Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, April 23, 2025

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE SIKU KUU YA PASAKA. RUVU STARS BAND YAKINUKISHA MOROGORO.











 


Na Mlala Nje Dustan Shekidele,Morogoro.

KUSHEHEREKEA Siku kuu ya Pasaka Band ya Ruvu Stars’Wazee wa Kuku na Mayai yake’ kutoka Mkoa wa Pwani, Jumapili ya Pasaka wameuwasha Moto mkali kwenye ukumbi wa Florida uliopo Msamvu Mkoani hapa.

Kama kawaida kwenye siku kuu hiyo ya Pasaka ambayo Wakristo wote duniani walisheherekea kufufuka kwa Mokozi wao Yesu Kristo’Nabii Issa’ aliyeishinda mauti na kuushangaza ulimwengu  baada ya kuuwawa kikatili na watesi wake kisha akafufua ndani ya siku tatu toka alivyozikwa, Mlala Nje alizunguka kumbi za Starehe kusaka matukio.

 Kwenye shoo hiyo kivutio kikubwa kilikuwa kwa Wanenguaji wa Band hiyo ambao walikongo nyoyo za mashabiki waliojazana kwenye ukumbi huo uliopo jirani na Stend ya Mabasi ya Mikoani ya Msamvu.

Moja ya Vionjo vya madensa hao ni kurusha sarakani jukwaani eneo na kupanda juu ya nguzo za jukwaa na kunengua wakiwa huko huko kirereni mwa nguzo hizo za plastiki.

Akihojiwa na Mlala Nje Kiongozi wa band hiyo  Mponda Mahmoud Maarufu MK Masauti[Pichani mwenye Mic mdomoni na flana nyeupe] amesema wamefunga safari kutoka Ruvu  kuja Morogoro kutoa burudani ya viwango kwa mashabiki wa Mji kasoro bahari[Morogoro].

Baada ya kukamilika kwa shoo hiyo majira ya saa 9 usiku Vijana hao wa Ruvu waliingia kwenye Lori la Jeshi na kurejea Ruvu Mkoa wa Pwani kwa kuendeleza burudani kwenye viwanja vya maeneo hayo.

 

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...