Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, November 21, 2021

NYUMBA YA MFANYABIASHARA MAARUFU MORO YATEKETEA KWA MOTO.

Mjengo huo wa kifahari ukiendelea kuteketea kwa Moto
Wananchi wakishuhudia tukio hilo kwa hudhuni kunbwa

Mmilkki wa Nyumba hiyi Yakuti Maiza azungumza na Mwandishi wa habari hizi eneo la tukio

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood kulia mwenye barakoa na diwani wa Kata ya Mji Mpya Mh Emmy Kiula  kwa pamoja wakimfariji Yakuti Maiza  mwenye Flana nyeuri kati


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 MJENGO wa kisasa wa Mfanyabiashara Maarufu Mkoani Morogoro Yakuti Maiza uliopo Mtaa wa Fumilwa B Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro umeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea jana Majira ya Mchana na kwamba hakuna mtu aliyepoteza Maisha wala kujeruhiwa ingawa sehemu kubwa ya Mali zilizomo ndani ya nyumba hiyo ziliteketea kwa Moto.

 

Akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu Mmiliki wa nyumba hiyo  Bw Maiza alisema Chanzo cha Moto huyo ni hitirafu ya Umeme iliyotokea kwenye moja ya chumba.  

“Shekidele kama unavyoona nyumba yangu inaungua na mpaka sasa watu wa faya wala Tanesco hawajafika licha ya kuwapa taarifa Mapema ofisi za Tanesco ziko hapo jirani hali kadharika Ofisi za Faya nazo haziko mbali sana na hapa kwangu”alisema Maiza Pichani mwenye flana nyeusi.

Alipoulziwa kama kuna mtu amejeruhiwa au kupoteza maisha kwenye tukio hilo  alijibu

 

”Tuna mshukuru Mungu hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa ingawa sehemu kubwa ya vitu vyangu vya thamani zilivyomo ndani zinaendelea kuteketea kwa Moto kama unavyoshuhudia”alisema Mfanyabiashara huyo huku akiwa na hudhuni kubwa. Wakati Mtandao huu ukiendelea kuwahoji watu mbali mbali Maafande wa  Kikosi cha Zima Moto na Mafundi wa Tanesco walifika eneo la tukio na kila mmoja walitimiza majukumu yake huku mafundi wa Tanesco wakipanga juu ya nguzo na kukata mawasiliano ya umeme yaliyoelekea kwenye nyumba hiyo.

 

Katika hatua nyingine mara baada ya kikosi cha Zima Moto na Uokoaji kufika eneo la tukio baadhi ya wananchi wakiongozwa na Abdallah Maiza ambaye ni mdogo wa Mmiliki wa nyumba hiyo kwa pamoja waliwatupi maneno Makali Maafande  wa Zima Moto huku kina mama wakilipiga gari la fanya kwa Khanga na Vitenge walivyo vya kwa maana ya kuwasirisha hasira zao kwa Maafande hao.

 

Hata hivyo Makamanda hao hawakujali maneno hayo badala yake  walikuwa bize kufunga Mipira na kuungamisha mashine za maji kutoka kwenye gari na kuzima Moto huyo ingawa Afande Mmoja alionekana kukerwa na Maneno hayo ya Shombo na kuamua  kujibishana na Dullah Maiza wakitaka kuzipacha kavu kavu.

 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Fumilwa B Said Jungu aliyekuwepo eneo la tukio alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwenye Mtaa wake.  

 

Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood na diwani wa kata ya Mji Mpya Mh Emmy Kiula walifika eneo la tukio na kumfariji Mkazi wao huyo aliyekumbwa na janga hilo la Moto.

 

Katika tukio lingine Fundi Maarufu wa Simu Kata ya Mji Mpya Mbaraka Mselemu alijitosa kwenye moto huo na kuokoa kitabu Kitakatifu cha Biblia na kwa miujiza ya Mwenyezi Mungu Mubaraka ambaye ni Muumini wa dini ya kiislama alitoka salama bila kujeruhiwa Popote.  

Clip Video za matukio yote hayo zitaruka hewani hivi Youtube ya Shekidele tv Online  na Global tv Online hivyo usicheze mbali na tv hizo  ushuhudie Mubashara kina mama wakilitandika gari la zima Moto na Khanga pamoja na Baraka kujitosa kwenye Moto nakufanikiwa kuikoa Biblia.

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...