Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, November 28, 2024

WANANCHI WAELEZA SABABU TANESCO KUSUASUA KUBADILISHA NGUZO.





 


     Na Dustan Shekidele,Morogoro.

IMEFICHUKA.

Wananchi Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa, wamefichua siri ya Tanesco  kusuasua kubadili nguzo  iliyooza na kusababisha Nyaya za umeme kushuka chini eneo la barabara.

Akizungumza na Mtandao huu mmoja wawananchi wa Mtaa huo aliyeomba hifadhi ya Jina lake alimng’ata sikio Mwandishi wa habari hizi akimueleza haya.

“ Tunashukuru kwa juhuzi zako zilizopelekea Tanesco kuja fasta kubadili nguzo, awari sisi wananchi tukiongozwa na Baba Mwingi tulitoa taarifa Tanesco zaidi ya mara 3  wanakuja  wanaangali hii nguzo na nyaya zilivyolege  wanajadiliana huku wakipiga simu kasha wanaondoka zao bila kufanya chochote.

Tulipowauliza walisema eneo ilipo  nguzo muda wowote TARURA watajenga daraja na kuweka Lami barabara hii wanasubiri kazi hiyo ya ujezi wa barabra ianze waje kuhamisha nguzo.

Cha kushangaza tulivyokueleza wewe na kutoa kwenye Mtandao wako Tanesco wamebadili nguzo na kuiweka hapo hapo eneo la barabara.”alisema Mwananchi huyo.

Kufuatia hali hiyo Mtandao huu ulimuliza mmoja wa mafundi  aliyekuwa site akibadili nguzo hiyo alisema.

“ Ni kweli nguzo ipo eneo la barabara kama unavyoiona, ujezi wa barabara utakapoanza wenzetu wa TARURA watatuita na kutuonyesha eneo la kuihamisha  hivyo kwa sasa tunatibu tatizo hili la kubadilisha nguzo”alisema mtumishi huyo wa Tanesco.

Ili kujua ukweli wa taarifa hizo Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Kassimu Ramadhani Lukinga Maarufu Mzee Kiuno alioulizwa alisema.

“ Ni kweli barabara hii inakarabatiwa kwa kiwango cha Lami kutoka Sido jirani na Kanisa la KKKT Usharika wa Mji Mpya inakwenda kuungana na barabara ya Lami ya  Kichangani.

Kama unavyoona hapa kwenye hiki kidaraja kidogo kulikuwa na vibanda vya wamachinga mwezi uliopita vimevunjwa kupisha ujenzi wa barabara hii,.

Kwa kuanza litajengwa daraja kubwa la kupita magari eneo hili la Mto Morogoro na unavyoniona na kwenda pale kwa Mziray kuomba eneo ambalo Mkandarasi wa daraja  ataweka vifaa vyake, mambo yakienda vizuri Jumatatu kazi ya ujenzi wa daraja unaanza”alisema Mwenyekiti huyo.

Uchunguzi uliofanywa na Mtandao huu umebaini ukarabati wa barabara hiyo unalenga kupunguza foleni katikati ya Mji.

Kwamba kwa magari yanayotokea Msamvu kuelekea Gereza kuu la Manispaa, Kikosi cha kuliza ghasi cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro‘FFU. Stesheni kuu ya Treni.na Hosital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro watakatiza kwenye barabara hiyo.

  Barabara hiyo inayokatiza Maghorofa ya Reli, Shule ya Msingi Kaloleni na uwanja wa Mazoezi wa timu ya Reli ya Morogoro inatoboa hadi maeneo ya Kichangani, Kilakala, Makabuli ya Kolla, Kigurunyembe na Bingwa.  

Ujio wa barabara hii itakuwa faraja kwa wananchi wanaoishi ng’ambo ya Mto Morogoro hasa wafanyakazi wa shirika la Reli wanaoishi  kota na Maghorofa ya Reli, wanafunzi wa shule ya Kaloleni na Wazee wanaolelewa kwenye kambi ya Funga funga.

