Beki kisiki wa Mangolo Fc Sady Mapuya akimiliki mpira huku akinyemelewa na mshambuliaji wa Washashi Fc Shani Adrew ambaye alikuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Mangolo.
Ifahamike Mapuya alikuwa beki kisiki wa Lipuli ya Iringa wakati huo ukishiriki Ligi kuu, baada ya timu hiyo kushuka daraja Mapuya aliikimbia na kurejea nyumbani kwao Morogoro ambapo kwa sasa anaitumikia timu ya Moro Kids inayoshiriki Ligi daraja la Pili akiwa Nahodha wa kikosi hicho.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
ROBO Fainali ya kwanza ya Ligi za Mtaani Maarufu ‘Ndondo Cup’ iliyozikutanisha timu mbili kutoka Mtaa mmoja, Mangolo Fc na Washashi Fc umepigwa jana Uwanja wa Saba saba kwa Mangolo kuibuka na ushindi wa Pelnati 7-6 baada ya dakika 90 miamba hiyo kutoka suluu 0-0.
Timu hizo zilizosheheni wachezaji wengi nyota nchini zinatoka eneo mmoja zikitengwanisha na shule ya Msingi Mwembesho, Maskani ya Mangolo ipo eneo la uwanja wa michezo wa shule hiyo huku Maskani ya Washashi ikiwa geti kuu la kuingia kwenye shule hiyo. .
kwenye Mtanange’Derby’ hiyo iliyokuwa ‘tamu’ kwa muda wote wa dakika 90 Video Assistart Referee[VAR] ya Mtandao wa Shekidele iling’amua tukio moja tata lililosababishwa na na beki wa Mangolo Fc ambaye pia ni mchezaji wa Tabora United inayoshiriki Ligi kuu.
Tukio hilo litaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment