Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, December 30, 2024

MASHABIKI WAFURIKA KUSHUHUDIA DERBY KALI YA NDONDO CUP.




Black Peole wakichomoa bao hilo na kumuacha kipa wa Viba Gumbo Mfaume akidaka hewa.

 
Bauns Big Suma kutoka Gym ya Bad Boya Mjini Mpya akiwa makini kulinda usalama kwenye Dabi hiyo
.


Kiungo fundi wa Black Viba akiwatoka mabeki wa Back people na kufumua shuti kali lililopaa juu ya gori


Kweli kutoka kisoka ni bahati jamaa huyu Kiungo fundi wa Mpira Star Mwande ambaye kwenye Dabi hiyo aliitumikia Black People kama kawaida yake juzi alikichafua sana kwenye gemu hiyo



 

 

    Na Dustan Shekidele,Morogoro,

Mashabiki wa Soka Mkoa wa Morogoro juzi walifurika Uwanja wa  CCM Saba saba ‘Shamba la Babu’kushuhudia Derby kali ya Ndondo Cup kati ya timu mahasimu Mkoa hapa, Black People’Taifa la Watu weuzi kutoka Kata ya Mji Mpya na Black Viba ‘Watakatifu Weusi’ kutoka Kata ya Mbuyuni.

Katika Dabi hiyo ya Nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo ya Ndondo, hadi dakika 45 za kwanza zinatamatika,wababe hao walitoka sale ya bao 1-1, Viba wakitangulia kupata bao dakika 36 na People kuchomoa bao hilo dakika ya 44 na kuzima ‘kigoma’ cha mashabiki wa Viba kilichokuwakikitamba uwanjani hapo.

Dakika 45 za pili zilianza kwa timu hizo zilizosheheni vyota wengi wa mkoa Morogoro wanajiandaa kutoka kwenda timu kubwa kushambulianza k wa zamu huku kila timu ikihitaji kuibuka mshindi na kutinga fainali.

Kwa mshangao wawengi dakika 57 gemu hiyo ilivunjika baada ya vulugu kubwa kutokea uwanjani, polisi waingilia kati.

 Kama kawaiwa Mpiga picha wa Mtandao huu alikusanya picha zote za vulugu hizo, hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu  kuona picha hizo na kujua chanzo cha vulugu hizo.

No comments:

Post a Comment

KARUME DAY, MH DIWANI ATOA SADAKA KWA NDEGE NJIWA.

                                    Ramadhan Rajabu                                                      Nassoro Hamoud' Mpemba'    ...