Na Dustan Shekidele,Morogoro.
IMEFICHUKA.
Wananchi Mtaa wa Makaburi ‘A’ Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa, wamefichua siri ya Tanesco kusuasua kubadili nguzo iliyooza na kusababisha Nyaya za umeme kushuka chini eneo la barabara.
Akizungumza na Mtandao huu mmoja wawananchi wa Mtaa huo aliyeomba hifadhi ya Jina lake alimng’ata sikio Mwandishi wa habari hizi akimueleza haya.
“ Tunashukuru kwa juhuzi zako zilizopelekea Tanesco kuja fasta kubadili nguzo, awari sisi wananchi tukiongozwa na Baba Mwingi tulitoa taarifa Tanesco zaidi ya mara 3 wanakuja wanaangali hii nguzo na nyaya zilivyolege wanajadiliana huku wakipiga simu kasha wanaondoka zao bila kufanya chochote.
Tulipowauliza walisema eneo ilipo nguzo muda wowote TARURA watajenga daraja na kuweka Lami barabara hii wanasubiri kazi hiyo ya ujezi wa barabra ianze waje kuhamisha nguzo.
Cha kushangaza tulivyokueleza wewe na kutoa kwenye Mtandao wako Tanesco wamebadili nguzo na kuiweka hapo hapo eneo la barabara.”alisema Mwananchi huyo.
Kufuatia hali hiyo Mtandao huu ulimuliza mmoja wa mafundi aliyekuwa site akibadili nguzo hiyo alisema.
“ Ni kweli nguzo ipo eneo la barabara kama unavyoiona, ujezi wa barabara utakapoanza wenzetu wa TARURA watatuita na kutuonyesha eneo la kuihamisha hivyo kwa sasa tunatibu tatizo hili la kubadilisha nguzo”alisema mtumishi huyo wa Tanesco.
Ili kujua ukweli wa taarifa hizo Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Kassimu Ramadhani Lukinga Maarufu Mzee Kiuno alioulizwa alisema.
“ Ni kweli barabara hii inakarabatiwa kwa kiwango cha Lami kutoka Sido jirani na Kanisa la KKKT Usharika wa Mji Mpya inakwenda kuungana na barabara ya Lami ya Kichangani.
Kama unavyoona hapa kwenye hiki kidaraja kidogo kulikuwa na vibanda vya wamachinga mwezi uliopita vimevunjwa kupisha ujenzi wa barabara hii,.
Kwa kuanza litajengwa daraja kubwa la kupita magari eneo hili la Mto Morogoro na unavyoniona na kwenda pale kwa Mziray kuomba eneo ambalo Mkandarasi wa daraja ataweka vifaa vyake, mambo yakienda vizuri Jumatatu kazi ya ujenzi wa daraja unaanza”alisema Mwenyekiti huyo.
Uchunguzi uliofanywa na Mtandao huu umebaini ukarabati wa barabara hiyo unalenga kupunguza foleni katikati ya Mji.
Kwamba kwa magari yanayotokea Msamvu kuelekea Gereza kuu la Manispaa, Kikosi cha kuliza ghasi cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro‘FFU. Stesheni kuu ya Treni.na Hosital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro watakatiza kwenye barabara hiyo.
Barabara hiyo inayokatiza Maghorofa ya Reli, Shule ya Msingi Kaloleni na uwanja wa Mazoezi wa timu ya Reli ya Morogoro inatoboa hadi maeneo ya Kichangani, Kilakala, Makabuli ya Kolla, Kigurunyembe na Bingwa.
Ujio wa barabara hii itakuwa faraja kwa wananchi wanaoishi ng’ambo ya Mto Morogoro hasa wafanyakazi wa shirika la Reli wanaoishi kota na Maghorofa ya Reli, wanafunzi wa shule ya Kaloleni na Wazee wanaolelewa kwenye kambi ya Funga funga.
Makundi yote hayo ni kama walikuwa kwenye kisiwa cha peke yao,kwani gari kubwa hazina uwezo wa kufika eneo hilo hivyo kama ingetokea janga la Moto gari za Jeshi la Zima Moto na Uokoaji zisinge kuwa na uwezo wa kufika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment