Lori la pili likiwanini na nguzo mbili za kisasa
........Mafunsdi wakiendelea kufunga waya kwernye nguzo mpya
......Mmoja wawanachi wa Mtaa huo akiangalia nguzo ya Umeme iliyotolewa ikioneka kuoza sehemu ya chini
Waya hizo za Umeme kwa sasa zikiwa juu ya barabara
Na Dustan Shekidele Morogoro.
MENEJA wa Shirika la Umeme Tanazania’Tanesco Mkoa wa Morogoro’ Fadhiri Chilombe amesikia kilio cha wananchi wa Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya Mkoani Morogoro waliokuwa na kero ya Nyaya za Umeme kuning’inia barabara jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.
Stori hii iliruka jana na kuahidi kuendelea leo kwa Mwandishi wa Mtandao huu kutinga eneo la tukio kufuatilia kama kweli Tanesco wamerekebisha tatizo hilo kama alivyoahidi Meneja huyo.
Hiyo Jumatuta asubuhi na Mapema Mwanahabari huyo alitinga eneo hilo na kushuhudia Malori Mawili ya Tanesco yakitinga eneo hilo Lori moja lilibeba lundo la wafanyakazi wa shirikani hilo huku lingine likiwasili na Nguzo mbili za kisasa za zege.
Baada ya Muda umeme ulikatwa mtaa huo na zoezi la kubadilisha nguzo hizo ulianza na kazi hiyo haikuwa nyepesi siku hiyo ya Jumatatu hawakufanikiwa kuikamilisha.
Mafundio hao walirejea jana Jumanne na Mwandishi wa Mtandao huu naye alirejea tena jana kufuatilia kazi hiyo aliyotumwa na wananchi.
Hatimaye majira ya saa 9 Alasiri mafundi hao walikamilisha kazi hiyo kwa Weledi Mkubwa,baada ya kazi hiyo kukamilika kundi la wananchi wake kwa waume walimzingira mwandishi wa Mtandao huu na kumpongeza kwa kufanikisha kero yao kutatuliwa.
Kwa upande wake Mwandishi huo alimshukuru Meneja wa Tanesco kwa kuwa msikivu wa kutatua kwa haraka kero za wananchi.
Katika hatua nyingine Wakati Mwandishi wa habari hizi anajiandakuondoka eneo hilo Mwananchi mmoja alimfuata na kumueleza ugumu uliopelekea Tanesco kubadili nguzo nguzo hizo eneo hilo.
Habari hiyo mpya ya kushangaza itaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment