Na Dustan Shekidele,Morogorto.
MOSHI Mweupe umeanza kuonekana eneo la daraja la Relwe almaarufu daraja la Ng’ombe.
Jana majira ya asubuhi Mtandao huu ulikatiza eneo la mradi huo unaojengwa na Mkandarasi Mzawa kampuni ya Cope ya Mkoani Morogoro na kushuhudia mafundi wakiendelea na kazi kwa kasi jana Jumapili.
Akizungumza na Mtandao huu fundi Mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa sababu yeye si msemaji wa kamuni hiyo.aliutonya mtandao huu kwamba jana hiyo hiyo majira ya mchana watembea kwa miguu wataruhusiwa kupita kwenye daraja hilo,
‘’Baada ya kupanga haya mawe kwenye kingo za daraja mchana mtambo utaingia mtoni kuchimba kwa lengo la kuongeza kina na mto, hivyo lile daraja la muda ambalo liko pale tutalivunja kutanua mto.
Hivyo tutawaruhusu watu kupita kwenye kwenye daraja jipya ukija mchana utashuhudia watu wakipita’’Alisema mafundi huyo.
Alipoulizwa litakamilika lini alijibu.
’’ Daraja hili liko hatua za mwisho kukamilika kama ni kwenye mpira ni dakika ya 88’’alisema fundi huyo.
Jana hiyo hiyo majira ya mchana Mtandao huu ulikatiza tena kwenye daraja hilo na kushuhudia watu wakivuka kwenye daraja hilo huku wakitabasamu.
Akijojiwa na Mtandao huu mmoja wawananchi wa eneo hilo Thabiti Mgalula alisema’’ Tunaishukuru serikali kwa kutujengea daraji hili la zuri tumafurahi leo tumeanza kulitumia kama unavyojua shekidele mimi naishi kota za Reli na mahitaji yetu muhimu yako ng’ambo ya daraja hili’’ alisema Mgalula ambaye ni mchezaji wa zamani wa Reli ile ya Kiboko ya Vigogo akicheza winga ya kulia.
Vile vile mtandao huu ulishuhudia Mtandao ukiwa ndani ya mto ukichimba kwa lengo la kuongeza kina cha urefu wa mto huo wa Morogoro unaotoka juu ya milima ya Uluguru kuelekea Mkoani Pwani.








No comments:
Post a Comment