Kamwenye Jembe halimtupi mkulima, Mwandishi wa Mtandao huu akivuna mkungu wa ndizi
Na Dunstan Shekidele Morogoro.
Kama kawaida Kila Jumatatu Mtandao Pendwa wa Shekidele unarusha habari kali ya wiki.
Kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wetu jana Jumatatu hatukuweza kurusha habari hiyo na Mbadala wake inaruka leo Jumanne, hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea kwa wasomaji wetu.
Baada ya ufafanuzi huo tuingie kwenye habari hiyo kali iliyosakwa wiki iliyopita, ambapo wapangaji Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro wameitisha kikao na kumuweka kiti Moto baba Mwenyenyumba wao wakipinga kumlipia kodi ya jengo la nyumba yake kupitia michango ya Luku ya Umeme wanachanga.
Baada ya Mwandishi wa habari hizi kurambishwa ubuyu huyo na wambea wa Mtaa ,alimtafuta baba Mwenyenyumba huyo ili kusikia kauli yake.
Baba mjengo huyo aliyeomba hifadhi ya Jina lake alithibitisha kuwekwa kiti Moto na wapangaji wake na mahojiano yetu yalikuwa hivi.
Mwandishi. Mzee mshikamoo.
Baba Mjengo. Marahaba karibu sana.
Mwandishi. Asante Mimi ni Mwanahabari nasiki hivi karibuni
wapangaji wako walikuweka kiti moto Agenda ya kikao hicho ilikuwa ni ipi?
Baba Mjengo. Yaani ni Mambo ya ajabu sana mimi na nyumba yangu wapangaji wananinyanyasa jambo ambalo sikubaliani nalo.
Nyumba hii inavyumba 15 kila mwezi tunatumia umeme wa elfu 15 hivyo kila mpangaji kwa mwezi analipa elfu moja ya Umeme.
Agenda ya kikao hichowanadai kila mwezi wananilipia Kodi ya jengo kupitia Luku hivyo wamehitaji walipe mia 9 hiyo mia nilipe mimi kama kodi ya jengo langu wao hiyo kodi ya jengo wanadai haiwahusu.
Mwandishi. Kwa hiyo umekubari kufanya hivyo?
Baba Mjengo sijakubari baada ya kikao wote nimewafukuza kwenye nyumba yangu, Mgosi watu hawana shukrani.
Mimi ninanyumba Tatu hii hapa Morogoro na mbili ziko nyumbani Tanga nyumba zote 3 kila moja inavyumba 15
Miaka yote ikifika mwenye Mtukufu wa Ramadhan mwezi huo wapangaji wangu wote hawalipi kodi wanakaa bure kama sadaka yangu ya mwenye mtukufu wa Ramadhan.
Leo hawa wapangaji wa Morogoro wananiweka kiti moto kwa shilingi mia moja malalamiko hayo wangeya peleka Tanesco walioweka kodi ya Jengo kwenye Luku.
Mwandishi. Je umeshapata wapangaji wengine na kama umepata Elimu gani juu ya shwala hilo la Luku ili usije kuwekwa tena kiti moto ?
Baba Mjengo nimepata baadhi ya wapangaji vyumba vingine havijapata wapangaji, kila mtangaji anayeingia namueleza swala hilo nashukuru wote walioingia wanajitambua baadhi wamesema nyumba walizotoka kwa mwezi walikuwa wakilipa umeme mpaka elfu 5 kuwambia hapa kwangu umeme kwa mwezi elfu moja wameshangaa sana nashukuru wapangaji wangu hawana vifaa vinavyo kula umeme mwingi.
Mwandishi Asante kwa ushirikiano yako.
Baba Mjengo. Ok asante na wewe kwa kuja ila ombi langu ndugu Mwandishi kata yetu hii ya Tungi tuna kero kubwa ya Maji hebu tusaidie kupaza sauti kwa viongozi.
Mwandishi. Sawa nitafanya hivyo.
No comments:
Post a Comment