Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, April 27, 2025

VAR YA MTANDAO WA SHEKIDELE IMEBAINI TUKIO HILI.

                   Nassirin Kombo beki wa Tabora United










 

.

   Na Dustan Shekidele,Morogoro.

KWENYE Berby ya juzi ya Michuano ya Ndondo Cup,kati ya Mangolo Fc na Washashi Fc iliyopigwa uwanja wa Saba saba Mkoani hapa na timu hizo kutoka eneo Moja la Mwembesongo  zilitoka Suluu ya 0-0.

Dakika 67 beki wa Mangolo Fc Nassiri Kombo Maarufu ‘Nasri Sccoba’ambaye ni mchezaji wa timu ya Tabora United akijiunga na timu hiyo msimuu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Manungu  Kata ya Mtibwa Tarafa ya Turiani Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

Akijiamini huku akiwa mtu wa Mwisho aliuchezea mpira nje ya 18 na kujikuta akinyang’anywa na Winga wa Washashi Shani Adrew aliyemzunguka na  kuingia ndani ya 18.

 

 Wakati winga huyo mwenye mbio kama swala akijiandaa kufunga Nasri Sccoba alimkwatua kwa nyuma na kuanguka chini akiuacha mpira ukinyakwa kirahisi na Kipa.

Kwa Mujibu wa sheria 17 za Soka tukio hilo lilipaswa kuwa  Pelnaty lakini Mwamuzi wa mchezo huo alipeta akiashiria hakuna fau, tukio hilo lilisabisha Rais wa Washashi Fc kuingia uwanjani akitaka kumpiga refa.

Kabla ya kumkaribia refa huyo baadhi ya wachezaji wa Washashi walimdaka kiongozi wao huyo na kumtoa nje ya uwanja na mpira ukaendelea na kutamatika kwa Suluu.

Kwa sababu mchezo huo ni lazima mshindi apatikane timu hizo ziliingia kwenye kipengele cha kupigia mikwaju ya pelnati ambapo Mangolo Fc ‘Vijana wa Dida Masela’ walifanikiwa kutinga Nusu fainali baada ya kuwafunga Washashi kwa Pelnati 7-6.

Mpiga picha wa Mtandao aliyekuwa uwanjani hapo na kamera yake ya kisasa yenye Viwango vya VAR [Video Assistart Referee] alirekodi tukio hilo hatua kwa hatua kila picha moja ilipiga kwa sekundi 1 hivyo ndani ya sekunde 11 kamera hiyo yenye uwezo wa kwenda na kasi ya mpira ilipiga picha 11 kama zinavyoonekana pichani.

Pia kamera hiyo inauwezo wa kupiga picha umbari  wa mita 300 kwa wakazi wa Dar es salaamu umbali huo ni kama kutoka Ubungo Plaza Mpaka Manzese Darajani ‘Tip Top’.

 Kwa wakazi wa Morogoro umbali huo ni  kutoka Msamvu Shule eneo la Mtaa  Mpaka Msamvu Stend ya Mabasi, wahenga wana sema kujisifu sio dhambi ila dhambi ni kuziendekeza hizo sifa.

Hivyo kama una sherehe yako yoyote wasiliana na Mpiga picha wa Mtandao huu kwa namba 0754 28 90 73. Whatssap No 0715 289073 bei zake ni karibu na bure,ma anazingatia utu zaidi kuliko biashara.

 

   

No comments:

Post a Comment

MAKALA PLANET NDONDO CUP. SIRI DAMU CHAFU KUTWAA UBINGWA MARA MBILI MFURULIZO HII HAPA.

  Baadhi ya mashabiki waliofulika kwenye mashishindano hayo.                           .....Kikosi cha Damu chafu Mkuu wa Wilaya Mhe Kilakal...