Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, June 30, 2025

MKUU WA WILAYA ACHANA MISTARI KWENYE NDONDO CUP.





 


    Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MKUU wa Wilaya ya Morogoro Mh Mussa Kilakala Ijumaa iliyopita alikuwa kivutio  kwa mashabiki kibao waliofulika  Uwanja wa Saba saba kushuhudia Fainali ya Planet Ndondo Cup, baada ya mkuu huyo kuchana mistari ya Viwango.

 

Kiongozi huyo ‘Janki’ aliyekuwa mgeni Rasmi kwenye fainali hiyo, baada ya kuwakagua wanafainali Damu Chafu Fc na Chaka Bvu Fc alikabidhiwa Mic kuzungumza na wananchi wake waliofulika uwanjani hapo.

 

 Baada ya salamu Mh Kilakala aliwatania Mashabiki wa Simba na Yanga akisema”

Kwenye fainaili tunaweza kupata vipaji kama vya Pacome,Job, Mzize Aucho na Chama

Hatutegemei kuona Vipaji kama vya Mpanzu na Kibu D”

 

 Utani huo aliamsha shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki wa Yanga waliompa zawadi ya Makofi na Vigeregere huku mashabiki wa Simba wakipiga kimya wakizuka kwa kuchati na simu zao baadhi yao wakiwa na viswaswadu kama sio vitochi.

 

Baada ya utani huo Mkuu huyo wa Wilaya aliimba akichana ‘Vina’ Mistari ya Viwango vya bigwa wa Rhymes 2004  Mwana Morogoro Seleman Msindi Afande Sele.

 

 Safari hii ‘Big Bos’ huyo wa Wilaya alishangiliwa na mashabiki wote wakiwemo wa Simba, Yanga, Damu chafu na Chaka Bovu huku baadhi yao  wakipaza sauti wakihitaji Mh Kilakala aendelee kuwapa burudani.

Hata hivyo kwa kuheshimu Muda Mkuu huyo aliyechana mistari hiyo kwa takribani dakika 1 alitejesha Mic kwa Mc na mbungi akaendelea.

Baada ya gemu hiyo kutamatika kwa Damu chafu kuibuka na ushindi wa bao 3-0 Mtandao huu ulizungumza na baadhi ya mashabiki wa simba na yanga.

 Wa kwanza kuzungumza ni shabiki wa Simba Juma Abdul” kwa kauli ile mmoja kwa moja Mheshimiwa ni Yanga damu sasa tumkumbushe. kwenye Fainali hii aliyosema tutawapata wachezaji wa Yanga pekee tumuambie hakuna mchezaji yoyote wa Yanga  aliyepatikana au atakayepatikana kwenye mashindano haya zaidi ya  wachezaji wa Simba.

 

  Leo kwenye benchi la Damu chafu yupo Shiza Kichuya aliyeifunga Yanga mara kibao kwa mipira ya mbali kona. Ally Mustaph’ Barthez’ kafukuzwa Yanga kwa sababu ya magori ya kona ya Kichuya.

 

Kwenye fainali ya Mwaka jana  mshandano haya haya Damu Chafu imetoa beki kisiki wa Simba Abdulrazack Spear Hamza”

Kwa upande wake Shabiki wa Yanga Joseph Adinani alisema”Maneno ya Mkuu wetu wa wilaya yana maana kubwa sana na yaheshimiwe na watu wote”

Kwenye gemu hiyo Kichuya aliingia kipindi cha pili na wakati Mkuu wa Wilaya akiyasema hayo Mtandao huu ulimkodolea Macho Kichuya   alicheka  huku  akiinamia chini.

Pichani Mkuu huyo wa Wilaya akichana Mistari

TUKIO LA DABI YA YANGA NA SIMBA LAIBUKIA KWENYE NDONDO CUP







                                                Mshasha

 
                            Na Dustan Shekidele Morogoro.
 
HII ni kama ile Pelnati aliyosababisha kipa wa Simba Mussa Kamara kwenye mchezo wa Dabi kati ya Yanga na Simba uliopigwa Jumatano iliyopita uwanja wa Mkapa Dar na mnyama simba kupokea kichapo cha bao 2-0. 
 
Kwenye tukio hilo Kipa wa Simba Kamara akiwa ndani ya boksi aliacha mpira na kuuvaa mwili wa Kiungo ‘fundi’ wa Yanga Pacome na Mwamuzi wa mchezo huo kutoka Misri aliamulu mkwaju wa pelnati.
 
Pacome aliyekuwa mwiba mchungu kwa Simba kwenye mchezo huo alibeba jukumu la kupiga Pelnati hiyo aliyoipiga kiufundi na kuipatia timu yake bao la kwanza. 
 
