Neema Muilokozi akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mama yakeDavidi Juma akiweka msalama kwenye kjburi la mama yake.
...Msaafara ukiongozw ana Matarumbeta ulkielekea makaburini nyumbani kwa marehemuMwili wa bibi kete ukitokandani ya kanisa la KKKT Usharika wa Mlalo Msafara umeasili nyumbani kwa marehemu......Msafara umewasili Mkongoroni Mlalo Wilaya ya Lushoto TangaMwandishi wa Mtandao huu aliyekti siti za mbele akicvhukua matukio yote ya barabarani, hapa msafara ukivuka daraja la Wami........Msafara huo ukikatiza mitaa mbali mbali ya jiji la DarMwili ukiigizwa kwenye gari tayari kwa safari la TangaNeema Mulokozi aliyekuwa akimuga mama yakeBirthday yake ya mwisho iliyofanyika Sempemba 27 iliruka gazeti la UwaziBibi Kete akimpa wosia Mjukuu wake Dustan Shekidele kwa Lugha ya KisambaaBibi Kete akimrishs keki Mjukuu wake Dustan Shekidele
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MKE wangu
kipenzi, My Number One. Honey.Kabari yangu, Msiri wangu hayo yote ni majina
mazuri niliyokuita Mpendwa bibi yangu Kete Abdallah ambaye jana umetimiza miaka 5 toka ulipoiaga hii dunia,
Desemba 22- 2019 ukiwa na umri wa miaka 103.
Watoto wako
wapendwa Tumaini Samwel Juma Mrs. Peter Zakaria
Shekidele.ambaye ndiye Mama yangu Mzazi, David Samwel Juma na Neema Samwel Juma
Mrs. Mulokozi wanakukumbuka daima.
Wajukuu,
Vitukuu na Vilembwe zaidi 100 tunakukumbuka Mpendwa bibi yetu tuna kumbuka ulipotimiza
miaka 100 Wajukuu, Vijukuu na Vilembwe kwa pamoja tulikubaliana kila Mwaka
tukufanyie sherehe Kubwa ya kumbukizi ya
siku yako ya kuzaliwa’Happy Birthday’.
Tunashukuru
tulilimiza hilo kwa kukufanyia sherehe nyumbani kwako Moshi Baa Mombasa Gongola
Mboto Jijini Dar es salaam na Birthday yako ya mwisho tuliifanya Septemba
27-2019 ulipotimiza miaka 103.
Mwaka huo
huo Desemba 22 akiwa usingizini majira ya asabuhi alifariki dunia nyumbani
kwake Moshi Baa Dar na maiti kuhifadhiwa
hospital ya Amana.
Kufuatia
kifo hicho Mtoto wa Kiume David Juma’Anko’
anayeishi Marekani aliomba mama yake asizikwe mpaka afike, hivyo mwili huo iliendelea
kusalia Mochwari hadi Desemba 25 alipowasili nchini.
siku hiyo ya X Mas mwili ulitolewa Mochwari na kuwekwa ukumbi wa Hospital ya Amana ikafanyika lbada kisha watu wa Dar walitoa heshima za Mwisho.
Baadae Mwili
uliingizwa kwenye gari na safari ya kuelekea
Kijijini kwake Mlalo Lushoto Tanga kumpunzisha kwenye nyumba yake ya
Milele ilianza kwa msafara wa magari zaidi ya 5.
Desemba 26
lbada ya kumuombea marehemu ilifanyika kanisa la KKKT Usharika wa Mlalo na baadae
msafara ulioongozwa na Matalumbeta ulianza kuelekea kwenye kaburi lilipo nje ya nyumba ya Marehemu
tukampunzisha Mpendwa wetu kwenye nyumba yake hiyo ya Milele.
MJUKUU KUSIMAMISHWA KAZI.
Kufuatia
KIfo hicho Mjukuu wa Bibi huyo alisimamishwa kazi kwa kile kichoelezwa na
Uongozi wa kampuni ya yake ‘utoro kazini’.
Awari baada
ya Mjukuu huyo kutoa taarifa za kifo hicho kwenye uongozi wa kampuni walimpa ruhusa
ya wiki moja sambamba na kutuma
Mwakilishi kuiwakilisha kampuni kwenye msiba huo.
Kutoka na
mazingira ya msiba huo wiki moja aliyopewa mfanyakazi huyo haikutosha hivyo
ilimradhimu kukaa wiki mbili kumaliza msiba huo kufuatia kuchelewa kuzikwa kwa
marehemu na ukubwa wa mziba wenyewe upande wa kifamilia.
Hivyo huyo aliyefanya kazi kwenye kampuni hiyo
kwa miaka 17 baada ya kurejea kazini alikutana na barua ya kusimamiswa kazi.
AlipojalibuLicha kujitetea l utetezi wake haukusaidia chochote,
hadi sasa miaka 5 imepita bado amesimamishwa kazina bila kulipwa chochote,
lfahamike hadi sasa mtumishi huyo hajapewa
barua ya kumfukuza kazi huku akiwa na baadhi ya vifaa vya kampuni hiyo.
Kwa mujibu
wa uongozi wa kampuni hiyo inayojihusisha
na mambo ya habari ulisema kwamba wanatoa
ruhusa ndefu kwa mfanyakazi aliyefiwa na Baba,Mama, Mke\Mume au Mtoto la si kwa
kila ndugu.
Hivyo kila
Desemba 22 Mjukuu huyo jina kapuni ana kumbuka machungu mawili ya kuondokewa na mpendwa bibi
yake sambamba na kutimuliwa kazi kwa
kifo cha bibi yake inauma sana aishee.
Akizungumza
na Mtandao huu Mjuu huyo alisema “kifo cha bibi yangu kinadhamani kubwa kuliko
kazi” alisema kwa uchungu mkubwa.
Alipoulizwa kama amekwenda kulalamika kwenye
taasisi yoyote ya kiserikali Mjuu huyo alijibu.
“Sijalalamika popote hapa chini ya jua nimemshitakia MUNGU,ninachoweza kusema kila
siku ya kumbukizi ya kifo cha bibi yangu Desemba 22 nitalalamika kwenye maeneo
kama haya nikiadhimisha kumbukizi ya kifo cha mpendwa bibi yangu
kilichoambatana na kutimuliwa kazi” alisema na kuongeza .
“Ningekuwa
kwenye kipindi Redioni ningeomba nipigiwe
wimbo wa Muumini Mwijuma ‘Kocha wa dunia wa ’ Kifo cha baba yangu’ambaye
naye yalimkuta kama haya yangu na kuamua kutumia kipaji chake cha uimbaji
kulalamika dhdi ya Muajili wake”.alimalizia kusema Mjuu huyo wa kiume.