Mmiliki wa nyumba hiyo kwa pamoja waliwatupi maneno Makali Maafande  wa Zima Moto huku kina mama wakilipiga gari la fanya kwa Khanga na Vitenge walivyo vya kwa maana ya kuwasirisha hasira zao kwa Maafande hao.

 

Hata hivyo Makamanda hao hawakujali maneno hayo badala yake  walikuwa bize kufunga Mipira na kuungamisha mashine za maji kutoka kwenye gari na kuzima Moto huyo ingawa Afande Mmoja alionekana kukerwa na Maneno hayo ya Shombo na kuamua  kujibishana na Dullah Maiza wakitaka kuzipacha kavu kavu.

 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Fumilwa B Said Jungu aliyekuwepo eneo la tukio alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye Mtaa wake.  

 

Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood na diwani wa kata ya Mji Mpya Mh Emmy Kiula walifika eneo la tukio na kumfariji Mkazi wao huyo aliyekumbwa na janga hilo la Moto.

 

Katika tukio lingine Fundi Maarufu wa Simu Kata ya Mji Mpya Mbaraka Mselemu alijitosa kwenye moto huo na kuokoa kitabu Kitakatifu cha Biblia na kwa miujiza ya Mwenyezi Mungu Mubaraka ambaye ni Muumini wa dini ya kiislama alitoka salama bila kujeruhiwa Popote.  

Clip Video za matukio yote hayo zitaruka hewani hivi Youtube ya Shekidele tv Online  na Global tv Online hivyo usicheze mbali na tv hizo  ushuhudie Mubashara kina mama wakilitandika gari la zima Moto na Khanga pamoja na Baraka kujitosa kwenye Moto nakufanikiwa kuikoa Biblia.

 

 

 

Thursday, November 18, 2021

UDAKUZI SPESHO. MREMBO AIBA SIMU DUKANI AKAMATWA NA C.C.TV CAMERA.


 


 

Na Mdakuzi wa Mtandao huu.

HII sio powa aisee, dada mmoja’Mrembo wa Viwango vya Kimataifa’ ambaye jina lake halikufahamika mara Moja juzi alipata aibu ya kufunga Mwaka 2021 na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2022 baada ya kukamatwa na kupokea kichapo ‘hevi’ akidaiwa kuiba  simu dukani.

 

Tukio hilo la aina yake lilitokea kwenye Mtaa wa Makongoro Manispaa ya Morogoro ambapo dada huyo Mwenye Shepu zake na rangi iliyokorea vizuri aliyesuka nywele za bei mbaya baada ya kudaiwa kukwapua simu hiyo alikimbizwa Polisi na wasamalia wema waliyomsulusu asiendele kupokea kichapo kutoka kwa raia wenye hasira kali.

 

Kama kawaida Mdakuzi wa Mtandao huu baada ya kutonywa na ‘Source’wake waliosambaa maeneo mengi ya Mkoa wa Morogoro alitinga eneo la tukio na kuzungumza na muza  duka hilo Bw  Frank Fredrick [Pichani] ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 

Alipotakiwa kuelezea kwa undani tukio hilo Fredrick alisema

”Huyo dada alitumia ujanja wateja walipokuwa wengi alikuja dukani akachagua chagua simu kisha akachukua  moja na kuisunda kwenye mkoba wake bila kujua kama hapa dukani kuna kamera za Ulinzi.

 

Alipotoka nje tulimfuata na kumtaka alipie simu aliyoichukua akagoma akidai kwamba hakuchukua simu tukamvuta ndani na kumuonyesha Picha za kamera zinavyomuonyesha akiiba simu hiyo tukaichukua huku wananchi wenye hasira wakiwemo wateja wakimshushia Kichapo tukamnusuru kwa kupiga simu Polisi ambao walifika fasta na kuondoka naye”alisema Muza duka huyo.

 

Alipoulizwa simu hiyo ‘Janja’ ina thamani ya kiasi gani Fredrick alisema inathamani ya shilingi laki mbili na nusu.

 

Wambeya wanaomfahamu mdada huyo wa Mujini walimtonya Mbeya wa Mtandao huu wakidai  Mrembo huyo ni Mjane Mumewe ni miongoni mwa watu waliopoteza Maisha kwenye ajari ya Mlipuko wa Lori la Mafuta uliotokea Agost 10- 2019 eneo la Msamvu Mkoani Morogoro na kuuza watu wanaokadiriwa kufika mia moja.

 

“Shekidele tukuongezee nyama kwenye Stori yako huyu dada tunamfahamu Mumewe ni Miongoni mwa watu waliokufa kwenye ajari ya Moto pale Msamvu”walisema wambeya hao wenye jinsia ya kike walioamua kumnanga live mwanamke mwenzao.

 

Kwa mtu yoyote mwenye umbeya wa Mtaa awasiliane  fasata na Fagio la Mtaa Mwandishi wa Mtandao huu kwa namba 0627 48 88 20.

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...