Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, October 17, 2024

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu
.....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya
...Miili ya marehemu ingiinizwa kwenye majeneza tayari kwa kuelekea msikittini
                              .......Safari ya kuelekea msikitini


                      Marehemu Sebuge enzi za uhai wake

 

     Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

INASIGITISHA SANA. Muuza Magazeti Maarufu mkoani Morogoro  Sebuge Mohamed, anadaiwa kujinyonga hadi kufa, muda mfupi baada ya kutoka kwenye kikao cha  familia ya Mazishi ya Mpendwa dada yake Marehemu Mwahamisi Kaliati aliyefariki dunia Octobar 12.

Tukio hilo la kujinyonga limetokea usiku wa Octobar 13 nyumbani kwa Marehemu Sebuge Mtaa wa Ngoma B Kata ya Mji Mpya mkoani hapa,  muda mfupi baada ya Sebuge kutoka kwenye kikao hicho kilichofanyika  majira ya jioni nyumbani kwa marehemu Mwanahamisi  Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo.

Mara baada ya Mwandishi wa habari hizi kushiriki mazishi ya marehemu hao   waliosaliwa na kuzikwa siku moja Makaburi ya Kolla  Octobar 14,

Siku iliyofuata Octobar 15 Mwanahabari huyo aliingia mzigoni kwa kuwahoji watu mbali mbali wakiwemo wanafamilia na viongozi wa serikali ya Mtaa.

Mtandao huu ulifanikiwa kuzungumza na Bi.  Pili Sebuge ambaye ni Mama wa marehemu wote wawiwli waliozima ghafra kama mshumaa.

Alipotakiwa kueleza vifo hivyo  Bi’Mkubwa huyo alisema.

” Inauma sana Mwanangu Mwahamisi ambaye ni Mtoto wa dada yangu aliyeniachia ziwa alifariki kifo cha kawaida,siku iliyofuata tumeketi kikao cha familia cha kupanga mazishi.

  Sebuge ambaye ni Mtoto wangu wa kwanza  kumzaa aliketi hapo ulipokaa wewe akiongoza kikao hicho tukaamua Mwahamisi tumzike Ochotar 14.

Sebuge akatapanga wachinga Kaburi la dada’ke  wapishi na watu watakao kwenda kwa Abood kuomba basi”alisema Mama huyo na kuongeza.

Baada ya kikao kutamatika Mwanangu alimuacha mkewe hapa akatuaga kaenda kulala kwake.

Pale kwake anaishi na mwanae pamoja na Mpwa wake mtoto wa huyo Marehemu Mwanahamisi na kila siku alfajiri Mwanangu Sebuge huwaamsha hao wanae na kwenda kuswari ile swala ya saa 11alfajiri.

Kwa sababu watoto walishazoe kuswali swala hiyo baada ya kuona hawakuamshwa wakahisi labda baba yao ametangulia msikitini, wakaende msikitini walipomaliza kuswali hawakumuoba.

Ndipo waliporejea nyumbani walipoingia  chumbani chake wamemkuta Mwanangu ananing’inia juu ya paa amejinyonga”amesema Bi Mkubwa huyo na kuangua kilio na kushindwa kuendelea na mahojiano.  

Kwa pande wake Bi Aziza Omary ambaye ni Mke wa Marehemu alipohojiwa alisema.”Baba yetu wa familia ameondoka ameniachia malezi ya watoto wengu kinachoniuma zaidi  mtoto wetu Mohamed siku 6 mbele anatakiwa kujiunga chuo cha Afya baada ya kuhitimu kidato cha 6”alisema Mjane huyo na marehemu na kuangua kilio.

Akitoa mawaidha kabla ya marehemu wote wawili kwenda kuswaliwa Msikiti wa Mwembesongo, Shehe Maulid Baggo alisema.” Baada ya ndugu yetu kujinyonga watu walisema mengi kuhusiana na uhalali wa kumswalia au kutomswalia.

