Na Dustan Shekidele Morogoro.
NAWASALIMU kwa jina kuu la Yesu Kristo,ama baada ya salamu tuingie kwenye somo letu la Leo ambalo linahusu Chakula na kinywaji.
Hakuna asiyefahamu kwamba Chakula na kinywaji ni uhai wa kiumbe chochote kilichopo hapa Duniani kisipokula au kunywa lazima kifariki dunia.
Naamini Muda huu ninapoandika ujumbe huu kuna watu waina mbili , wenye njaa hawana chakula kwa sababu mbali mbali ikiwemo ufukura huku kuna baadhi ya watu wenye uwezo wanakula chakula kingi mpaka wana saza na kukitupa jalala ili hari kuna jirani yake amelala njaa kwa kukosa chakua.
Hii ya kutupa chakula ni chukizo kubwa mbele ya Mungu aliyekujalia kupata hicho chakula nawakumbusha na kuikumbusha pia nafsi yangu kwamba tusiwe wabinafsi wa kujilimbikizia mali sisi na familia zetu. Ifahamike kuwa tajiri au kuwa na mali nyingi sio dhambi. Ila dhambi ni namna ya kutumia huo utajiri wako.
Kundi la pili kuna baadhi ya watu wengi wao wakiwa ni matajiri wanachakula kingi lakini wanashindwa kula kwa sababu mbali mbali ikiwemo magonjwa.
Kwenye jamii yetu utasikia mtu anasema kutokana na magonjwa aliyonayo anayoishi ili aendelee kuishi Madaktari wamemzuia kula Nyama, Wali wenye mafuta, chai yenye sukari chakula chernye chumvi, asinywe Soda na Juice nakadharika na kadharika.
Kwa wewe ambaye siku zote unachakula ndani na huna ugonjwa wowote unaosababisha kuchagua chakula Mwambie Mungu asante huku ukitenga muda wako kwenda nyumba ya lbada kumuabudu kwa wema huo anaoendelea kukutendea.
Utashangaa kuna mtu kapewa vyote Chakula na afya nyema lakini jumapili kama leo kanisani kwake kuna meza ya Bwana sakrameti Takatifu [kula na kunywa damu ya Yesu] Kwa sababu anazozijua yeye mtu huyo anakimbia kula na kunywa Sakramenti hiyo.
MADHARA YA CHAKULA NA KINYWAJ.
Sio kila chakula unacho ni sahihi kwako vingine ni mitego kwako, mfano Mwanafunzi ‘Dent’ anakaribishwa chips kuku na mwanaume, Mwisho wa siku ofa hiyo itamgharimu pakubwa anaweza kupata Mimba au gonjwa hatari la UKIMWI na kukatisha ndoto zake za kimaisha kwa tamaa ya Chips Yai ambayo dharama yake haizidi elfu 5.
Mke wa mtu anapewa Ofa ya Bia na Njama Choma anasaliti ndoa yake anaibanyua Amri ya 6[Usizini] mwisho ya siku anazoa Gonjwa la Ukimwi huko nje anampelekea Mumewe ndani badae wote wawili wanakufa na kuwaacha watoto zao yatima kwa tamaa ya Pombe na Nyama Choma ambayo gharama yake haizidi elfu 20.
KIIMANI KWA WAMCHAO MUNGU.
Sio kila kalamu unayoalikwa inautukufu wa Mungu, nyingine ni Madhebau za kipepo[Kishetani] Mfano unaalikwa kwenye kalamu kumbe shughuri hiyo ni ya kumsimika Mganga wa kienyeji.
Au unaalikwa kwenye Mkutano kumbe mkutano huo kiongozi anayetaka uongozi anaandaa chakula kwa lengo la kuwakusanya wajumbe wamchague kwenye nafasi anayogombea.
Mwenye masikio na asikie asiye na masikio…..]
Kwa leo naishi hapa tukutane kwenye mada nyingine Jumapili ijayo panapo majaliwa ya Mwennyezi Mungu.