Makundi yote hayo ni kama walikuwa kwenye kisiwa cha peke yao,kwani gari kubwa hazina uwezo wa kufika eneo hilo hivyo kama ingetokea janga la Moto gari za Jeshi la Zima Moto na Uokoaji zisinge kuwa na uwezo wa kufika eneo hilo.

Wednesday, November 27, 2024

MENEJA TANESCO ASIKIA KILIO CHA WANANCHI.

Lori la Tanesco likiwani huku likiwa na lundo la mafundi
              Lori la pili likiwanini na nguzo mbili za kisasa
........Mafunsdi wakiendelea kufunga waya kwernye nguzo mpya
......Mmoja wawanachi wa Mtaa huo akiangalia nguzo ya Umeme iliyotolewa ikioneka kuoza sehemu ya chini
          Waya hizo za Umeme kwa sasa zikiwa juu ya barabara
 

 

     Na Dustan Shekidele Morogoro.

MENEJA wa Shirika la Umeme Tanazania’Tanesco Mkoa wa Morogoro’ Fadhiri Chilombe amesikia kilio cha wananchi wa Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya Mkoani Morogoro waliokuwa na kero ya Nyaya za Umeme kuning’inia barabara jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.

Stori hii iliruka jana na kuahidi kuendelea leo kwa Mwandishi wa Mtandao huu kutinga eneo la tukio kufuatilia kama kweli Tanesco wamerekebisha tatizo hilo kama alivyoahidi Meneja huyo.

Hiyo Jumatuta asubuhi na Mapema Mwanahabari huyo alitinga eneo hilo na kushuhudia Malori Mawili ya Tanesco yakitinga eneo hilo Lori moja lilibeba lundo la wafanyakazi wa shirikani hilo huku lingine likiwasili na Nguzo mbili za kisasa za zege.

Baada ya Muda umeme ulikatwa mtaa huo na zoezi la kubadilisha nguzo hizo ulianza na kazi hiyo haikuwa nyepesi siku hiyo ya Jumatatu hawakufanikiwa kuikamilisha.

Mafundio hao walirejea  jana Jumanne na Mwandishi wa Mtandao huu naye alirejea tena jana kufuatilia kazi hiyo aliyotumwa na wananchi.

Hatimaye majira ya saa 9 Alasiri mafundi hao walikamilisha kazi hiyo kwa Weledi Mkubwa,baada ya kazi hiyo kukamilika  kundi la wananchi  wake kwa waume walimzingira mwandishi wa Mtandao huu na kumpongeza kwa kufanikisha kero yao kutatuliwa.

Kwa upande wake Mwandishi huo alimshukuru Meneja wa Tanesco kwa kuwa msikivu wa kutatua kwa haraka kero za wananchi.

 Katika hatua nyingine Wakati Mwandishi wa habari hizi anajiandakuondoka eneo hilo Mwananchi mmoja alimfuata na kumueleza ugumu uliopelekea Tanesco kubadili nguzo nguzo hizo eneo hilo.

Habari hiyo mpya ya kushangaza itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

Tuesday, November 26, 2024

HABARI KALI YA KITAA. NYAYA ZA UMEME ZAZUA TAHARUKI MTAA WA MAKABURI ‘A



 ’

                              Na Dustan Shekidele,Morogoro.
KAMA kawaida Leo Jumanne Mtandao Pendwa wa Shekidele unaendelea na kipengele cha habari kali ya kitaa ambapo kila uchao kipengele hichi kinaendelea kujizolea umaarufu kwa habari kili za kitaa.
 
Katika kuthibitisha hilo wiki iliyopita wananchi wa Mtaa wa Makaburi ‘A’Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa, walimtafuta Mwandishi wa Mtandao huu na kumuomba atinge mtaani kwao na fagio lake la Mtaa afagie kero yao.
 
Mtumishi huyo wa wananchi alitii wito huo na juzi Jumapili alifika na kushuhudi Nyaya za Umeme kulegea na kushuka jirani ya barabara jambo ambalo ni hatari kwa watumiaji wa barabara hiyo hasa nyakati za usiku.
 
