Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, October 28, 2021

MZEE SUNDAR MANARA AMFURAHI MTOTO ALIYETINGA JEZI YA YANGA.

Mchezaji wa zmanai wa Yanga Sundar Manara 'Computer akiwa na mtoto shabiki wa Yanga Leone Aristo Niktas
Aristo Niktas ambaye ni baba mzazi wa dogo huyo akimpa maelezo ya Ziada Mzee Manara kuhusiana na mtoto huyo kuipenda timu ya Yanga

                         Dogo Janja akiwa kwenye Benchi
Mshambuliaji hatari wa zamanai wa Yanga Makumbi Juma akiwa na dogo Leone Niktasi



Mshambuliaji hatari wa zamanai wa Reli Veterani  Aristo Niktasi akipiga' Jiramba'
 

                      Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

FUNDI wa mpira enzi hiyo Mzee Sundar Manara’Computer’ ameshindwa kuzuia hisia zake baada ya kumuona Mtoto Leone Aristotie Niktas ametinga jezi ya Yanga.

Mzee Manara ambaye ni baba mzazi wa Afisa habari wa Yanga Haji  Manara mara baada ya kumuona dogo huyo kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro alimwita na kumkumbatia huku akitabasamu akivutiwa na dogo janja huyo aliyetinga Uzi wa chama la Wananchi.

 

Dodo huyo ambaye ni mtoto wa aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’ Aristotie Niktasi alitinga uwanja hapo akiwa sambamba na baba yake ambaye pia ni Mwanachama ‘lia lia’ wa Yanga.

 

Kwa jinsi dogo  huyo alivyodamshi na uzi huo wa Yanga watu wengi walivutia akiwemo pia mchezaji wa zamani wa Yanga Makumbi Juma ‘Homa la Jiji’ amabaye naye alishindwa kuzuia mahaba yake na kujikuta akimvuta mtoto huyo kwenye himaya yake na kupiga naye stori huku akicheza naye Mpira.

 

Matukio hayo yalitokea hivi karibu kwenye bonanza la wachezaji nyota wa zamani wakiwemo wa Simba na Yanga.

 

Aristo’Mgosi’ ambaye ni Giriki aliyekulia Lushoto Mkoani Tanga, kwenye bonanza hilo aliitumikia timu ya Reli Veterani ya Mkoani Morogoro.

Wakati Mastaa hao wa zamani wa Yanga wakigombea kupiga Picha na dogo Janja huyo Wachezaji wa zamani wa Simba Akiwemo Sundar Juma waliwatupia maneno ya kejeri Mastaa hao wa Yanga kwa kitendo hicho wakionekana kukerwa.

 

“ Huo ni Usanii motto huyo wa miaka 4 hana akili za kupenda Yanga au Simba mnachofanya hapo ni kumlazimisha kupenda timu yenu mbovu” walisema Mastaa hao wa zamani wa Simba.

 

Kufuatia kauli hiyo Mwandishi wa habari hizi alizungumza na baba mzazi wa mtoto huyo ambapo alipotakiwa kuelezea madai hayo wa Mastaa wa Simba alisema

 

” Mgosi Sekidele kuna meseli inasema Mtoto wa nyoka ni nyoka wewe unanijua fika mimi ni Yanga iweje Mwanangu awe Simba ngoja nikae mbali then umulize mwanangu yeye ni Simba au Yanga atakupa majibu”alisema Aristo ambaye ni kigogo wa kampuni moja binafsi ya mkoani hapa.

 

Dogo huyo alipoulizwa na Mtandao huu bila kusita alijibu kwa kinywa kipana kwamba yeye ni Yanga.

         

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...