Na Dustan Shekidele, Morogoro.
LICHA ya Viongozi wetu wakuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan,Mkamu wa Rais Mh Dkt Philip Mpango na Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa.
Mara kwa mara kutoa Maagizo ya kuwataka watendaji wa serikali kuwa na kauli nzuri kwa wananchi sambamba na kufanya kazi kwa Weledi, baadhi ya watumishi hao wanapuuza Maagizo hayo.
Hilo limethihilika jana baada ya Mwandishi wa habari hizi kukutana na kadhia hiyo ya kutolewa maneno makali na watumishi wawili wa Zahanati ya Kata ya Mji Mpya.
Mwanahabari huyo alitinga kwenye kituo hciho cha Afya kwa lengo la kuchoma Sindano ya Kinga ya Tetenasi baada ya kupigwa na chupa kwenye paji la Uso.
Baada ya shambulizi hilo Rehemu Shekidele dada wa Mwandishi huyo ambaye ni Muuguzi hospital ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro, alimshauri kwenda kuchoma Sindano ya Tetenasi.
Alitiii ushauri huo na kutinga Zanahati ya Mji Mpya na kukutana na madudu haya.
HALI ILIKUWA HIVI.
Nimefika mapokezi sijakuta mtu nimesimama zaidi ya dakika 5 akaja Nesi na kuliza shida yangu, nikamueleza kwamba nahitaji kuchonga sindano ya Kinga ya Tetenasi.
Bila kusema chochote kafungua ndoo iliyokuwa juu ya meza katoa kichupa cha dawa kisha kachukua bomba la sindano bila kuandika popote kaanza kuvuta dawa kwenye kichupa hicho na kuingiza kwenye bomba la Sindano.
Wakati akiendelea kufanya hivyo akaniambia nivue shati anichome kwenye paja la mkono kisha akiniambia nitoe elfu 5 kama gharama za sindano hiyo.
Nikamueleza kwamba nina Bima ya Afya, akanitazama kwa jicho kali kisha akaniambia niingie ndani kwenye Computer nikaingizwe kwenye mfumo kisha nirejee kwake.
Nimeingia ndani kwenye hicho chumba hapakuwa na muhudumu nimekaa tena kama dakika 10 nikiwa na wagonjwa wengine tukisubiri huduma hiyo.
Nilivyoona muda unasonga nikaamua kuzunguka vyumba vingine kutafuta muhudumu wa kitengo hicho, nikaambiwa muhudumu wa kitendo hicho ni huyo huyo Nesi aliyekuwa nje eneo la mapokezi.
Nikaludi kwake akaniambia muhudumu wa kitendo hicho ametoka amemshikia kwa muda na kwamba nisubiri amalize kumuhudia mgonjwa atakuja.
Chaajabu licha ya kukuta foleni ya wagonjwa wakisubiri huduma yake, kapanda juu ya kiti na kuanza kupiga stori na Nesi mwingine.
Nikamuliza kwa hekima kwamba umekuta foleni kubwa wagonjwa wakikusubiri tena wakiwemo wanawake wenzio wenye watoto wagonjwa badala ya kuwahudumia unaanza maongezi.
Kauli hiyo nikama nimepigw ajiwe kwenye mzinga wa nyuki nilishambuliwa kwa maneno makali na manesi hao wawili ambao kimsingi hawakunifahamu na mimi siwafahamu.
Baadhi ya maneno hayo yanayoandikika mtandaoni ni haya ‘ Sisi tuna njaa hatujala huyu Nesi ni Mgeni leo ndio amelipoti hapa kituoni hajui chakula kinauzwa wapi’Maneno mengine makali zaidi kwa sheria za Kitaaluma na baki nayo moyoni
Nikawajibu sisi wananchi tumefuata huduma hapa kituoni hilo la Nesi mgeni au hamjala sisi wagonjwa yanatuhusu nini au mnataka wagonjwa tuwanunulie chakula? Maneno hayo yamewachoma wakafungua busta tena.
‘ Sisi sio Punda ni binadam kama nyinyi mnetoka majumbani kwenu mmeshiba mkifika hapa mnanata kutupelekesha.
Nesi huyu mrefu kwenda chini[mfupi]huku akiwa amenuna kama karamba ndimu kachukua kadi yangu ya Bima ya Afya kaniingiza kwenye mtandao alipomaliza kaniambai kituo hakina Daftari hivyo niende dukani kununua nikamuliza kituo cha Afya hakina daftari la mia 3 kasema ndio.
Kwa sababu nilihitaji uchunguzi wangu utimie nikaenda kununu Daftari hili kwa bei ya mia 3, nikajerea akanipa fomu za Bima na kunielekeza kwa Daktari.
Ama kwa hakika Daktari alinipokea vizuri na kunihudumia vizuri, kwa huduma yake nzuri nikamuomba na hiyo sindano anichome yeye nikigoma kuchomwa na huyo Nesi mwenye Njaa iliyojaa kisirani.
Daktari huyo mtiifu kakubuli ombi langu katoka ofisini kwake kaja kwenye ofisi ya huyo Nesi na kunichoma Sindano hiyo kisha akaniambia baada ya mwezi nirejee kuchoma ya pili.
Kituko kingine Nesi huyo kachukua hizo za Bima kanisainisha, kawaida ukishapata hudumu unakabidhiwa copy.
Nilipohitaji copy Nesi huyo kagoma kunipa akidai njaa inamuuma hajamaliza kuingia taarifa zangu kwenye Mtandao.
Nilifosi kupewa haki yangu hiyo ya Copy Nesi huyo aligoma katu katu nikaamua kuepusha kelele eneo la wagonjwa, hekina na busara kwa pamoja vikaniongoza kuicha copy hiyo.
Ushauri wangu kwa Wizara ya Afya wafanye kama walivyofanya wenzao wa Wizara ya Mambo ya Ndani, kila polisi unatambulika kwa namba zake kifuani. Ukiona Polisi kakukose au kukufanyia jambo jema unamtambua kwa namba zake ambazo ni nne tu rahisi kuzishika. Manesi na Madaktari nao wangekuwa na hizo namba tungewatambua hapa ningetaja namba za huyu Daktari aliyenipa hudumu nzuri Mungu ambariki na hapa pia ningetaja namba na hao manesi visiwani wanaowafokea wagonjwa.
Stori hii itaendele baadae kuelezea kisa cha Mwandishi wa habari hizi kupigwa na chupa chini ya jicho wakati akiamulia ugomvi wa mtu na mkewe.
No comments:
Post a Comment