Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, August 31, 2025

UJUMBE WA NENO LA MUNGU JUMAPILI YA LEO AGOSTI 31 UNAHUSU CHAKULA NA KINYWAJI.

Pichani mtumishi wa Munngu Dustan Shekidele akiwa na wanae Tumaini[kushoto] na Neema  kwa pamoja wanamshukuru Mungu  kwa kuwapa chakula na afya nyema inayowapa fursa ya kula na kunywa chochote.

 

   

          Na Dustan Shekidele Morogoro.

NAWASALIMU kwa jina kuu la Yesu Kristo,ama baada ya salamu tuingie kwenye somo letu la Leo ambalo linahusu Chakula na kinywaji.

 

Hakuna asiyefahamu kwamba Chakula na kinywaji ni uhai wa kiumbe chochote kilichopo hapa Duniani kisipokula au kunywa lazima kifariki dunia.

 

Naamini Muda huu ninapoandika ujumbe huu kuna watu waina mbili , wenye njaa hawana chakula kwa sababu mbali mbali ikiwemo ufukura  huku kuna baadhi  ya watu wenye uwezo wanakula chakula kingi mpaka wana saza na kukitupa jalala ili hari kuna jirani yake amelala  njaa kwa kukosa chakua.

 

 Hii ya kutupa chakula ni chukizo kubwa mbele ya  Mungu aliyekujalia kupata hicho chakula nawakumbusha na kuikumbusha pia nafsi yangu kwamba tusiwe wabinafsi wa kujilimbikizia mali sisi na familia zetu. Ifahamike kuwa tajiri au kuwa na mali nyingi sio dhambi. Ila dhambi ni namna ya kutumia huo utajiri wako.

 

Kundi la pili kuna baadhi ya watu wengi wao wakiwa ni matajiri wanachakula kingi lakini wanashindwa kula  kwa sababu mbali mbali ikiwemo magonjwa.

Kwenye jamii yetu utasikia mtu anasema kutokana na magonjwa aliyonayo anayoishi ili aendelee kuishi Madaktari wamemzuia kula Nyama, Wali wenye mafuta,  chai yenye sukari chakula chernye chumvi, asinywe Soda na Juice nakadharika na kadharika.

 

Kwa wewe ambaye siku zote unachakula ndani na huna ugonjwa wowote unaosababisha kuchagua chakula  Mwambie Mungu asante huku ukitenga muda wako  kwenda  nyumba ya lbada kumuabudu kwa wema huo anaoendelea kukutendea.

Utashangaa kuna mtu kapewa vyote Chakula na afya nyema lakini jumapili kama leo kanisani kwake kuna meza ya  Bwana sakrameti Takatifu [kula na kunywa damu ya Yesu] Kwa sababu anazozijua yeye mtu huyo anakimbia kula na kunywa Sakramenti hiyo.

 

         MADHARA YA CHAKULA NA KINYWAJ.

Sio kila chakula unacho ni sahihi kwako vingine ni mitego kwako, mfano Mwanafunzi ‘Dent’ anakaribishwa chips kuku na mwanaume, Mwisho wa siku ofa hiyo itamgharimu pakubwa anaweza  kupata Mimba au gonjwa hatari la UKIMWI na kukatisha ndoto zake za kimaisha kwa tamaa ya Chips Yai ambayo dharama yake haizidi elfu 5.

 

Mke wa mtu anapewa Ofa ya Bia na Njama Choma anasaliti ndoa yake anaibanyua Amri ya 6[Usizini]  mwisho ya siku anazoa Gonjwa la Ukimwi huko nje anampelekea Mumewe ndani badae wote wawili wanakufa na kuwaacha watoto zao yatima kwa tamaa ya Pombe na Nyama Choma ambayo gharama yake haizidi elfu 20.

        KIIMANI KWA WAMCHAO MUNGU.

Sio kila kalamu unayoalikwa  inautukufu wa Mungu, nyingine ni Madhebau za kipepo[Kishetani] Mfano unaalikwa kwenye kalamu kumbe shughuri hiyo ni ya kumsimika Mganga wa kienyeji.

 

Au unaalikwa kwenye Mkutano kumbe mkutano huo kiongozi anayetaka uongozi anaandaa chakula kwa lengo la kuwakusanya wajumbe  wamchague kwenye nafasi anayogombea.

Mwenye masikio na asikie asiye na masikio…..]

Kwa leo naishi hapa tukutane kwenye mada nyingine Jumapili ijayo panapo majaliwa ya Mwennyezi Mungu.

 


 

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...