Wakizungumza na Mtandao huu wazee wawili wa mtaa huo Ngwangwai Kasembi’Maarufu Baba yoyoo’na Mzee Mohamed Maarufu Baba Mwinyi’anayemiliki nyumba 3 kwa mpigo zinazoonekali kulia jirani na Nyaya hizo walisema.
 
“Angali hii hatari nyaya hizi za Umeme zimeshuka chini katikati ya barabara hii kubwa ambayo inatumiwa na watu wengi wanaoelekea hospital ya Mkoa wa Morogoro na stesheni kuu ta Treni”alisema Baba Yoyoo huku akionyesha Waya hizo.
Kwa upande wake Baba Mwingi ambaye moja ya nyumba zake hizo kuna mashine za kukoboa na kusaga nafaka alisema.
“Tumekuita wewe Mwandishi Shekidele labda kupitia wewe kero hii ya hatari itaondoka mtaani kwake, mimi nimetoa taarifa Makao makuu ya Tanesco Dodoma mara 3 nikapewa namba za taarifa lakini chaajabu zaidi ya wiki moja sasa hakuna hatua yoyote iliyochukulia” alisema Mzee huyo na kuongeza.
Huu utaratibu wa kutoa taarifa makao Makuu nahisi ndio changamoto kwani muhudumu huyu anapokea taarifa za nchini nzima hivyo utekelezaji wake unakuwa kama huu wa kusua sua”alimazima kusema mzee huyo huku akionekana kuwa na jazba.
Kufuatia malalamiko hayo Mwandishi wa habari hizi siku hiyo hiyo ya Jumapili alimtwangia simu Meneja wa Tenesco Mkoa wa Morogoro Fadhiri Chilombe alipoelezwa kero hiyo na hatua walichochukua wananchi hao ambazo zimeferi, Big Bosi huyo Tanesco Mkoa wa Morogoro alisema.
“Binafsi sina taarifa za tukio hilo hivyo ndugu Mwandishi naomba nielekeze eneo hilo kesho niwatuma mafundi wakalekebishe tatizo hilo”
Mwandishi alimuelekeza na kumueleza kwamba hiyo kesho naye atafuatilia mafundi kuona kama tatizo hilo limetatuliwa kwa usalama wa wananchi wanaotumia barabara hiyo.
Kesho Mtandao huu utatoa mrejesho wa habari hii kama mafundi hao wamefika mtaani hapo au la, hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

Thursday, November 21, 2024

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga


      Na Dustan Shekidele,Morogoro.

AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’Security Guard’ Mkoani Morogoro Ally Chinga amenusurika kifo baada ya kujipiga Risasi  wakati akijiandaa kukabiliana na Mwizi aliyevamia lindo lake usiku mnene.

Taarifa za tukio hilo zinadai wakati wa pulukushani hiyo Afande huyu amejikuta akijipiga risasa  kwenye mkono wa kushoto wakati akihangaika kuvua bunduki aliyoivaa kwenye bega la kushoto.

Kufuatia taarifa hizo za kusigitisha Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Afande huyo kwa lengo la kupata simulizi kamili ya mkasa huo.

“Siku ya tukio  nikiwa nimejificha kwenye eneo la giza kama kanuni zetu za ulinzi zinavyotuelekeza,huku nilikuwa na Mbwa anayenisaidia kwenye ulinzi.

Siunajua hatuluhusiwi kulala  kwenye lindo hivyo katika hali ya kupoteza usingizi niliamua kucheza gemu kwenye simu.

Majira ya saa 8 usiku Mbwa alinusa harufu akastuka bila kupiga kelele kwa sababu alikuwa na mafunzo ya Ulinzi nilipoinua macho nikamuona mwizi anataka kuluka ukuta aingie ndani.

 Kama unavyojua hiyo ni kama vita hujuia anasilaha gani huyo mwizi hivyo nikashusha bunduki kwenye bega ghafla mbwa aliyekuwa amelala chini alinyanyuka fasta amfuate mwizi ile ananyanyuka kagusa kitako cha bunduki ikanyanyuka kuja kwenye kifundo cha mkono wangu nikagusa sehemu ya kushuti bunduki ikafyatuka na kunijeruhi  kwenye mkono”alisema Afande huyo na kuongeza.

