Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, August 26, 2025

BWANA HARUSI AMKOSHA ASKOFU BAADA YA KUITAJA YANGA KANISANI.

Baba Askfu Msimbe akiingia kanisan huku akiwasimia waumini wake

             Bwana harusi Saema akizungumza na Mtanda huu

                  ....Mzee Massawe na kadi zake za Yanga

 


   Na Dustan Shekidele. Morogoro.

HIVI wewe huogopi? Yanga inatajwa mpaka kanisani.

Bwaha harusi  ameitaja Yanga akiwa juu ya Madhebau ya kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Mama wa Kanisa Kigurunyembe Mkoani hapa.

 Mwanandoa huyo Seraphin Josephat Salema[Pichani mwenye suti kali]amewataja mabingwa hao wa kihistoria [Yanga] wakati akitoa neno la shukrani kwa kanisa na  Askofu Razarus Vitalis Msimbe.

Kwa nini Bwaha harusi  ameitaja yanga? Ijumaa iliyopita kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro kwa ufadhiri wa Askofu Msimbe walifungisha ndoa 101  kwa wakati mmoja maarufu[Ndoa za mafungu].

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimethibitishwa na Askofu Msimbe zinadai Big Boss huyo wa kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro ametoa Milioa 10 kutoka mfukoni kwake kugharamia ndoa hizo.

 

Kwa Upendo huo  mmoja wa maharusi Selema aliamua kupanda madhebahuni na kumshukuru Askofu huyo kwa jambo hilo kubwa alilowafanyia.

 

“Kwa niaba ya maharusi wote tunakushukuru sana baba Askofu kwa jambo hili kubwa ulillotufanyia kwenye historia  ya maisha yetu mwenyezi Mungu akubariki sana, umeupiga mwingi kama Yanga.

 

Hivyo nawaomba maharusi wote na wasimamizi wetu tupite mbele tumpemkono wa shukrani Askofu wetu”alisema Bwanahauri huyo na kupokea zawadi ya makofi na vigeregere.

 

Baadae Mtandao huu ulimshuhudia Askofu Msimbe akitabasamu muda wote huku akisogea kwenye benchi la Selema na kupiga naye picha kama wanavyoonekana pichani.

 

Mwingine aliyefurahishwa na kauli hiyo ni Mwanachama maarufu wa Yanga mkoani Morogoro Mzee Leold Massawe kutoka tawi kuu la Yanga la mkoani hapa.

 

Mzee Massawe ambaye ni Mwanajeshi Mstaafu mara nyingi Yanga inapofika Mkoani Morogoro  mtadaoo huu humshuhuidia akiongoza kitengo la Ulinzi na usalama wa timu yao.

 

‘Mjeda’ huyo ambaye ni Muumini mzuri wa kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro kwenye lbada hiyo alikuwa ni miongoni mwa mshuhuda wa Ndoa hizo.

 

Wakati akihojiwa na Mtandao huu Mzee Massawe [Yanga Lia lia] alichana Waleti yake na kuchomoa kadi  mbili za Yanga ile ya uwanachama na ile ya Bank akimuonyesha Mwandishi wa habari hizi.

            MSIKIE ASKOFU .

Siku hiyo hiyo ya ijumaa majira ya usiku Mtandao huu ulimtwangia simu Askofu Msimbe na mahojiano yetu yalikuwa hivi.

Mtandao. Tumsifu Yesu Kristo baba Askofu.

Askofu. Milele Amina karibu.

Mtandao. Wakati mmoja wa maharusi akitoa neno la shukrani kwa wema uliowafanyia alipoitaja Yanga ulishindwa kujizuia akuangua kicheko,kwa kitendo hicho baadhi ya waumini wako waliibuka minong’ono wakisema wewe ni shabiki wa Yanga je ni kweli wewe ni Yanga au Simba Wazee wa Ubaya Ubwela?

Askofu. Kabla ya kujibu kaangua kicheko kisha akasema.

Niwe mkweli naipenda sana Yanga ikifungwa naumia sana na ikifanya vizuri nafurahi sana hivyo huyu Bwanaharusi kwenye neno lake la shukrani kwangu na kwa kanisani mwisho aliitaja Yanga jambo hilo pia limenifurahisha kwa sababu ametaja timu yangu ya Moyoni.

Mtandao. Sawa asante nikutakia usiku Mwema.

Askofu. Nakwako pia.

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...