Na Dustan Shekidele,Morogorto.
MOSHI Mweupe
umeanza kuonekana eneo la daraja la Relwe almaarufu daraja la Ng’ombe.
Jana majira ya asubuhi Mtandao huu ulikatiza eneo
la mradi huo unaojengwa na Mkandarasi Mzawa kampuni ya Cope ya Mkoani Morogoro
na kushuhudia mafundi wakiendelea na kazi kwa kasi jana Jumapili.
Akizungumza
na Mtandao huu fundi Mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa sababu yeye si
msemaji wa kamuni hiyo.aliutonya mtandao huu kwamba jana hiyo hiyo majira ya
mchana watembea kwa miguu wataruhusiwa kupita kwenye daraja hilo,
‘’Baada ya
kupanga haya mawe kwenye kingo za daraja mchana mtambo utaingia mtoni kuchimba
kwa lengo la kuongeza kina na mto, hivyo lile daraja la muda ambalo liko pale tutalivunja
kutanua mto.
Hivyo tutawaruhusu
watu kupita kwenye kwenye daraja jipya ukija mchana utashuhudia watu wakipita’’Alisema mafundi
huyo.
Alipoulizwa
litakamilika lini alijibu.
’’ Daraja
hili liko hatua za mwisho kukamilika kama ni kwenye mpira ni dakika ya 88’’alisema
fundi huyo.
Jana hiyo
hiyo majira ya mchana Mtandao huu ulikatiza tena kwenye daraja hilo na
kushuhudia watu wakivuka kwenye daraja hilo huku wakitabasamu.
Akijojiwa na
Mtandao huu mmoja wawananchi wa eneo hilo Thabiti Mgalula alisema’’
Tunaishukuru serikali kwa kutujengea daraji hili la zuri tumafurahi leo
tumeanza kulitumia kama unavyojua shekidele mimi naishi kota za Reli na
mahitaji yetu muhimu yako ng’ambo ya daraja hili’’ alisema Mgalula ambaye ni
mchezaji wa zamani wa Reli ile ya Kiboko ya Vigogo akicheza winga ya kulia.
Vile vile mtandao huu ulishuhudia Mtandao
ukiwa ndani ya mto ukichimba kwa lengo la kuongeza kina cha urefu wa mto huo wa
Morogoro unaotoka juu ya milima ya
Uluguru kuelekea Mkoani Pwani.