Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, October 31, 2021

PADRI AIMWAGIA MAJI YA BARAKA PIKIPIKI YA MWANDISHI WA HABARI.


Padri akiendelea kuimwagia Maji ya baraka Pikipiki hiyo

Pikipiki hiyo ikijianda kuingia Mboga ya wanyama ya Mikumi Majira ya saa 12 Jioni akielekea Kilombero

Pikipiki hiyo ikiwa katikati ya Msitu Mnene ikielekea Matombo  Wilaya ya  Morogoro Vijijini
Pikipiki hiyo ikijianda kupanda Mlima wa Ng'aro Kijiji cha Kiloka Wilaya ya Morogoro Vijijini

...Wakati Pikipiki hiyo ikitokea Kilindi Mkoani Tanga ilipofika Tarafa ya Turiani Wilaya ya Movomero ilipasuka Mpira wa Nyuma baada ya kukanyaka Kisiki. Tukio hili lilitokea kabla ya Padri huyo ajaimwagia Maji ya baraka Pikipiki hiyo ya kazi
....Pikipiki hiyo ikiwa katikati ya Soko Kuu la Wilaya ya Kilosa
Pikipiki hiyo ikiwa Soko Kuu la Mkuyuni Morogoro Vijijini
Pikipiki hiyo ikiwa Kijiji cha Melela Mlandizi Wilaya ya Movomero
 

Padri wa Kanisa Katoli Jimbo la Morogoro Parokia ya Area Five Nane Nane katika kudhamini mchango wa Pikipiki ya Mwandishi wa Mtandao huu inayosafiri usiku na mchana Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro, kwenye Misitu Minene na Mbunga za Wanyama wakali. 
 
Mwana habari huyo akitafuta habari za kijamii hasa za kuwatetea wanyonge hivyo Mtumishi huyo wa Mungu aliamua kukimwagia Maji ya baraka chombo hicho kwa lengo la kukiondolea Mikosi mbali mbali zikiwemo ajari.
 
Kwa niaba ya wananchi hao Wangone Mwandishi wa habari hizi anamshukuru Mtumishi huyo wa Mungu kwa kutambua jambo hilo.

Saturday, October 30, 2021

BABA NA MWANA

Haji Manara aliyesimama akiwa na baba yake Mazazi Mzee Sundar Manara'Computer'
                Shiza Kichuya Kulia na baba yake mazazi
                        Adamu Seleman kulia  na Mwanaye
 

.
Picha no 1
 Mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya Tifa ya Tanzana Mzee Sundar Manara[Aliyeketi kwenye kiti akiwa na Mwanaye Haji Manara ambaye kwa sasa ni Afisa habari wa Yanga. Wawili hao walinaswa na Kamera za Mtandao huu kwenye Msiba wa Mwalimu Mohamed Msomari Mtaa wa Stesheni Manispaa ya Morogoro. siku kadhaa zilizopita.
 
Picha no 2
Winga wa zamani wa Simba Shiza Kichuya[kulia] ambaye kwa sasa anakipiga timu ya Namungo ya Lindi akiwa na baba yake Mazazi Ramadhana Kichuya, mara baa ya mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Shule ya Msingi Msamvu baada ya msimu wa ligi kuu kukamilika miaka kadhaa iliyopita.
Picha no 3 
 
Beki wa zamani wa Simba Adam Seleman 'TATA' kulia akiwa na Mwanaye Miraj Adam Selema ambaye naye miaka kadhaa iliyopita akiitumikia timu ya Simba kabla ya kuachwa na timu hiyo baada ya kuvunjika Mguu kwenye gemu ya Simba na Mgambo ya Tanga.

Friday, October 29, 2021

MASTAA RELI KIBOKO YA VIGOGO BAADHI YAO NI HAWA HAPA.


 


                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
 
Ikumbukwe timu ya Reli ya Mkoani Morogoro ilipachikwa jina la Reli Kiboko ya Vigogo baada ya Kuvifunga Vigogo vya soka nchini Simba yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Dar na Yanga yenye Maskani yake Makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar kila walipokuta na Reli kutoka Mji Kasoro Bahari’Morogoro’ walichezea Kichapo iwe nyumbani kwao Dar au Moro. 
 
