Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Kila Mkoa hapa nchini unasifa zake za kutoa wasanii wengi wa fani mbali mbali kama vile Soka, Riadha Muziki wa bongofleva Nyimbo za lnjiri na Uigizaji.
Mkoa wa Morogoro unaongoza nchini kwa kuzalisha wachezanyo wengi wa Mpira wa Minguu nchini wanaotamba timu mbali mbali zikiwemo Simba, Yanga na Azam.
Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kuzalisha wachezaji wengi wa Riadha Wazee wa Kukimbiza Upepo’ Mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kusambaza wanamuziki nyota wa Bongofleva kama vile Nassib Abdul'Diamond Platnums’ Ally Kiba, Ommy Dimpoz na Mikoa ya Dar es salaam na Pwan yenyewe inaongoza kuzalisha Waingizaji wa Filam na Vichekezo.
Hii na Chomekea Mkoa wa Mara wenyewe unaongoza kutoa wapiganaje’Wanajeshi’ wengi kwenye kambi nyingi za Jeshi nchini.
Wadau mtandao huu mtakubaliana nami kwamba kwa sasa hapa nchini Mkoa wa Mbeya ndio unaongoza kwa kutoa waimbaji wengi nyota wa nyimbo za lnjiri.
Miongoni mwa waimbaji hao ni pamoja na Bahati, Bukuku[kulia]Matha Mwaipaja]Kati] na Stara Thomas, kwa pamoja Mastaa hao wakipozi mbele ya Kamera za Mtandao huu kwenye moja ya Tamasha la lnjiri lililofanyika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Kwa stara Thomas sijang’amua Mara Moja mkoa anaotoka.
CAPTION
PICHA YA KATI JUU
Mwandishi wa Mtandao huu kulia akimuweka Mtu kati Msanii nyota wa lnjiri[Muziki wa kumtukuza Mungu’ na Muziki wa kizazi Kipya’Bongofleva’ Stara Thomas.
Kwenye mahojiano hayo aliulizwa swali, kwa nini anakuwa vuguvugu Moto si Moto baridi si baridi kwa maana mchana anaimba nyimbo za kumtukuza Mungu nyimbo za lnjiri na Usiku anaimba nyimbo za Bongofleva nyimbo za kidunia,kwamba kiimani jambo hilo limekaa kaaje?
Swali hilo lilionekana kumzidi kimo Msanii huyo ambapo alipotakiwia kujibu muda mwingi aliutumia kuchezea macho yake na mwisho akajibu kwa kifupi akisema.
” Swala hilo limekaa vibaya so muda wowote kuanzia sasa nitaachana na muziki wa kidunia na kubaki kwenye kazi Moja ya kumtumikia Mungu wangu ambaye ni Mwaminifu kwangu”
No comments:
Post a Comment