Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, December 23, 2024

DESEMBE 22 MY WANGU UMETIMIZA MIAKA 5 TOKA UIAGE DUNIA.

 


Neema Muilokozi akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mama yake
Davidi Juma akiweka msalama kwenye kjburi la mama yake

....Msaafara ukiongozw ana Matarumbeta ulkielekea makaburini nyumbani kwa marehemu
Mwili wa bibi kete ukitokandani ya kanisa la KKKT Usharika wa Mlalo
                  Msafara umeasili nyumbani kwa marehemu
......Msafara umewasili Mkongoroni Mlalo Wilaya ya Lushoto Tanga
Mwandishi wa Mtandao huu aliyekti siti za mbele akicvhukua matukio yote ya barabarani, hapa msafara ukivuka daraja la Wami.
.......Msafara huo ukikatiza mitaa mbali mbali ya jiji la Dar
Mwili ukiigizwa kwenye gari tayari kwa safari la Tanga
Neema Mulokozi aliyekuwa akimuga mama  yake

Birthday yake ya mwisho iliyofanyika Sempemba 27 iliruka gazeti la Uwazi

Bibi Kete akimpa wosia Mjukuu wake Dustan Shekidele kwa Lugha ya Kisambaa



Bibi Kete akimrishs keki Mjukuu wake Dustan Shekidele

 

       Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MKE wangu kipenzi, My Number One. Honey.Kabari yangu, Msiri wangu hayo yote ni majina mazuri niliyokuita Mpendwa bibi yangu Kete Abdallah ambaye jana  umetimiza miaka 5 toka ulipoiaga hii dunia, Desemba 22- 2019 ukiwa na umri wa miaka 103.

Watoto wako wapendwa Tumaini Samwel Juma Mrs.  Peter Zakaria Shekidele.ambaye ndiye Mama yangu Mzazi, David Samwel Juma na Neema Samwel Juma Mrs. Mulokozi wanakukumbuka daima.

Wajukuu, Vitukuu na Vilembwe zaidi 100 tunakukumbuka  Mpendwa bibi yetu tuna kumbuka ulipotimiza miaka 100 Wajukuu, Vijukuu na Vilembwe kwa pamoja tulikubaliana kila Mwaka tukufanyie sherehe Kubwa ya kumbukizi  ya siku yako ya kuzaliwa’Happy Birthday’.

Tunashukuru tulilimiza hilo kwa kukufanyia sherehe nyumbani kwako Moshi Baa Mombasa Gongola Mboto Jijini Dar es salaam na Birthday yako ya mwisho tuliifanya Septemba 27-2019 ulipotimiza miaka 103.

Mwaka huo huo Desemba 22 akiwa usingizini majira ya asabuhi alifariki dunia nyumbani kwake Moshi Baa Dar na maiti  kuhifadhiwa hospital ya Amana.

Kufuatia kifo hicho Mtoto  wa Kiume David Juma’Anko’ anayeishi Marekani aliomba mama yake asizikwe  mpaka afike, hivyo mwili huo iliendelea kusalia Mochwari hadi Desemba 25 alipowasili nchini.

 siku hiyo ya X Mas mwili  ulitolewa Mochwari na kuwekwa  ukumbi wa Hospital ya Amana ikafanyika lbada  kisha watu wa Dar walitoa heshima za Mwisho.

Baadae Mwili uliingizwa kwenye gari na safari ya kuelekea  Kijijini kwake Mlalo Lushoto Tanga kumpunzisha kwenye nyumba yake ya Milele ilianza kwa msafara wa magari zaidi ya 5.

Desemba 26 lbada ya kumuombea marehemu ilifanyika kanisa la KKKT Usharika wa Mlalo na baadae msafara ulioongozwa na Matalumbeta ulianza kuelekea kwenye kaburi  lilipo nje ya nyumba ya Marehemu tukampunzisha Mpendwa wetu kwenye nyumba yake hiyo ya Milele.

    MJUKUU KUSIMAMISHWA KAZI.

Kufuatia KIfo hicho Mjukuu wa Bibi huyo  alisimamishwa kazi kwa kile kichoelezwa na Uongozi wa kampuni ya yake ‘utoro kazini’.

Awari baada ya Mjukuu huyo kutoa taarifa za kifo hicho kwenye uongozi wa kampuni walimpa ruhusa ya wiki moja  sambamba na kutuma Mwakilishi kuiwakilisha kampuni kwenye msiba huo.

Kutoka na mazingira ya msiba huo wiki moja aliyopewa mfanyakazi huyo haikutosha hivyo ilimradhimu kukaa wiki mbili kumaliza msiba huo kufuatia kuchelewa kuzikwa kwa marehemu na ukubwa wa mziba wenyewe upande wa kifamilia.

 Hivyo huyo aliyefanya kazi kwenye kampuni hiyo kwa miaka 17 baada ya kurejea kazini alikutana na barua ya kusimamiswa kazi.

AlipojalibuLicha  kujitetea l utetezi wake haukusaidia chochote, hadi sasa miaka 5 imepita bado amesimamishwa kazina bila kulipwa chochote,

 lfahamike hadi sasa mtumishi huyo hajapewa barua ya kumfukuza kazi huku akiwa na baadhi ya vifaa vya kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa uongozi  wa kampuni hiyo inayojihusisha  na mambo ya habari ulisema kwamba wanatoa ruhusa ndefu kwa mfanyakazi aliyefiwa na Baba,Mama, Mke\Mume au Mtoto la si kwa kila ndugu.

Hivyo kila Desemba 22 Mjukuu huyo jina kapuni ana kumbuka  machungu mawili ya kuondokewa na mpendwa bibi yake sambamba na kutimuliwa kazi kwa  kifo cha bibi yake inauma sana aishee.

Akizungumza na Mtandao huu Mjuu huyo alisema “kifo cha bibi yangu kinadhamani kubwa kuliko kazi” alisema kwa uchungu mkubwa.

 Alipoulizwa kama amekwenda kulalamika kwenye taasisi yoyote ya kiserikali Mjuu huyo alijibu.

 “Sijalalamika popote hapa chini ya jua  nimemshitakia MUNGU,ninachoweza kusema kila siku ya kumbukizi ya kifo cha bibi yangu Desemba 22 nitalalamika kwenye maeneo kama haya nikiadhimisha kumbukizi ya kifo cha mpendwa bibi yangu kilichoambatana na kutimuliwa kazi” alisema na kuongeza .

“Ningekuwa kwenye kipindi Redioni ningeomba nipigiwe  wimbo wa Muumini Mwijuma ‘Kocha wa dunia wa ’ Kifo cha baba yangu’ambaye naye yalimkuta kama haya yangu na kuamua kutumia kipaji chake cha uimbaji kulalamika dhdi ya Muajili wake”.alimalizia kusema Mjuu huyo wa kiume.

 

 

No comments:

Post a Comment

KARUME DAY, MH DIWANI ATOA SADAKA KWA NDEGE NJIWA.

                                    Ramadhan Rajabu                                                      Nassoro Hamoud' Mpemba'    ...