Baadhi ya Mastaa hao wa Reli Kiboko ya Vigogo ni hawa kutoka Kulia ni Ally Jangalu ‘Mwananguu’’ambaye baadaye alitoka Reli na Kujiunga na Pan Afrika, Malota Soma ‘Ball Jagra’ baada ya kung’ara alinyakuliwa na Simba, David Mihambo’Fundi wa Mpira’ ambaye naye alitimkia Simba. 
 
Wengine ni Hamis Malifedha’ yeye kali yake ya Mpira iliishia hapo hapo Reli.
Fikiri Magosso ‘baba ldrissa’naye alitimkia Simba na Steven Mdachi huyu kisa chake kinafikirisha baada ya kuifunga Simba kwenye ligi kuu.
 
Wakali hao kutoka Mtaa wa Msimbazi wenye Pilikapilika nyingi walimuazima Mdachi kuitumika Simba kwenye Michezo wa Kimataifa Pekee.
 
Mastaa hao wa 'Long time'walinaswa na kamera za Mtandao huu kwenye Bonanza la wachezaji nyota wa zamani lililofanyika hivi karibuni Uwanja wa Jamhuri Mkoa Morogoro. huku kila mmoja akiitumia kia timu yake wengine walitokea Dar na wengine bado wanaishi hapa hapa Moro. Kwa vile Mwandishi wa Mtandao huu anawafahamu vizuri aliwakusanya na kuwa photo picha hii adhimu.

Thursday, October 28, 2021

MZEE SUNDAR MANARA AMFURAHI MTOTO ALIYETINGA JEZI YA YANGA.

Mchezaji wa zmanai wa Yanga Sundar Manara 'Computer akiwa na mtoto shabiki wa Yanga Leone Aristo Niktas
Aristo Niktas ambaye ni baba mzazi wa dogo huyo akimpa maelezo ya Ziada Mzee Manara kuhusiana na mtoto huyo kuipenda timu ya Yanga

                         Dogo Janja akiwa kwenye Benchi
Mshambuliaji hatari wa zamanai wa Yanga Makumbi Juma akiwa na dogo Leone Niktasi



Mshambuliaji hatari wa zamanai wa Reli Veterani  Aristo Niktasi akipiga' Jiramba'
 

                      Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

FUNDI wa mpira enzi hiyo Mzee Sundar Manara’Computer’ ameshindwa kuzuia hisia zake baada ya kumuona Mtoto Leone Aristotie Niktas ametinga jezi ya Yanga.

Mzee Manara ambaye ni baba mzazi wa Afisa habari wa Yanga Haji  Manara mara baada ya kumuona dogo huyo kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro alimwita na kumkumbatia huku akitabasamu akivutiwa na dogo janja huyo aliyetinga Uzi wa chama la Wananchi.

 

Dodo huyo ambaye ni mtoto wa aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Aristotie Niktasi alitinga uwanja hapo akiwa sambamba na baba yake ambaye pia ni Mwanachama ‘lia lia’ wa Yanga.

 

Kwa jinsi dogo  huyo alivyodamshi na uzi huo wa Yanga watu wengi walivutia akiwemo pia mchezaji wa zamani wa Yanga Makumbi Juma ‘Homa la Jiji’ amabaye naye alishindwa kuzuia mahaba yake na kujikuta akimvuta mtoto huyo kwenye himaya yake na kupiga naye stori huku akicheza naye Mpira.

 

Matukio hayo yalitokea hivi karibu kwenye bonanza la wachezaji nyota wa zamani wakiwemo wa Simba na Yanga.

 

Aristo’Mgosi’ ambaye ni Giriki aliyekulia Lushoto Mkoani Tanga, kwenye bonanza hilo aliitumikia timu ya Reli Veterani ya Mkoani Morogoro.

Wakati Mastaa hao wa zamani wa Yanga wakigombea kupiga Picha na dogo Janja huyo Wachezaji wa zamani wa Simba Akiwemo Sundar Juma waliwatupia maneno ya kejeri Mastaa hao wa Yanga kwa kitendo hicho wakionekana kukerwa.

 

“ Huo ni Usanii motto huyo wa miaka 4 hana akili za kupenda Yanga au Simba mnachofanya hapo ni kumlazimisha kupenda timu yenu mbovu” walisema Mastaa hao wa zamani wa Simba.

