Na Dustan Shekidele,Morogoro.
UTAFTI wa kienyeji uliofanywa na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Morogoro umebaini kwamba rangi ya ukindu ni kinga sahihi ya vifaranga vya kuku kukamatwa na Ndege Mwenye Maafufu ‘Kipanga’.
Kufuatia hali hiyo wiki hii Mwandishi wa habari hizi aliingia mtaa kuichimba habari hiyo ambapo juzi alikatiza Mtaa wa Mafisa Mwanzo Mwisho Kata ya Mwembesongo na kushuhudia Vifaranga vya kuku vikiwa na rangi hiyo ya ukindu.
Taarifa zinadai baada ya kuzaliwa vifaranga hivyo vilitumbukizwa kwenye kopo lenye rangi ya Ukindu kwa lengo la kuvilinda visikamatwe na Mwewe.
Akizungumza na Mtandao huu mmoja wawananchi wa Mkoa wa Morogoro Asha Juma alisema” Kwa umavyojua kwa sasa biashara ya kuku wa kienyeji imekuwa nzuri sana, bei ya chini Jogoo ni elfu 30, na teteza kwa maana ya kuku jike ni elfu 20.
Sasa tuna vita kali na Mwewe kuku anaweza kufyatua vifaranga 11 utakuta viwili tu ndio vinakua vingine vyote vinaliwa na Mwewe, hivyo tumebuni mbinu hii ya kuvipaka ukindu ambao unamzuia Mwewe kukamata vifaranga”alisema Bi Mkubwa huyo na kuendelea kudadavua.
“ Ukienda Vijijini ambako kuna Mwewe wengi mfano Mikese, Kiloka, Mkambarani. Ubena, Bwawani. Gwata unaona wafungaji wengi wa kuku wanatumia mbinu hiyo ya ukindu.”alimalizia kusema Mama huyo. Alipoulizwa kitu gani kinachomfanya Ndege huyo aina ya Mwewe, kuogopa kuvikamata vifaranga hivyo vya Ndege aina ya Kuku.?
Alijibu “Kwa Mujibu wa utafiti wetu wa kienyeji Mwewe haipendi harufu ya rangi ya ukindu”
UKINDU NI NINI.
Ukindu ni rangi ya mkeka ambayo pia kwa baadhi ya wafanyabiashara wa mbao wasio waaminifu huitumia kupaka kwenye mbao na kuwadanganya wateja wao kama ni dawa ya mchwa na wadudu wanaopekecha mbao.
Ushauri na Mwandishi wa habari hizi kwa wanunuzi wa mbao kwa lengo la kupaua nyumba zao, kama unamshaka na anayekuuzia mbao hizo ni hari ununue dawa hiyo ya mchwa Og wewe mwenyewe inauzwa bei mbaya kikopo kidogo elfu 20 na kopo kubwa elfu 40.
Matumizi ya dawa hiyo ili iwe kali zaidi kopo dogo unachanganya na maji lita 20 unaloweka mbao hizo kwenye maji hayo yenye sumu kwa dakika 20 mbao hizo zitakunywa maji hayo yenye sumu hiyo kiboko ya mchwa na wadudu wanaokula mbao.