HABARI ZA KIJAMII, SIASA,MICHEZO BURUDANI HADITHI NA MAKALA
Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73
Monday, March 10, 2025
MAMA ASIMULIA MAZITO BAADA YA KUTOKA CHUMBA CHAUPASUAJI NA MWAE ALIYEANGUKIWA NA UKUTA.
Gresi Kaloli akizungumza na Mtandao huu huku akiwa na na Mwane
Dent Mwahawa Mohamed baada ya kutoka hospital
Mwenyekiti wa Mtaa Marry Kachale
Shuhuda Mariamu Athuman akiangalia ukuta huo
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MAMA wa Dent wa la 3 aliyeangukiwa
na ukuta Bi. Gresi Fred Kaloli, amefunguka mazito baada ya kutoka chumba na upasuaji[Thieta]na Mwanae Mwanahawa
Mohamed Mkumba[10laliyeangukiwa na ukuta wiki iliyopita.
Juzi Mtandao huu uliripoti tukio hilo na kuahidi kuendelea na habari hii
kwa kuzungumza na Mama mzazi wa Dent huyo ambaye wakati habari hiyo ikienda
mitamboni Mwanafunzi huyo anayesoma dasara la tatu shule ya Msingi Mtawara
Mkoani hapa alikuwa Thieta akipigania uhai wake.
Kwa Rehema za Mwenyezimungu Dent huyo aliyefanyiwa upasuaji mara mbili wa
kutolewa damu chafu iliyoganda mwilini baada ya kuangukiwa na ukuta uliopo
jirani na nyumbani kwao Alhamisi ya Februari 21.
Baada ya kutoka Thieta mahojiano na Mama huyo yalikuwa hivi.
Mwandishi. Awari ya wote pote kwa mkasi mzito uliomkuta Mwanao, ama baada
ya salamu na pole kwa faida ya wasomaji wa Mtandao pendwa wa Shekidele naomba
ujitambulishe majina yako kisha utueleze A-Z tukio hilo.
Mama wa Dent. Asante kwa kutupa pole pia tunashukuru kwa sababu umekuwa
Mwandishi wa habari wa kwanza kuja kutupa pole na kutuhoji kuhusiana na ajali
hiyo iliyompata mtoto wangu.
Siku ya tukio Alhamis kama kawaida Mwanangu Mwanahawa Mohamed Mkumbwa
mwenye umri wa miaka 10 anayesoma darasa la tatu Shule ya Msingi Mtawara
aliamka saa 12 kufanya maandalizi ya kwenda shule.
Wakati huo mimi nilikuwa kitandani nimelala, ghafra nasiki vilio na
makelele nikakarupuka nilivyotoka nje
nimemshuhudia mwanangu ameangukiwa na ukuta wa jirani,
Kama mzazi baada ya kushuhudia kundi la watu wakihangaika kumchomoa
mwanangu kwenye kifusi tumbo la uzazi lilinikata nikaanguka chini kwa bahati
wasamalia wema hao walifanikiwa kumtoa mwanangu akiwa hai tukakodi boda boda
boda tukamkimbiza hospital.
Baada ya masaa 3 mbele nilimuona mwanangu akizidi kuregea nilipomtazama
zaidi nilishuhudia macho yake yakiwa meupe kama pamaba, baada ya kumchunguza madaktari
wamebani damu imefia ndani ya mwili, hivyo waliamua kumfanyia upasuaji kutoa
damu chafu iliyoganda na kumuweka damu mpya”alisema Mama huyo na kuendelea
“Mwanangu alitoka Thieta siku iliyofuata ambayo nasiki ulikuja hapa
hospital kutuona aliingizwa tena Thieta kufanyiwa upasuaji wa pili baada ya
sehemu ya mgongoni nayo kuvia damu chafu.
Nashukuru jana tumetoka hospital kama unavyoona muda huu nimetoka
kumsafisha kwenye majeraha” haya ndio maelezo yangu
Mwandishi. Umetumilia shilingi ngapi kwenye matibanuna huyo mwenye ukuta amechangia kiasi gani?
Mama wa Dent. Mpasa sasa gharama zote ni Laki 7 na nusu nab ado tunatumia
usafiri wa kwenda hospital kila siku kuchukua dawa na kusafisha vidonda, huyo
Mwenyeukuta baada ya kubanwa sana ametoa laki moja toka atoe hiyo laki
sijamuona tena kuja kutuona,kipekee na washukuru madaktari na wauguzi wa
hospital ya Mkoa kwa kupigania uhai wa mwanangu pilinawashukuru watu mbali mbali walionichangia kwenye
matibabu hasa Mama Nyau mke wa diwani wetu pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa Mama
Marry Kachale wamejitoa sana mwisho niwashukuru wananchi waliopambana kumchomoa
mwangu kwenye ule ukuta.
Mwandishi. Taarifa nilizozipata eneo la tukio zinadai ukuta ule wa Tofari
za kuchoma ulikuwa hatarishi muda mrefu kwa nini uliruhusu Mwanao mara kwa mara
akasugue miguu kwenye jiwe lililopo chini ya ukuta huo hatarishi?
Mama Dent. Ni kwelie ukuta ule ulikuwa unaufa mkubwa na ulikuwa umepinda
tulimjulisha huyo jirani yetu mwenye
nyumba[Anamtaja jina] lakini hakuchukua hatua yoyote wengine waliamua kwenda
kumshitaki kwa mwenyekiti lakini bado hakuufanyia matengenezo mpaka
ulivyomuangukia mwangungu.
Kuhusu kumuacha mwangu asugue miguu pale kama ambavyo nilikuambia awari
wakati tukio linatokea mimi nilikuwa ndani nimelala hivyo sikumuona akisugua
miguu pale.
Mwandishi Ok asante kwa ushirikiano.
Mtandao huu kwa sasa unahifaddhi jina la Mmiliki wa ukuta huo kwa sababu
haja patikana kuzungumzia jambo hilo juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Baada ya kumsikia Mama huyo Mwandishi wa habari hizi aliludi tena kwa Mwenyekiti
wa Mtaa Mama Marry Kachale na Mahojiano yetu yalikuwa hivi.
Mwandishi. Samahani Mwenyekiti swala hili awari ulisharizungumzaia lakini
baada ya kuzungumza na Mama wa Mtoto nimepata maswali ambayo nahitaji majibu
kutoka kwako.
Je kama mkuu wa ulinzi na Aman
kwenyeMtaa
wako tukio hili umelipoti polisi?
Mwenyekiti. Ndio baada ya tukio nilimpigia OCD sikumpata nikampigia RPC
nikamueleza akaniambia ataniunganisha na Askari wa chini yake aje eneo la
tukio.
Mpaka muda huu sijamuona huyo Askari kwa sasa tuko bize na mgonjwa Mungu
akisaidia akipata nafuu tutalifuatilia jambo hilo nitakupa mrejesho Shekidele.
Mwandishi. Ok asante na hongera kwa kujitoa kwenye shida za wananchi wako.
Mwenyekiti. Asante hongera na wewe kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuripoti
habari za kijamii.
No comments:
Post a Comment