Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, October 29, 2021

MASTAA RELI KIBOKO YA VIGOGO BAADHI YAO NI HAWA HAPA.


 


                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
 
Ikumbukwe timu ya Reli ya Mkoani Morogoro ilipachikwa jina la Reli Kiboko ya Vigogo baada ya Kuvifunga Vigogo vya soka nchini Simba yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Dar na Yanga yenye Maskani yake Makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar kila walipokuta na Reli kutoka Mji Kasoro Bahari’Morogoro’ walichezea Kichapo iwe nyumbani kwao Dar au Moro. 
 
Baadhi ya Mastaa hao wa Reli Kiboko ya Vigogo ni hawa kutoka Kulia ni Ally Jangalu ‘Mwananguu’’ambaye baadaye alitoka Reli na Kujiunga na Pan Afrika, Malota Soma ‘Ball Jagra’ baada ya kung’ara alinyakuliwa na Simba, David Mihambo’Fundi wa Mpira’ ambaye naye alitimkia Simba. 
 
Wengine ni Hamis Malifedha’ yeye kali yake ya Mpira iliishia hapo hapo Reli.
Fikiri Magosso ‘baba ldrissa’naye alitimkia Simba na Steven Mdachi huyu kisa chake kinafikirisha baada ya kuifunga Simba kwenye ligi kuu.
 
Wakali hao kutoka Mtaa wa Msimbazi wenye Pilikapilika nyingi walimuazima Mdachi kuitumika Simba kwenye Michezo wa Kimataifa Pekee.
 
Mastaa hao wa 'Long time'walinaswa na kamera za Mtandao huu kwenye Bonanza la wachezaji nyota wa zamani lililofanyika hivi karibuni Uwanja wa Jamhuri Mkoa Morogoro. huku kila mmoja akiitumia kia timu yake wengine walitokea Dar na wengine bado wanaishi hapa hapa Moro. Kwa vile Mwandishi wa Mtandao huu anawafahamu vizuri aliwakusanya na kuwa photo picha hii adhimu.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...