Tukio kama hilo limetokea kwenye mchezo wa Fainali ya Planet Ndondo Cup kati ya Damu Chafu Fc na Chaka Bovu Fc
Mshambuliaji hatari wa Damu Chafu Johasson Clement Mshasha aliingia ndani na boksi na mpira ukiwa kwenye himaya yake akijiandaa kufunga Kipa wa Chaka bovu Tobah Kutisha anayeitumiki Mtibwa Sugar kwa kushilikia na na beki wake waliacha mpira na kumvaa Mshasha, refa wa mchezo huo Afande wa jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro Athuman Lazi ambaye ni mwamuzi wa zamani wa Ligi Kuu alimeza filimbi akimaanisha hakuna faulo
Ifahamike Mshasha alikuwa mchezaji nyota ya Mawenzi Market ya Mkoani hapa, baada ya timu hiyo kushuka daraja kutoka la kwanza kwenda la Pili wamiliki wa timu hiyo wafanyabiashara wa Soko la Matunda la Mawenzi waliamua kuiuza timu hiyo kwa Mwanasiasa maarufu mkoani Singida.
Mshasha alihamishiwa kwenye timu ya DTB Fc baadae ikabadilishwa jina ikaitwa Singida Big Stars wakati huo ikiwa daraja la pili, yeye na Hamis Tambwe waliipandisha Ligi kuu, Tambwe akiwa klnara wa ubachikaji mabao na Mshasha akishika nafasi ya pili.
Baada ya kupanda Ligi Kuu ,Mshasha na Tambwe waliachwa kwenye timu hiyo iliyosajiri wachezaji wengi nyota kutoka mataifa mbali mbali ikiwemo mataifa yanayoongoza kwa ubora wa Soka Duniani Brazil na Argentina

 

Sunday, June 29, 2025

WAKATI TIMU YAKE IKIJINDAA NA MCHEZO WA PLAYOFFS.MCHEZAJI WA FOUNTAIN GATE AONEKANA KWENYE NDONDO CUP MOROGORO








 

  

      Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 WAKATI  timu yake ya Fountain Gate Fc akijiandaa kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili wa Mtoano kubaki Ligi Kuu ‘Playoffs’dhidi ya Tanzania Prinsns utakafanyika kesho Jumatatu Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, mshambuliaji tegeo wa timu hiyo Salum Kihimbwa ‘Chuji’amenaswa na kamera za Mtandao huu akiitumikia timu ya Chaka Bovu kwenye mchezo wa Fainali ya Michuano ya Planet Ndondo Cup uliofanyika juzi Ijumaa kwenye Uwanja wa Saba saba Mkoani hapa. Kwenye mchezo wa Mkondo wa kwanza uliofanyika Alhamisi iliyopita nyumbani kwa Fountain Gate Manyara timu hiz zilitoka sale ya bao 1-1 Wajera jera Prinson wakiwa na faida ya gori a Ugenini Kwenye matokeo ya Jumla mshindi atabaki Ligi Kuu huku aliyeshindwa atekwenda kucheza Playoffs nyingine na timu ya Daraja kwanza Stend United Chama la Wana inayomilikiwa na wafanyabiashara wa Stend ya Mabasi ya Shinyanga.

 

Chapu kwa haraka wakati timu zikielekea Mapunziko Mtandao huu ulimfuata mchezaji huyo na kumuliza kulikoni timu yake inapigania kubaki Ligi kuu yeye yuko Morogoro kwenye Ndondo Cup.

 

Kihimbwa aijibu kwa Mkato “ Jumatatu sitakwenda kwenye mchezo huo nimeludia nyumbani Morogoro”

          HISTRIA FUPI YA KIHIMBWA

Amesajiiwa na Polisi Morogoro sasa [Polisi Tanzania] yenye maskani yake Kilimanjaro akitokea timu ya daraja la Pili ya Mkamba Ranger ya Kilombero.

 

Baada ya Polisi Moro Kushuka Daraja Kihimbwa akitimkia Mtibwa Sugar,huko aliitumikia timu hiyo takribani Misimu mitatu kabla ya kuihama na kujiunga na Tanzania Prinsons.

 

 Alidumu kwa maafande hao  kwa msimu mmoja kabla ya kujiunga na ile Ihefui ya Moto ya Kocha Zuberi Katwila kabla na kuikimbia timu hiyo Mashamba ya mpunga Mbarali Mbeya na kujiunga na Fountain Gate anayoitumikia mpaka sasa.

 

Juzi kwenye mchezo huo wa Fainali uliotamatika kwa Damu Chafu kuichapa Chaka Bovu chuma 3-0 Afande ‘Voda fasta’  lbrahim Pinto aliyekuwa uwanjani hapo akilinda usalama wa Raia na Mali zao. baada ya kumuona Kihimbwa aliyecheza naye Polisi Moro alimvaa na kusalimiana naye kama walivyo naswa na kamera za Mtandao huu.