Kwa msikiti wetu wa Mwembesongo tunaamini anayetoa huku ni mwenyezi Mungu pekee na si mwanadamu hivyo tubebe maiti zote mbili tukaziswalie pale msikitini kisha tukazike”alisema Shehe Baggo na kupokea zawadi ya makofi  kutoka kwa Umati wawatu walifurika msibani hapo mtaa wa River Side .

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Daniel Matonya alithibitisha Mwananchi wake kujinyonga ndani ya mtaa wake.

Alipoulizwa kama anajua chanzo cha mwananchi wake huyo kuchukua maamuzi hayo magumu ya kujitoa uhai, mwenyekiti huyo alisema.

“ Baada ya kupokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa wananchi alfajiri ya siku ya tukio awari nilimpigia Mh Diwani Emmy Kiula, baadae nikampiga simu Polisi walifika wakaushusha mwili kisha wakaupekua mwili wa marehemu kama kuna ujumbe wowote amkeandika.

Kweli kwenye mfuko wake walikuta barua ndefu polisi wakamwita Mtoto wa marehemu wakamuuliza huu ni mwandiko wa baba yako? Mohamed baada ya kuangalia ile barua kasema ni mwandiko wa baba yake.

Kilichoandikiwa hata mimi mwenyekiti sikuambiwa hivyo sijui chanzo cha kifo ninachoweza kuthibitisha kwako ni kwamba marehemu ameacha jumbe”amesema Mwenyekiti huyo.

Mtandao huu unatoa pole kwa familia, Mungu azidi kuwatia nguvu kwenye kipindi hichi kigumu mnachopitia cha kuondokewa na wapendwa wetu .

                

Wednesday, October 16, 2024

MORO KIDS MABINGWA WA WILAYA CRDB FEDERETION CUP 24- 25.

Mh Selestini Mbilinyi akiwasalimia wachezajii wa Uluguru Montain Academy
              ......Akiwasalimia wachezaji wa Moro  Youth
Kocha Mkuu wa Uluguru  Ally Jangalu akikabidhwa fomu na mchezaji wake
                                                     Kikosi cha Moro  Youth
                                  Kikosi cha Uluguru
Mwamuzi akimkagua mchezaji wa Moro Youth aliyeumia
                                  Heka heka uwanjani




Mtifuano Mkali beki wa Moro Youth Hamza Ally akimdhibiti winga wa Uluguru Juma lssa asilete madhara gorini kwake





Kufungwa ni Noma Moja haika mbili haikai, kocha wa Uluguru Ally Jangali akianglia saa wakati tiimu yake ikiwa nyumba kw abao 2-0, kulia ni wasaidizi wake  Kocha wa makipa Bure Mtagwa, Kocha Msaidizi Mohamed Mtono, na Meneja wa timu Hamis Malifedha. Wote hao waliwahi kuitumikia Reli ya Morogoro

Mh Mbilinyingi akimkabidhi kombe la Ubingwa Nahonda wa Moro Youth Kondo Maulid


     Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Moro Youth  imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Michuano ya shirikisho Maarufu CRDB Bank Federetion Cup Wilaya ya Morogoro msimu huu wa 24-25.

Vijana hao wa Moro ambayo ni kikosi cha pili cha timu ya Moro Kids inayoshiriki ligi daraja la Pili Tanzania [SDL], imefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuinyuka timu ngumu ya Uluguru Mountain Academy kwenye mchezo wa fainali uliopigwa juzi Uwanja wa Saba saba Mkoani hapa.

Toka gemu hiyo inaanza Vijana wa Kiluguru waliwakimbiza vilivyo Vijana wa Moro, muda wote wakiwa kwenyye lango lao wakisaka bao. Juhudi hizo waluguru ziligonga mwamba dakika 27 baada ya Winga wa Moro Youth Benson Kenedy kuunganisha kwa kichwa kona iliyochongwa na  Hassan Coaster na kumpita kipa wa Uluguru Poul Simon.

