Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, November 18, 2021

UDAKUZI SPESHO. MREMBO AIBA SIMU DUKANI AKAMATWA NA C.C.TV CAMERA.


 


 

Na Mdakuzi wa Mtandao huu.

HII sio powa aisee, dada mmoja’Mrembo wa Viwango vya Kimataifa’ ambaye jina lake halikufahamika mara Moja juzi alipata aibu ya kufunga Mwaka 2021 na kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2022 baada ya kukamatwa na kupokea kichapo ‘hevi’ akidaiwa kuiba  simu dukani.

 

Tukio hilo la aina yake lilitokea kwenye Mtaa wa Makongoro Manispaa ya Morogoro ambapo dada huyo Mwenye Shepu zake na rangi iliyokorea vizuri aliyesuka nywele za bei mbaya baada ya kudaiwa kukwapua simu hiyo alikimbizwa Polisi na wasamalia wema waliyomsulusu asiendele kupokea kichapo kutoka kwa raia wenye hasira kali.

 

Kama kawaida Mdakuzi wa Mtandao huu baada ya kutonywa na ‘Source’wake waliosambaa maeneo mengi ya Mkoa wa Morogoro alitinga eneo la tukio na kuzungumza na muza  duka hilo Bw  Frank Fredrick [Pichani] ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 

Alipotakiwa kuelezea kwa undani tukio hilo Fredrick alisema

”Huyo dada alitumia ujanja wateja walipokuwa wengi alikuja dukani akachagua chagua simu kisha akachukua  moja na kuisunda kwenye mkoba wake bila kujua kama hapa dukani kuna kamera za Ulinzi.

 

Alipotoka nje tulimfuata na kumtaka alipie simu aliyoichukua akagoma akidai kwamba hakuchukua simu tukamvuta ndani na kumuonyesha Picha za kamera zinavyomuonyesha akiiba simu hiyo tukaichukua huku wananchi wenye hasira wakiwemo wateja wakimshushia Kichapo tukamnusuru kwa kupiga simu Polisi ambao walifika fasta na kuondoka naye”alisema Muza duka huyo.

 

Alipoulizwa simu hiyo ‘Janja’ ina thamani ya kiasi gani Fredrick alisema inathamani ya shilingi laki mbili na nusu.

 

Wambeya wanaomfahamu mdada huyo wa Mujini walimtonya Mbeya wa Mtandao huu wakidai  Mrembo huyo ni Mjane Mumewe ni miongoni mwa watu waliopoteza Maisha kwenye ajari ya Mlipuko wa Lori la Mafuta uliotokea Agost 10- 2019 eneo la Msamvu Mkoani Morogoro na kuuza watu wanaokadiriwa kufika mia moja.

 

“Shekidele tukuongezee nyama kwenye Stori yako huyu dada tunamfahamu Mumewe ni Miongoni mwa watu waliokufa kwenye ajari ya Moto pale Msamvu”walisema wambeya hao wenye jinsia ya kike walioamua kumnanga live mwanamke mwenzao.

 

Kwa mtu yoyote mwenye umbeya wa Mtaa awasiliane  fasata na Fagio la Mtaa Mwandishi wa Mtandao huu kwa namba 0627 48 88 20.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...