IMEISHA HIYOO DAMU CHAFU MABINGWA WA PLANET NDONDO CUP 2024-2025

                        Timu zikiingia uwanjani      

Mkuu wa Wilaya Mhe Mussa Kilakala akizungumza kabla ya gemu hiyo kuanza

             Warembo wakiingiza kombe uwanjani
kiksosi cha Damu Chafu kiichoanza juzi Shiza Kichuya alingia kipindi cha pii
Rais wa Damu Chafu Ayub kati dakika zote 90 alikuwa bize na vijana wake kuzunguka uwanja wa saba saba. Alipofika gori la kaskazini mwa uwanja alisimama na kusalimiana na Mpiga picha wa Mtandao huu

Sales Manager wa Kings Super Brands Limited Geofrey Karumura kulia akimkabidhi Mfano wa hundi ya Milion Mbili Nahodha wa Chaka Bovu Fc George Chota
.....Mhe Mussa Kilakala kushoto akimkabidhi  mfano wa hundi ya Milion 4 Nahodha wa Damu Chafu Sady Mapuya
,,,,Nahodha wa Makombe Sady Mapuya akiwa na kombe
              Mabingwa Damu Chafu wakiwa na Mwali wao

 


     Na Dustan Shekidele Morogoro.

TIMU ya Damu Chafu Fc ikiongozwa na Shiza Ramadhan Kichuya’ Mzee wa Kona gori’ jana wamefanikiwa kutetea ubingwa  wa Michuano ya Planet Ndondo Cup 2025,baada ya kuinyuka timu ya Chaka Bovu Fc ‘Vijana wa Nickson Kibabage kwa bao 3-0.

 

Hadi dakika 45 za awari zinatamatika kwenye gemu hiyo iliyopigwa uwanja wa Saba saba na kushuhudiwa na Umati Mkubwa wa mashabiki walioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe Mussa Kilakala washindi walikuwa mbele kwa bao 1-0 zilizopachikwa dakika ya 12 na Clement Mshasha mchezaji wa zamani wa Singida Big Stars.

 

Chama la Masela Damu Chafu ambao mwaka jana wakiwa na beki wa Simba Abdrazack Spear  Hamza walitwa ubingwa huo kwenye uwanja huo huo wa Saba saba walikianza kipindi cha pili kwa kasi ya SGR na kufanikiwa kuongeza mabao mawili ya haraka haraka. 

 

Baada ya gemu hiyo kutamatika Mgeni Rasmi  Mhe Mussa Kilakala alimkabidhi kombe Nahodha wa Damu Chafu Sady Mapuya na kiticha cha pesa Milioni 4 kwa mfumo wa hundi.

 

Nahodha wa Chaka Bovu George Chota anayeitumikia Mtibwa Sugar alikabidhiwa Milioni 2  na Geofrey Karumuna ambaye ni Meneja Mauzo wa kamuni ya Kings Super Brands Limited.

Kampuni hiyo inayojihusisha na utengenezaji wa Pombe ni mmoja ya wadhamini wa mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 4 za Black People, Damu Chafu, Wakushi na Chaka Bovu.

 Wakihojiwa na Planent Redio siku mbili kabla ya fainali hiyo Viongozi wa Chaka Bovu walisema kwamba endapo wangefanikiwa kutwaa ubingwa huo na kukabidhiwa kitita hicho cha Milioni 4 wangefanya yafuatayo,

Mosi wangetoa sadaka ya kununua Luku ya elfu 50 kwa misikiti 5 kila msikiti mmoja ikipewa Luku ya elfu 50,

 

Pili wangeso duwa ya kuwarehemu marehemu ambapo dua hiyo ingekwenda sambamba ba sadaka ya chakula’

 

Chaka Bovu walitinga fainali baada ya kuwafunga  Wakushi na Damu chafu waliwafunga Black People.

Wiki iliyopita Mtandao huu ulikutana na Rais wa Black People Seif Kijiji nyuma ya Kanisa la TAG Mwembesongo na kumuliza sababu za kufungwa na Damu Chafu alijibu hivi.

“Shekidele kwenye gemu ile nilicheza na timu nne kwa mpigo ndio maana nimezidiwa Damu Chafu alisaidiwa na timu za Chadongo, Burkinafaso na Asseple Fc timu zote hizo zinatoka Mafisa kata ya Mwembesongo n azote zimekufa ila viongozi wao wapo” alisema Seif.

Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matuki kibao kwenye fainai hiyo hivyo endelea kuwa jirani na mtandao huu muda wote.

Wednesday, June 25, 2025

KIJIWE NONGWA. UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA













 


Na Mpekunyuzi wa Mitandao Dunstan Shekidele.
 
Kama kawaida mtumishi wako, kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijamii kukusanya jumbe mbali mbali.
 
Miongoni mwa jumbe hizo ni za Kuelimisha, Kukosoa na Maneno ya hekima yanayotukumbusha kuwa jirani na Mwenyezi MUNGU.
Tukutane Wiki Ijayo kwa mabango Mengine yenye Jumbe Moto Moto.

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...