......Maharusi wakivishana pete baada ya kura kiapo cha Ndoa
.....Maharusi hao 101 pamja na wasimamizi wao 101 ndugu na jamaa zao wakiwa nje ya kanisa wakijiandaa kula chakula kiihcho andaliwa na baba Askfu
Muonekana mzuri wa kanisa katoliki Parokia ya Kigunyenyembe
Askofu Msimbe akiombea chakua
.
Na Dustan Shekidele Morogoro.
IJUMAA iliyopita kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro kupitia kiongozi mkuu wa Jimbo hilo Askofu Lazarus Vitalis Msimbe, wameandaa ndoa za mafungu.
Katika ibada hiyo ya ndoa iliyofanyika Parokia ya ‘Bikira Maria Mama wa Kanisa’ Kigurunyembe kata ya Kilakala Mkoani hapa.wanandoa 101 walijitokeza kubariki ndoa zao‘kupasha Moto Kiporo’ huku kivutio kikubwa kikiwa kwa mahurusi ‘Vikongwe’ Silali Banyakirusa mwenye umri wa miaka 75 na mchumba’ke Bibi harusi Kalolina Mshauri mwenye umri wa miaka 77’
Baada ya kura kiapo cha ndoa na kuunganishwa kuwa mwili mmoja Mtandao huu uliwafuata maharusi hao na kufanya nao mahojiano maalum wa kwanza fungunguka aikuwa bwana hasusi
Mtandao. Mzee wangu shikamoo na hongera kwa kufunga Ndoa.
Bwana Harusi. Marahaba na asante kwa pongezi.
Mtandao. kwa mtazamo wangu kwa maharusi wote 101 wewe na mkeo ndio mnaonekana kuwa na umri mkubwa je una miaka mingapi na mmeishi kwenye uchumba kwa muda gani?
Bwana harusi. Mimi ninamiaka 75 na uchumba wetu unamiezi 2 tu, jumapili kama mbili hvi zilizopita tumesikia tangazo kanisa kwamba Askofu wetu ameandaa ndoa kwa waumini wake hivyo tumejiandikisha na hatimaye Leo tumefunga ndoa binafsi namshukuru sana baba Askofu kwa jambo hili
Mtandao. Kweli nimeamini kila jambo la Kheri lina kuwa na baraka za Mungu.mkiwa ndani ya penzi Jipya lenye umri wa miezi 2 ikatokea nafasi hii hadhimu ya kufunga ndoa.
Umesema uchumba wenu ni mchanga je awari ulikuwa na mahusiano mengine nakama uikuwa nayo umejaliwa kupata watoto na wajukuu wangapi?
Bwana hasuri. Nikweli huko nyuma nikuwa na mahusiano mengine nimejaliwa kupata watoto 4 na wajukuu 9
Mtandao. Asante kwa ushirikiano nawaombea kwa Mungu abariki ndoa yengu iwe ya amani na furaha huku mkibebeana misalaba kwenye madhaifu yenu kwani hakuna binadamu mkamilifu isipkuwa Mungu pekee.
Bwana haurusi. Asante sana kwa maneno ya hekima.nawe Mungu akubariki kwenye kazi zako.
Kwa upande wake Bibi harusi amesema yeye na Mumewe huyo wanaishi Kichangani baada ya kukutana wameamua kufunga ndoa ns utu uzima wao.
“ Unajua lbada njema huanzia nyumbani sasa kama mnaishi kinyumba miaka nenda miaka ludi nyumbani yenye haiwezi kuwa na baraka ndio maana na utu uzima wetu huu mimi na mwenzangu baada na kupata fursa hii tumeamua kuichangamika”amesema Bi. Kalolini.
Kama ilivyo kwa mumewe Bi Kalolini awari alikuwa na mahusiano mengine na alipoulizwa ana watoto na wajukuu wangapi alijibu.
“kwa umri wangu huu wa miaka 77 nimejaliwa kupata watoto 7 na wajukuu 14”
AMSIKIE ASKOFU SASA.
Kutokana ubize na uchovu wa kufungisha kwa mpigo ndoa hizo 101 busara zilimungoza Mwandishi wa habari hizi kumpa muda wa kupunzika Askofu Msimbe na kwamba siku iliyofuata majira ya usiku Mtandao huu ulimtwangia simu Askofu huyo na kufanya naye mahojiano kama ifuatavyo.
Mwandishi. Baba Askofu Tumsifu Yesu Kristo
Askofu. Milele Amina
Mwandishi.Pole kwa kazi ngumu ya jana ya kufungisha ndoa 101 lakini nikupongeze kwa uchungaji mzuri wa ndoo yako uliofanikisha kuwarejesha zizini mwa bwana kutoka kwenye dhambi ya kuishi bila ndoa.
Askofu Asante sana kwa maneno ya faraja.
Mwandishi. Taarifa nilizo nayo ni kwamba shughuri nzima umeandaa wewe ikiwemo chakula cha watu zaidi ya elfu moja tuliokuwa pale kanisani tumekula na kunywa je ni pesa za kanisa au zimetoka mfukoni kwako ?
Swali la pili niliwaona maharusi kutoa Maeneo ya mbali kama vile Mzumbe, Lukobe Mkundi Tungi,Misongeni na Kingolwira je umetumia njia gani kuwapa taarifa?
Askofu. Kwanza ufahamua tukio lile ni la Jimbo lote la Morogoro ambalo mimi naliongoza ndio maana umeona wanandoa tukoka maeneo yote ya Jimbo.
Kuhusu taarifa nilimpa kazi hiyo Msaidizi wangu Padri Sewando ambaye aliwaagiza makatekista wote jimboni kuwatangazia waumini wetu uwepo wa jambo hilo.
Kimsingi tukio lile lilipaswa lifanyike kanisa kuu la Mt. Patrick kama unavyojua kanisa hilo kwa sasa lipo kwenye ukarabati Mkubwa ndio maana tukaamua kufanya pale Parokia ya Kigurunyembe.
Kuhusu kuandaa shunguli ile ni mimi niiyendaa nimetumia million 10 kuanzia chakula na gharama nyingine.
Mwandishi.Mungu akubariki sana kwa Moyo wako huo. pale kanisani palikuwa na minong’ono wakiuliza kama utaanda tena tukio kama hili je jibu lako ni lipi kwa hao waumini wako?
Askofu. Swali zuri Mungu akipenda mwenzi wa 12 tutaandaa tena tukio kama lile hivyo waumini wetu wajiandae.
Mwandishi Sawa mtumishi wa Mungu barikiwa sana na asante kwa ‘time’ yako.
Askofu Asante na wewe pia usiku mwema.
Katikati ya Ibada hiyo mmoja wa maharusi aiyepewa nafasi ya kutoa neno la shukrani. kaitaja timu ya Yanga Askofu katia neno.habari hiyo na picha itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment