Mwana Birthday Shekidele akitoka nyumbani kuelekea kituo cha watoto yatima cha Mihayo.
Mwana Birthday Shekidele akiendelea kugawa zawadi kwa watoro hao yatima.
.......Akigawa chabarua chenye dawa ya kua Mmbu
Mwana Birthday Shekidele akimkabidhi zawadi ya nguo mtoto Kamila wa kituo hicho cha kulelea watoro yatima cha Mehayo....Akizungumza na ndugu zake hao wanaoishi kwenye kituo hicho
Mkoba wa kike aliokabidhiwa Matroni wa kituo hicho
.
Na Mwandishi Wetu Morogoro.
Mwandishi wa Mtandao huu. Dustan Shekidele. Desemba 25 aliadhimisha kukumbizi yake ya kuzaliwa’Happy Birthday kwa kukata na kula keki na watoto yatima wa Kituo cha Mehayo kilichopo Kata ya Mazimbu Mkoani hapa.
Mara baada ya zoezi hilo lililoongozwa na Matroni wa kituo hicho Bi, Esther Daniel kutamatika, Shekidele alifungusha fuko la zawadi na kuwakazi watoto hao.
Miongoni mwa zawadi hizo ni Nguo na vyandarua’Neti’ pamoja na mkoba wa kisasa aliopewa Matroni huyo kama motisha ya kazi kubwa anayoifanya ya kuwahudumia ndugu zetu hao wenye changamoto mbali mbali.
MAZINGATIO YA ZAWADI.
Wasomani wa Mtandao huu watakumbuka Kwenye Birthaday ya Shekidele iliyofanyika Desemba 25-2023 kituoni hapo, mara baada ya Mwana Birthday huyo kukata keki na kulishana na watoto hao.
Aliuvua uwana Birthday na kuuvaa Uandishi wa habari ambapo alimuliza Matroni Esther changamo zilizopo kituo hapo ili mtu atakaye guswa aweze kusaidia.
Matron alisema.”Kwa niaba ya Mkurugeni wa kituo Mama Linda Sprian Gido tunakushukuru kwa zawadi unazozileta kila siku ya Birthday yako.
Kila Mwaka umefika hapa kituoni na kukata keki na hao watoto ambao wengi wao hawana wazazi hivyo ishu ya kukata na kula keki kwao ilikuwa kama ndoto”alisema Matroni huyo na kuongeza.
Kuhusu changamoto ziko nyingi baadhi ni ukosefu wa Sukari kama unavyojua hapa kituoni kuna watu zaidi ya 50 kwa namba hiyo unapima mwenyewe matumizi ya sukari kwa siku ni kiasi gani tukikosa sukari tunawachemshia uji asubuni.
Changamoto ngingine ni chakula na Madawa, hapa kituoni tuna uhaba wa Net watoto wanalala bila chandarua kwa hali hiyo wanapata maradhi mara kwa mara, hivyo mtu atakayeguswa atusaidie Net kupunguza haya maradhi ya mara kwa mara nayokula pesa nyingi kama unavyojua Mtoto anavyoumwa hospital hawajua kama ni Yatima au Mlemavu wanataka pesa”alisema Matroni huyo.
Alipoulizwa kufuatia hali hiyo anamaombi gani kwa serikali?
Alijibu.
Maombi yangu wasaidie vitu vya watoto yatima Bima ya Afya naamini hiyo inawapunguzia mzigo wamiliki wa vituo hivyo”
Kwa kuzingatia maombi hayo kwenye Birthday ya Mwaka huu Shekidele alibeba Net na kuwakabidhi watoto hao.
Kuhusu ombi la Bima ya Afya kama serikali itasikia maombi hayo Shekidele amesema atajitolea kuisaidia serikali kwa kuwapiga passpot Size watoto wa Vitu vyote vya jimbo la Morogoro Mjini bure hata wakiwa zaidi ya 500.
Akithibitsiha hilo Shekidele alisema”Hasara Roho pesa makaratasi, mimi ni Mpiga picha kazi ya kuwapiga Passpoti Size watoto hao iko ndani ya uwezo wangu.
Kwenye maisha yangu nilichangua kazi ya Mwanasheria[Wakili] kwa lengo la kuwatetea wanyonge, baada ya kushindwa kufikia tamanio langu hilo kwa sababu za kiuchumi, nikageuika kwenye Uwandishi wa habari kwa lengo lile lile la kuwateta na kuwasemea wanyonge na watu wenye uhitaji.
Nikitumia karamu yangu kupaza sauti kwa wasio na sauti .”alisema Shekidele na kuongeza.
“Kwenye Birthday ya Mwaka huu nimewaahdi wale watoto kwamba Mwenyezi Mungu akinipa zawadi ya Uhai na kuniongeza Mwaka Mwingine basi Birthday ya Mwakani Desemba 25-2025 nitamkodi mpishi Maarufu wa Pilau Mkoa wa Morogoro apige Pilau kituoni hapo.
Wakiona kimya wajue waliompenda Mungu amempenda zaidi” Shekidele aliwambia watoto hao kama anavyoonekana pichani.
No comments:
Post a Comment