Wakati mali ikielekea kuzama gorini beki Luqman Juma alichupa kama nyani na kuunyaka mpira huo, Mwamuzi aliamua Mkwaju wa penality na kumtoa nje  kwa kumzawaidia Umeme’kadi njekundu’. 

Kufuatia adhabu hizo mbili kwa mpigo tena za mwanzoni kabisa mwa mchezo ziliwanyong’onyesha Vijana wa Kiluguru na kujikuta wakipachikwa bao la pili dakika ya 78.

Baada ya kunyakua Ubingwa wa Ligi hiyo iliyoshirikisha timu 16 Moro Youth kutoka kwenye Academy Maarufu nchini ya Moro Kids walikabidhiwa Kombe  pesa  250,000.

 Uluguru Academy inayomilikiwa na wachezaji nyota wa  zamani, John Simkoko  mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Uluguru Mountain, Hussein Ngurungu Mwenyekiti, Ally Jangalu  kocha Mkuu wa taasisi, Mohamed Mtono Kocha Msaidizi na Bure Mtagwa Kocha wa Makipa, wao waliambulia kifuta jasho cha lakini Moja na nusu.

Mgeni rasmi katika fainali hiyo alikuwa Mwenyekiti wa chama cha Soka Wilaya ya Morogoro [MDFA] Mh Selestin Mbilinyi.

Mara baada Mh Mbilinyi kunyakua uwenyekiti huo takribani miezi 5 iliyopita Wilaya ya Morogoro imepiga hatua kubwa kisoka chini ya Uongozi wake Moro Kids imefanikiwa kupanda daraja la pili.

Kwa mafanikio hayo  baadhi ya watu waliibuka na kutafuta kanuni za kumuodoa madarakani Mhe Mbilinyi ambaye pia ni diwani wa Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.

Siko zote Mungu husimani upande wa mwenye haki hivyo licha ya nguvu kubwa kutumika za kutaka kumng’oa Mh Mbilinyi Mungu alikuwa upande wake na mwisho wa siku watu hao waliferi.

 Kwa sasa Mhe Mbilinyi ambaye pia ni diwani wa Kata ya Lukobe ‘Kipenzi cha Wana Lukobe’ anaendelea kukalia kiti hicho kwa mamlaka ya Mungu na wajumbe wa mkutano Mkuu wa MDFAwalimchangua kihalali.

PIchani Mhe Mbilinyi akikagua timu ya Uluguru Mountain.

Picha no 2 Mh Mbilinyi akimkabidhi kombe la Ubingwa Nahodha wa Moro Youth Kondo Maulid.

Angalia picha za Matukio mbali mbali ya fainali hiyo kwenye profaili na Mtandao huu.



 

Monday, October 14, 2024

UDAKUZI SPESHO. MAMA AMSHANGAA MWANAE ALIYETOA SADAKA NYINGI KANISANI

Mwandishi wa habari hizi akimhoji Askofu Jacob Ole Maneo wa KKKT Dayosisi ya Morogoro.  

 

 Mdakuzi akizungumza na Askofu Teresphori Mkude wa Kanisa la Roman Dayosisi ya Morogoro. 

Kwa sasa Askofu Mkude amestaafu cheo hicho cha Uaskofu.


  Mdakuzi akimhoji Mwimbaji Maarufu wa nyimbo za lnjiri nchini Stara Thomas

              

  Na Dunstan Shekidele,Morogoro. UKISTAAJABU ya Mussa, hutoyaona ya Firahuni.

 Msemo huo umetimia jana  kwenye lbada ya Sakrameti ya Ekaristi kufuatia Mzazi kumshangaa mwanae aliyetoa kiwango kikubwa cha sadaka.

Tukio hilo limetokea Jana Jumapili Mkoani hapa,kwenye lbada hiyo iliyofanyika kwenye moja ya kanisa Kongwe nchini, jina linahifadhi kwa sababu za kiudakuzi.

            ISHU ILIKUWA HIVI.

