Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, June 30, 2025

MKUU WA WILAYA ACHANA MISTARI KWENYE NDONDO CUP.





 


    Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MKUU wa Wilaya ya Morogoro Mh Mussa Kilakala Ijumaa iliyopita alikuwa kivutio  kwa mashabiki kibao waliofulika  Uwanja wa Saba saba kushuhudia Fainali ya Planet Ndondo Cup, baada ya mkuu huyo kuchana mistari ya Viwango.

 

Kiongozi huyo ‘Janki’ aliyekuwa mgeni Rasmi kwenye fainali hiyo, baada ya kuwakagua wanafainali Damu Chafu Fc na Chaka Bvu Fc alikabidhiwa Mic kuzungumza na wananchi wake waliofulika uwanjani hapo.

 

 Baada ya salamu Mh Kilakala aliwatania Mashabiki wa Simba na Yanga akisema”

Kwenye fainaili tunaweza kupata vipaji kama vya Pacome,Job, Mzize Aucho na Chama

Hatutegemei kuona Vipaji kama vya Mpanzu na Kibu D”

 

 Utani huo aliamsha shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki wa Yanga waliompa zawadi ya Makofi na Vigeregere huku mashabiki wa Simba wakipiga kimya wakizuka kwa kuchati na simu zao baadhi yao wakiwa na viswaswadu kama sio vitochi.

 

Baada ya utani huo Mkuu huyo wa Wilaya aliimba akichana ‘Vina’ Mistari ya Viwango vya bigwa wa Rhymes 2004  Mwana Morogoro Seleman Msindi Afande Sele.

 

 Safari hii ‘Big Bos’ huyo wa Wilaya alishangiliwa na mashabiki wote wakiwemo wa Simba, Yanga, Damu chafu na Chaka Bovu huku baadhi yao  wakipaza sauti wakihitaji Mh Kilakala aendelee kuwapa burudani.

Hata hivyo kwa kuheshimu Muda Mkuu huyo aliyechana mistari hiyo kwa takribani dakika 1 alitejesha Mic kwa Mc na mbungi akaendelea.

Baada ya gemu hiyo kutamatika kwa Damu chafu kuibuka na ushindi wa bao 3-0 Mtandao huu ulizungumza na baadhi ya mashabiki wa simba na yanga.

 Wa kwanza kuzungumza ni shabiki wa Simba Juma Abdul” kwa kauli ile mmoja kwa moja Mheshimiwa ni Yanga damu sasa tumkumbushe. kwenye Fainali hii aliyosema tutawapata wachezaji wa Yanga pekee tumuambie hakuna mchezaji yoyote wa Yanga  aliyepatikana au atakayepatikana kwenye mashindano haya zaidi ya  wachezaji wa Simba.

 

  Leo kwenye benchi la Damu chafu yupo Shiza Kichuya aliyeifunga Yanga mara kibao kwa mipira ya mbali kona. Ally Mustaph’ Barthez’ kafukuzwa Yanga kwa sababu ya magori ya kona ya Kichuya.

 

Kwenye fainali ya Mwaka jana  mshandano haya haya Damu Chafu imetoa beki kisiki wa Simba Abdulrazack Spear Hamza”

Kwa upande wake Shabiki wa Yanga Joseph Adinani alisema”Maneno ya Mkuu wetu wa wilaya yana maana kubwa sana na yaheshimiwe na watu wote”

Kwenye gemu hiyo Kichuya aliingia kipindi cha pili na wakati Mkuu wa Wilaya akiyasema hayo Mtandao huu ulimkodolea Macho Kichuya   alicheka  huku  akiinamia chini.

Pichani Mkuu huyo wa Wilaya akichana Mistari

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...