Na Mwandishi wetu Morogoro.
DESEMBE 25 ni siku kuu ya Krismasi, siku ya kuadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa Yesu Kristo yapata miaka 2000 iliyopita.
Taarifa za kuzaliwa kwake tena kwenye zizi la Ng’ombe Mjini Bethlehemu ziliposambaa kwamba Mfalme wa Wayahudi kazaliwa, Mfalme Herode kusikia hivyo, katoa agizo la kusakwa na kuuwawa watoto wote wa kiume wenye umri chini ya miaka 2. Imeandikwa Mathayo 2 mstari 16.
Mungu ni Mwema licha ya msako huo Yesu aliponyeka na kuendeleza ufalme wake na kumuacha Mfalme Herode akiduwaa kwa amri yake hiyo ya kuuwa watoto wasio na hatia kugonga Mwamba.
Yesu aliendelea kuwindwa hatimaye alipofika umri wa miaka 33 alikamatwa akapigwa mijeledi, akavishwa taji la miba kisha akitundikwa Msalabani akapigiliwa misumari alipokaribia kukata roho Yesu alisema maneno haya ya kiyahudi ‘Heroi Heoi lama wa mabirai’ Maana yake Mungu wangu Mungu wangu Mbona umeniacha?.
Baada ya kusema maneno hayo Yesu akainamisha shingo msalabani na kukata roho. Ukuu wa Mungu umetimia hakumuacha Mwanae, Yesu baada ya kuzikwa siku ya tatu alifufuka na kuwaacha watu midomo wazi wakishuhudia jiwe kubwa liliweka kwenye kaburi lake likiondolewa na Mwamba Yesu kafufuka.sote tusema Haleluya Mwana wa Mungu yu hai.
Leo Desemba 25-2024 tunaadhimisha Siku kuu ya Krismasi tukikumbuka kifo cha Mpendwa wetu Yesu Kristo aliyetoa sadaka maisha yake ili mimi na wewe tupone.
Siku kama ya Leo mikaa kadhaa iliyopita Familia ya Peter Zakaria Shekidele na mkewe Tumaini Samwel Juma walijaliwa kupata Mtoto wa Kiume waliyembatiza jina la Dustan Peter Shekidele akiwa ni mtoto wao wa 5 kwenye familia hiyo iliyofunga kizazi na watoto 7.
Hii Leo Desemba 25 Dustan anaunga na wakristo wote kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa na Mokozi Yesu Kristo.
Akizungumza na Mtandao huu Dustan alisema. “Awari ya yote najisikia fahari kubwa kuzaliwa siku moja na Mwokozi Yesu, kwa mantini hiyo sote tuliozaliwa siku moja na Yesu[Nabii lssa] tunapaswa kuishi maisha ya kitakatifu kama alivyoishi Yesu ili tunavyoadhimisha siku hii matendo yetu yakisi mema mengi aliyofanya Mwana Birthday mwenztu Yesu”alisema na kuongeza.
Kufuatia hali hiyo kama kawaida Leo jioni nitaadhimisha siku yangu ya kuzaliwa kwa kutembelea kituo cha watoto Yatima cha Mihaya kilichopo kata ya Mazingu Mkoani hapa.
Nikiwa huko nitakata keki na ndugu zangu hao kisha nitawapa zawazi kadhaa nilizojaliwa na Mwenyezi Mungu, baada ya kufanya hivyo Sherehe yangu itaishia hapo.
Inashangaza Mungu kakupa zawazi ya kukuongezea Mwaka, baada ya kumshukuru kwa kutenda mema ili mwakani akuongeze mwaka Mwingine, unashuhudia mtu anakodi ukumbu na kuwanywesha watu bia baadae watu hao wake kwa waume wakishalewa baadhi yao wanasalitia ndoa zao na wasio na ndoa wanaansisha mahusiano mapya kupitia siku yako hiyo ya kuzaliwa, kwangu mimi hilo sio sawa mwenye masiki na asikie nasiye na msikio[….]”alimalizia kusema Shekidele.
No comments:
Post a Comment