Shuhuda wa tukio hilo Mariam Athuman akimuonyesha Mwandishi wa Mtandao huu ukuta huo na jiwe ambalo dent huyo alikuwa akisugua miguu.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
KAMA kawaida kipengele pendwa cha habari kali ya kitaa kupitia mtandao pendwa wa Shekidele, kinaendelea Leo ijumaa kwa habari ya kuumiza moyo.
Mwanafunzi ‘Dent’ anayesoma darasa la Tatu shule ya Msingi Mtawara Mkoani hapa, Mwahawa Mohamed Mkubwa[10]amenusulika kifo baada ya kuangukiwa na ukuta uliopojirani na nyumba anayoishi.
Tukio hilo la kusigitisha limetokea wiki iliyopita majira ya saa 12 asubuhi Mtaa wa Mfunguakinywa Kata ya Mwembesongo, Wakati Dent huyo akisugua miguu kwenye jiwe akijiandaa kwenda shule.
Baada ya kutokea kwa tukio hilo mmoja wa wananachi Ramadhani Mtagwa alitoa taarifa sahihi kwa Mwandishi wa habari hizi akisema.
”Shekidele njoo hapa Magolo Mtaa wa Mfunguakinywa mtoto kangukiwa na ukuta muda huu watu wanahangaika kumchomoa kwenye kifusi” alisema Rama Mtangwa ambaye Hayati Jela Mtagwa mchezaji nyota wa Pani na timu ya Taifa ya Tanzania ni baba yake Mdogo.
Bila kuchelewa Fasta Mwandishi wa habari hizi alipiga gia pikipiki yake ya Mwendo kasi na kutinga eneo la tukio ndani ya dakika 0.
Alipofika alikuta tayari dent huyo amefukuliwa kwenye kifusi hicho na kukimbizwa hospital ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa usafiri wa boda boda.
Akihojiwa na Mtandao huu shuhuda wa tukio hilo Bi.Mariam Athuman alikuwa na haya kusema.
” Kwa siku nyingi huu ukuta wa jirani yetu ulikuwa hatarishi ulipinda upande mmoja pia ulikuwa na ufa mkubwa tulitoa taarifa kwa mwenyekiti wa Mtaa ambaye alimjulisha mmiliki wa nyumba cha ajabu mwenyenyumba huyo hakuchukua hatua yoyote ya kuukarabati hadi ulipomuangukia huyu mtoto hii.
Saa 12 watoto waliamka wakijianda kwenda shule baada ya kupiga mswaki walisugua miguu kwenye hili jiwe ambalo lipo chini ya ukuta chaajabu wakati Mwanahawa anaendelea kusugua miguu ghafra ukuta huo ulianguka na kumfunika” alisema shuhuda huyo na kuendelea kutema nyongo.
“Tumepiga nayowe watu wamejaa tukafanikiwa kumchomoa kwenye kifusi lakini chaajabu hakutoka damu yoyote kama unashuhudia Mwandishi amefunikwa hata lakini hakuna hata tone moja la damu muda huu tumekodi boda boda mama yake kamkimbiza hospital”amemalizia kusema mama huyo ambaye ni mama mwenyenyumba anayoishi mtoto huyo.
Siku iliyofuata Mwandishi wa habari hizi alitinga hospital kwa lengo la kumjulia hali mgonjwa sambamba na kuzungumza na Mama yake.
Mwandishi alipofika wodi namba 4 alipolazwa dent huyo alielezwa mtoto huyo ameingizwa chumba cha upasuaji.
“Huyo mtoto hali yake ni mbaya sana baada ya kuangukiwa na ukuta damu ilivia ndani hivyo muda huu wanamfanyia upasuaji kutoa damu iliyoganda na kumuwekea damu mpya kwa sasa ndugu wanahaha kumchangia damu ”alisema jirani mmoja aliyekuwepo hospitalini hapa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Marry Kachale amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“ Ni kweli shekidele mkazi wangu Mwanahawa Mkumba anayesoma darasa la tatu Mtawara ameangukiwa na ukuta, muda huu huko hospitali nitafute baadae tuongee zaidi”alisema Mwenyekiti huyo.
Mama mzazi wa Mtoto huyo Gresi Fred Kaloli ameahidi kuzungumza na Mwandishi wa habari hizi atakapotoka wodini, hivyo endeleo kuwa jirani na mtandao huu kupata ’Hapdet’muendelezo ya habari hii ya kusigitisha pia kwa upande wa Mwenyekiti naye sijamalizana naye kuna maswali kadhaa nitamuliza kuhusiana na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment