Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WAKATI timu yake ya Fountain Gate Fc akijiandaa kucheza mchezo wa Mkondo wa Pili wa Mtoano kubaki Ligi Kuu ‘Playoffs’dhidi ya Tanzania Prinsns utakafanyika kesho Jumatatu Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, mshambuliaji tegeo wa timu hiyo Salum Kihimbwa ‘Chuji’amenaswa na kamera za Mtandao huu akiitumikia timu ya Chaka Bovu kwenye mchezo wa Fainali ya Michuano ya Planet Ndondo Cup uliofanyika juzi Ijumaa kwenye Uwanja wa Saba saba Mkoani hapa. Kwenye mchezo wa Mkondo wa kwanza uliofanyika Alhamisi iliyopita nyumbani kwa Fountain Gate Manyara timu hiz zilitoka sale ya bao 1-1 Wajera jera Prinson wakiwa na faida ya gori a Ugenini Kwenye matokeo ya Jumla mshindi atabaki Ligi Kuu huku aliyeshindwa atekwenda kucheza Playoffs nyingine na timu ya Daraja kwanza Stend United Chama la Wana inayomilikiwa na wafanyabiashara wa Stend ya Mabasi ya Shinyanga.
Chapu kwa haraka wakati timu zikielekea Mapunziko Mtandao huu ulimfuata mchezaji huyo na kumuliza kulikoni timu yake inapigania kubaki Ligi kuu yeye yuko Morogoro kwenye Ndondo Cup.
Kihimbwa aijibu kwa Mkato “ Jumatatu sitakwenda kwenye mchezo huo nimeludia nyumbani Morogoro”
HISTRIA FUPI YA KIHIMBWA
Amesajiiwa na Polisi Morogoro sasa [Polisi Tanzania] yenye maskani yake Kilimanjaro akitokea timu ya daraja la Pili ya Mkamba Ranger ya Kilombero.
Baada ya Polisi Moro Kushuka Daraja Kihimbwa akitimkia Mtibwa Sugar,huko aliitumikia timu hiyo takribani Misimu mitatu kabla ya kuihama na kujiunga na Tanzania Prinsons.
Alidumu kwa maafande hao kwa msimu mmoja kabla ya kujiunga na ile Ihefui ya Moto ya Kocha Zuberi Katwila kabla na kuikimbia timu hiyo Mashamba ya mpunga Mbarali Mbeya na kujiunga na Fountain Gate anayoitumikia mpaka sasa.
Juzi kwenye mchezo huo wa Fainali uliotamatika kwa Damu Chafu kuichapa Chaka Bovu chuma 3-0 Afande ‘Voda fasta’ lbrahim Pinto aliyekuwa uwanjani hapo akilinda usalama wa Raia na Mali zao. baada ya kumuona Kihimbwa aliyecheza naye Polisi Moro alimvaa na kusalimiana naye kama walivyo naswa na kamera za Mtandao huu.
No comments:
Post a Comment