Hata hivyo namshukuru  Mungu bila kujeruhi mkono huenda Risasi zingepiga kichwani na kufumua ubongo wangu. Wakati hayo yakiendelea Mwizi huyo aliyekuwa na wenzie walikimbia na mimi kuomba msaada kwa majirani walifika na kunimbiza hospital”alimalizia kusimulia Afande huyo.

Baada ya maelezo hayo Mwandishi wa habari hizi alipata uwanja mpana  wa kuliza maswali.

Mwandishi. Kwa mtazamo naona hali yako  kiuchumia sio nzuri swali langu umeumia ukiwa kazini je kampuni  inakusaidia kwa kiwago gani kwenye tatizo hili?

Afande Ally. Naishukuru sana kampuni yangu imenisaidia kwenye matibabu zaidia ya lakini 7 wamelipa kama unavyoona hivi vyuma vya nje ya mkono ‘Antena’ imegharamia kampuni yangu sitaki kuwa mnafiki kwenye hili wamenisaidia kwa sehemu yao.

Mwandishi je kwa sasa unachangamoto gani kuhusiana na jereha hili?

Afande Ally. Changamoto ni nyingi kila siku natakiwa kikasafishe kidonda na kufunga bendeji Mpya gharama yake kila siku ni elfu 7 bila kusafisha kidonda mkono unaweza kuoza na kupelekea kukatwa hivyo kila siku zaidi ya mwezi sasa nalipa elfu 7 kunusuri mkono wangu usikatwe.

Nimeuza hadi simu yangu kukabiliana na gharama hizi lakini bado kwa sasa japo sijazoea nalazima kwenda mjini kuomba msaada kwenye maduka ijumaa na jumapili nakwenda kwenye nyumba za ibada kuomba msaada.

Mwandishi. Ulipowauliza madaktari hali hii ya kufunga kidonda itachukua muda gani?

Afande Ally. Wamesema inategemea maendelea ya kidonda lakini inaweza kuchukua mwezi na zaidi hivyo naomba wasamalia wema watakaoguswa changamoto yangu wanisaidie hiyo elfu 7 ni nje ya nauli ya kutoka nyumbani kila siku kwenda hospital ya Mkoa.

Mwandishi. Sawa toa namba ya simu kwa mtu atakaye guswa akuchangie chochote kitu.

Afande Ally. Simu sina kama nilivyokueleza nimeunza kukabiliana na matatizo haya.

Mwandishi. Huna namba ya mtu nayemuamia mfano mke wako au mwanao?

Afande Ally. Kweli mke wangu anasimu lakini namba yake sijaishika kichwani tukionana tena nitakupa.

Mwandishi ok sawa pole sana kwa changamoto hii haya ni mapito nakuombea kwa Mungu akivushe salama ili urejee kwenye hali yako ya kawaida.

Afande Ally Asante sana na wewe ubarikiwe kwa sapoti yako ya kuripoti changamoto zangu kwenye vyombo vya habari.

 

Alipotakiwa kueleza tukio hilo Afande Ally a

 


 

Tuesday, November 19, 2024

HABARI KALI YA KITAA. WAPANGAJI WAMUWEKA KITI MOTO MWENYE NYUMBA KISA LUKU.


 Kamwenye Jembe halimtupi mkulima, Mwandishi wa Mtandao huu akivuna mkungu wa ndizi


                      Na Dunstan Shekidele Morogoro.
Kama kawaida Kila Jumatatu Mtandao Pendwa wa Shekidele unarusha habari kali ya wiki.
 
Kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wetu jana Jumatatu hatukuweza kurusha habari hiyo na Mbadala wake inaruka leo Jumanne, hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea kwa wasomaji wetu.
 
