Mwenyekiti Marry Kachale mwenye mtandio Mweusi akizungumza na Mtandao huu.Shuhuda wa
tukio hilo Mariam Athuman akimuonyesha Mwandishi wa Mtandao huu ukuta huo na jiwe
ambalo dent huyo alikuwa akisugua miguu.
Na
Dustan Shekidele,Morogoro.
KAMA kawaida
kipengele pendwa cha habari kali ya kitaa kupitia mtandao pendwa wa Shekidele,
kinaendelea Leo ijumaa kwa habari ya kuumiza moyo.
Mwanafunzi ‘Dent’
anayesoma darasa la Tatu shule ya Msingi Mtawara Mkoani hapa, Mwahawa Mohamed
Mkubwa[10]amenusulika kifo baada ya kuangukiwa na ukuta uliopojirani na nyumba
anayoishi.
Tukio hilo la
kusigitisha limetokea wiki iliyopita majira ya saa 12 asubuhi Mtaa wa Mfunguakinywa Kata ya Mwembesongo, Wakati
Dent huyo akisugua miguu kwenye jiwe akijiandaa kwenda shule.
Baada ya
kutokea kwa tukio hilo mmoja wa wananachi Ramadhani Mtagwa alitoa taarifa sahihi kwa
Mwandishi wa habari hizi akisema.
”Shekidele
njoo hapa Magolo Mtaa wa Mfunguakinywa mtoto
kangukiwa na ukuta muda huu watu wanahangaika kumchomoa kwenye kifusi” alisema
Rama Mtangwa ambaye Hayati Jela Mtagwa mchezaji nyota wa Pani na timu ya Taifa
ya Tanzania ni baba yake Mdogo.
Bila
kuchelewa Fasta Mwandishi wa habari hizi alipiga gia pikipiki yake ya Mwendo
kasi na kutinga eneo la tukio ndani ya dakika 0.
Alipofika alikuta tayari dent huyo amefukuliwa kwenye
kifusi hicho na kukimbizwa hospital ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa usafiri wa
boda boda.
Akihojiwa na
Mtandao huu shuhuda wa tukio hilo Bi.Mariam Athuman alikuwa na haya kusema.
” Kwa siku
nyingi huu ukuta wa jirani yetu ulikuwa hatarishi ulipinda upande mmoja pia ulikuwa
na ufa mkubwa tulitoa taarifa kwa mwenyekiti wa Mtaa ambaye alimjulisha mmiliki
wa nyumba cha ajabu mwenyenyumba huyo hakuchukua hatua yoyote ya kuukarabati
hadi ulipomuangukia huyu mtoto hii.
Saa 12
watoto waliamka wakijianda kwenda shule baada ya kupiga mswaki walisugua miguu kwenye hili jiwe ambalo lipo
chini ya ukuta chaajabu wakati Mwanahawa anaendelea kusugua miguu ghafra ukuta
huo ulianguka na kumfunika” alisema shuhuda huyo na kuendelea kutema nyongo.
“Tumepiga
nayowe watu wamejaa tukafanikiwa kumchomoa kwenye kifusi lakini chaajabu hakutoka damu
yoyote kama unashuhudia Mwandishi amefunikwa hata lakini hakuna hata tone moja la
damu muda huu tumekodi boda boda mama yake kamkimbiza hospital”amemalizia
kusema mama huyo ambaye ni mama mwenyenyumba anayoishi mtoto huyo.
Siku
iliyofuata Mwandishi wa habari hizi alitinga hospital kwa lengo la kumjulia
hali mgonjwa sambamba na kuzungumza na
Mama yake.
Mwandishi
alipofika wodi namba 4 alipolazwa dent huyo alielezwa mtoto huyo ameingizwa chumba cha upasuaji.
“Huyo mtoto hali
yake ni mbaya sana baada ya kuangukiwa na ukuta damu ilivia ndani hivyo muda
huu wanamfanyia upasuaji kutoa damu iliyoganda
na kumuwekea damu mpya kwa sasa ndugu wanahaha kumchangia damu ”alisema
jirani mmoja aliyekuwepo hospitalini hapa.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa huo Marry Kachale amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“ Ni kweli
shekidele mkazi wangu Mwanahawa Mkumba anayesoma darasa la tatu Mtawara ameangukiwa
na ukuta, muda huu huko hospitali nitafute baadae tuongee zaidi”alisema
Mwenyekiti huyo.
Mama mzazi
wa Mtoto huyo Gresi Fred Kaloli ameahidi kuzungumza na Mwandishi wa habari hizi
atakapotoka wodini, hivyo endeleo kuwa jirani
na mtandao huu kupata ’Hapdet’muendelezo ya habari hii ya kusigitisha pia kwa
upande wa Mwenyekiti naye sijamalizana naye kuna maswali kadhaa nitamuliza kuhusiana na
tukio hilo.