Mdakuzi aliyekuwepo kanisani hapo mara baada ya kutamatika kwa lbada hiyo iliyojaza umati mkubwa wawatu kufuatia uwepo wa tukio hilo la madent zaidi ya 100 kupokea  Sakrameti hiyo Takatifu yenye msingi wa kulijenga kanisa la kesho kwa lmani ya Dhehebu hilo.

Mara baada ya kutamatika kwa lbada hiyo mmoja wawahitimu hao alilakiwa kwa basha na Mama yake  huku akimvisha taji baada ya kumaliza masoma hayo ambayo ni dira kwenye maisha yake ya kiimani.

Baada ya kutamatika kwa zoezi hilo la pongezi Mama huyo aliyesindikizwa na kundi la Mashosti zake waliong’ra kwa sare  za madera ya rangi ya mawingi,alimuamulu bint yake huyo amkabidhi ile  elfu 10 ya usafiri ili aite Bajaj warejea nyumbani kuendelea na sherehe.

 Bint huyo alimwambia Mama yake  kwamba elfu 20  aliyomkabidhi  ya sadaka na usafiri ameitoa yote sadaka.

”Ngoja kwanza nicheke, shoga zangu  huyu Mtoto asubuhi tumemkabidhi elfu 20 kwa mgawanyo kwamba elfu 5 ni zawadi ya padri, elfu 5 nyingine ni Sadaka na elfu 10 ni nauli ya Bajaj.

 chaajabu elfu 20 yote kaitoa sadaka sasa ataludi nyumbani na miguu”alisema Mama huyo.

Kufuatia kauli hiyo mmoja wa mashoga wa mama huyo alibeba jukumu la kumhoji mtoto huyo akimuliza ni kwa nini amekiuka maagizo ya Mama yake.?

Kwa ujasili mkubwa huku akijiamini mtoto huyo alijibu.”Nimekiuka maagizo hayo kwa sababu ya msimamo wa imani yangu iliyojengwa na mafundisho haya ya Ekaristi.

Kama hiyo haitosho leo kwa mara ya kwanza   nimeungama  baada ya kuungama tumetangazima kwamba kuna sadaka ya ziada ya kuwapa motisha makatekista wetu waliotufunisha zaidi ya mwaka hapa kanisani.

Hivyo kwa kuwa sikuwa na pesa nyingine zaidi ya ile elfu 10 ya nauli niliamua kuitoa  kwa lengo la kuilinda  imani yangu niko tayari kutembea kwa Miguu kuludi nyumbani”alisema Mtoto huyo.na kupokea zawadi ya Makofi na Vigeregere kutoka kwa kundi la watu walimshangaa kwa kutoa sadaka hiyo.

Maneno hayo yaliyojaa uzito mkubwa yalimgusa  Mama mzazi wa binti huyo, mdakuzi alimshuhudia mama huyo  akiluika huka kwa furaha sambamba na  akimbeba juu juu mwanae huku akisema kwa kiwango hicho cha lmani amefanya vizuri kutoa hiyo elfu 10 kuwapa zawadi waliofanya kazi kubwa ya kumuimalisha kiimani.  

Kwa furaha Mama huyo alifungua pochi na kutoa elfu 10 nyingine akaita Bajaj wakapanda na kuondoka zao

                    

 

Friday, October 11, 2024

MH DIWANI AONGOZA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA.

Mama Kiula akijiandikisha kwenye Daftari hilo hii leo.

     Na Dunstan Shekidele Morogoro.

Diwani wa Kata ya Mji Mpya Jimbo la Morogoro Mjini Mh Emmy Kiula.Maarufu Mama Kiula Leo amewaongoza wananchi wa Kata hiyo kujiandikisha kwenye Daftari la Makazi.

Mama Kiula amejiandikisha kwenye mtaa anaoishi wa Ngoma A uliopo kando kando ya Mto Morogoro.



 

Zoezi hilo litakalodumu kwa siku 10 limezinduliwa Leo na Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mara baada ya wananchi kujiandikisha watakuwa na haki ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Vijijim Vitongoji na MItaa uliopangwa kufanyika Novembar 27.

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...