 

Kufuatia kauli hiyo Mwandishi wa habari hizi alizungumza na baba mzazi wa mtoto huyo ambapo alipotakiwa kuelezea madai hayo wa Mastaa wa Simba alisema

 

” Mgosi Sekidele kuna meseli inasema Mtoto wa nyoka ni nyoka wewe unanijua fika mimi ni Yanga iweje Mwanangu awe Simba ngoja nikae mbali then umulize mwanangu yeye ni Simba au Yanga atakupa majibu”alisema Aristo ambaye ni kigogo wa kampuni moja binafsi ya mkoani hapa.

 

Dogo huyo alipoulizwa na Mtandao huu bila kusita alijibu kwa kinywa kipana kwamba yeye ni Yanga.

         

Wednesday, October 27, 2021

KAULI YA MZAZI KWA MWANAYE

Mwandishi wa Mtandao pichani akitafuta habari kwenye maeneo mbali mbali ya wilaya za Mkoa wa Morogoro



                    Mwandishi wa Mtandao huu aking'oa kisiki



 

Mzazi anapokuambia Mwanangu kuwa uyaone hana maana . uyaone Maghorofa ya Mjini au Vichaka vya Kijijini

Ana maana Uyaone maisha yalivyo na Changamoto. zake Hasi na Chanya. Negative na Positive,Raha na Shida.Matamu na Machungu

Sunday, October 24, 2021

WAKALI WA NYIMBO ZA INJIRI NCHINI WENGI WAO WANATOKEA MKOA WA MBEYA

 Bahati Bukuku akimkabidhi Kipaza sauti’Mic’ Mchungaji Emmanuel Mgaya Maarufu Masanja  Mkandamizaji’ ambaye pia ni Msanii Maarufu wa vichekesho chini akipiga kazi kundi la Original Commedy. 



Na Dunstan Shekidele,Morogoro.  

Kila Mkoa hapa nchini unasifa zake za kutoa wasanii wengi wa fani mbali mbali kama vile Soka, Riadha Muziki wa bongofleva Nyimbo za lnjiri na Uigizaji.

 

Mkoa wa Morogoro unaongoza nchini kwa kuzalisha wachezanyo wengi wa Mpira wa Minguu nchini wanaotamba timu mbali mbali zikiwemo Simba, Yanga na Azam.

 

Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kuzalisha wachezaji wengi wa Riadha Wazee wa Kukimbiza Upepo’ Mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kusambaza wanamuziki nyota wa Bongofleva kama vile Nassib Abdul'Diamond Platnums’ Ally Kiba, Ommy Dimpoz na Mikoa ya Dar es salaam na Pwan yenyewe inaongoza kuzalisha Waingizaji wa Filam na Vichekezo.

 

Hii na Chomekea Mkoa wa Mara wenyewe unaongoza kutoa wapiganaje’Wanajeshi’ wengi kwenye kambi nyingi za Jeshi nchini.

 

 

Wadau mtandao huu mtakubaliana nami  kwamba kwa sasa hapa nchini Mkoa wa Mbeya ndio unaongoza kwa kutoa waimbaji wengi nyota wa nyimbo za lnjiri.

 

Miongoni mwa waimbaji hao ni pamoja na Bahati, Bukuku[kulia]Matha Mwaipaja]Kati] na Stara Thomas, kwa pamoja Mastaa hao wakipozi mbele ya Kamera za Mtandao huu kwenye moja ya Tamasha la lnjiri lililofanyika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

 

Kwa stara Thomas sijang’amua Mara Moja mkoa anaotoka.

                                 CAPTION

 

 PICHA YA KATI JUU

Mwandishi wa Mtandao huu kulia akimuweka Mtu kati Msanii nyota wa lnjiri[Muziki wa kumtukuza Mungu’ na Muziki wa kizazi Kipya’Bongofleva’ Stara Thomas.

Kwenye mahojiano hayo aliulizwa swali, kwa nini anakuwa vuguvugu Moto si Moto baridi si baridi kwa maana  mchana anaimba nyimbo za kumtukuza Mungu nyimbo za lnjiri na Usiku anaimba nyimbo za Bongofleva nyimbo za kidunia,kwamba  kiimani jambo hilo limekaa kaaje?

 

Swali hilo lilionekana kumzidi kimo Msanii huyo ambapo  alipotakiwia  kujibu muda mwingi aliutumia kuchezea macho yake na mwisho akajibu kwa kifupi akisema.

 

” Swala hilo limekaa vibaya so muda wowote kuanzia sasa nitaachana na muziki wa kidunia na kubaki kwenye kazi Moja ya kumtumikia Mungu wangu ambaye ni Mwaminifu kwangu”

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...