Baada ya ufafanuzi huo tuingie kwenye habari hiyo kali iliyosakwa wiki iliyopita, ambapo wapangaji Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro wameitisha kikao na kumuweka kiti Moto baba Mwenyenyumba wao wakipinga kumlipia kodi ya jengo la nyumba yake kupitia michango ya Luku ya Umeme wanachanga.
Baada ya Mwandishi wa habari hizi kurambishwa ubuyu huyo na wambea wa Mtaa ,alimtafuta baba Mwenyenyumba huyo ili kusikia kauli yake. 
 
Baba mjengo huyo aliyeomba hifadhi ya Jina lake alithibitisha kuwekwa kiti Moto na wapangaji wake na mahojiano yetu yalikuwa hivi.
 
Mwandishi. Mzee mshikamoo.
 
Baba Mjengo. Marahaba karibu sana.
Mwandishi. Asante Mimi ni Mwanahabari nasiki hivi karibuni
wapangaji wako walikuweka kiti moto Agenda ya kikao hicho ilikuwa ni ipi?
 
Baba Mjengo. Yaani ni Mambo ya ajabu sana mimi na nyumba yangu wapangaji wananinyanyasa jambo ambalo sikubaliani nalo.
Nyumba hii inavyumba 15 kila mwezi tunatumia umeme wa elfu 15 hivyo kila mpangaji kwa mwezi analipa elfu moja ya Umeme.
Agenda ya kikao hichowanadai kila mwezi wananilipia Kodi ya jengo kupitia Luku hivyo wamehitaji walipe mia 9 hiyo mia nilipe mimi kama kodi ya jengo langu wao hiyo kodi ya jengo wanadai haiwahusu.
 
Mwandishi. Kwa hiyo umekubari kufanya hivyo?
 
Baba Mjengo sijakubari baada ya kikao wote nimewafukuza kwenye nyumba yangu, Mgosi watu hawana shukrani.
Mimi ninanyumba Tatu hii hapa Morogoro na mbili ziko nyumbani Tanga nyumba zote 3 kila moja inavyumba 15
 
Miaka yote ikifika mwenye Mtukufu wa Ramadhan mwezi huo wapangaji wangu wote hawalipi kodi wanakaa bure kama sadaka yangu ya mwenye mtukufu wa Ramadhan.
 
Leo hawa wapangaji wa Morogoro wananiweka kiti moto kwa shilingi mia moja malalamiko hayo wangeya peleka Tanesco walioweka kodi ya Jengo kwenye Luku. 
 
Mwandishi. Je umeshapata wapangaji wengine na kama umepata Elimu gani juu ya shwala hilo la Luku ili usije kuwekwa tena kiti moto ?
 
Baba Mjengo nimepata baadhi ya wapangaji vyumba vingine havijapata wapangaji, kila mtangaji anayeingia namueleza swala hilo nashukuru wote walioingia wanajitambua baadhi wamesema nyumba walizotoka kwa mwezi walikuwa wakilipa umeme mpaka elfu 5 kuwambia hapa kwangu umeme kwa mwezi elfu moja wameshangaa sana nashukuru wapangaji wangu hawana vifaa vinavyo kula umeme mwingi.
 
Mwandishi Asante kwa ushirikiano yako.
 
Baba Mjengo. Ok asante na wewe kwa kuja ila ombi langu ndugu Mwandishi kata yetu hii ya Tungi tuna kero kubwa ya Maji hebu tusaidie kupaza sauti kwa viongozi.
 
Mwandishi. Sawa nitafanya hivyo.

Friday, November 15, 2024

MBWA ASABABISHA AFANDE AJILIPUE RISASI


 

INASIGITISHA SANA

 Mbwa asababisha Afande ajilipue na Risasi Mkononi.

 Askari huyo anayetepembea na vyuma mkononi kasimulia A-Z alivyonusurika na kifo.

 Habari hiyo  itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao pendwa wa shekidele  upate habari Moto Moto za chini ya Kapeti.

UJUMBE WA NANE LA MUNGU USALAMA WA WATU WAMUNGU.

Mwandishi wa Mtandao huu akiwa kwenye msitu Mnene Matombo Wilaya ya Morogoro Vijiji ........Mwandishi huyo akiwa Juu ya Milima ya Mgeta wila...