Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, April 30, 2025

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI, MAISHA MAPYA YANGUSHA MOJA MOJA UKUMBINI.






 


Na Mlala Nje Dustan Shekidele,Morogoro.

 BAND ya Maisha Mapya’Vijana wadogo waliokomaa Vichwa kwa Ugumu wa Maisha’ Wiki End iliyopita wameuwasha Moto kwenye ukumbi Mmoja uliopo Msamvu Iringa Road kwa kuangusha moja moja mpaka Majogoo yalipowika mara tatu.

Baada ya kuwapagawisha mashabiki ‘Big Boss’Mmiliki wa Band hiyo Joshua Malekela Maafuru Joshkela Msingisi Mwamba kutoka Kijiji cha Msingi Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, aliacha kuimba akanyoosha mkono juu kuashiria vijana wake wamtwangie Sebene kavu.

Hapo sasa Joshua  kutupa Mic Chini akaanza  kunengua akijigaragaza chini huku akiteleza kwenye jukwaa kama kambara kwenye tope.

Kwa umahiri huo baadhi ya Mashabi walivutiwa na shoo hiyo wakaamua kunyanyuka kwenye viti na kumtunza pesa.

Wiki End ijayo Mlala Nje atahudhuria shoo ya Band ya Waluguru Original.kusaka matukio.

Mpendwa Msomaji wa Mtandao pendewa wa Shekidele kile kipengele chetu cha stori kali ya Mtaa kitaendelea hivi karibu ambapo Mtandao huo umenasa habari kali ya Kitaa.

 Kwa sasa Mwandishi wa Mtandao huu anakamilisha Stori hiyo kwa kumsaka Askofu wa Kanisa kutoa ufafanuzi wa habari hiyo hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kufuatilia habari hiyo kubwa kwenye Jamii yetu.

 

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...