Na Mwandishi Wetu Morogoro.
MWANDISHI wa habari Dustan Shekidele,amepigwa na chupa jichoni wakati akiamulia ugomvi wa mtu na mkewe .
Tukio hilo la kusigitisha limetokea Octobar 21 majira ya saa 3 usiku mtaa wa Area Six kata ya Kichangani Mkoani hapa.
Akisimulia Mkasa huo Shekidele alisema,
“Mara nyingi nikitoka kazini mapema huo naacha pikipiki Mjini narejea nyumbani na Miguu au na baiskeli kwa lengo la kufanya mazoezi.
Ratiba yangu iko hivi nikimaliza kazi saa 12 au saa moja naludi nyumbani na Miguu, nikimaliza saa 2 au saa 3 usiku nareja nyumbani na Baiskeli na nikimaliza saa 4 au saa 5 usiku naludi nyumbani na pikipiki.
Jana nilitoka kazini saa 3, nilipofika mtaa ya Area Six katikati ya barabara ya Lami yenye taa za Solla mbele yangu umbali wa takribani mita 200 nimeshuhudia Mwanaume akimchapa makonde Mwanamke ambaye hakujibu mashambuiliza badala yake aliangua kilio cha kuomba msaada huku akiendelea kupigwa kama ngoma”alisema Shekidele na kuendelea kudadavua mkasa huo.
Nilipokalibia nilisikia sauti ya Mungu ikinitaka nijitose kumtete Mwanamke huyo, nilitii sauti hiyo nikapack baskeli kando ya barabara ambayo naina msongamano wawatu hasa nyakati za usiku nikabeba jukumu la kumtetea Mwanamke huyo.
Wakari namtete kumbe Mwanaume huyo mfukoni alikuwa na Chupa ndogo ya pombe kali aina ya konyagi aliyoinywa nusu.
Hivyo wakati naendelea kumzuia Mwanaume huyo asiendele kumpiga Mama huyo njema hiyo alichomoa chupa mfukoni na kunipiga nayo kwenye paji la uso eneo la nyusi chini kidogo ya jicho kushoto.
Chupa hiyo ilipasuka vipande viwili”alisema Mwanahabari huyo na kuendelea kusimulia kisa hicho.
Mungu anisemehe na Jumapili nitakwenda kuungama Kanisani,kwa hasira niliokota kipande cha chupa kilichochongoka nakuanza kumchoma nacho jamaa huyo baada kuona nimemzidi nguvu kakimbia.
Huku damu zikiendelea kuvuja kama bomba la Maji, nimuliza Mwanamke huyo sababu za kupigwa na mwanaume huyo alisema,
Jamaa huyo ni mume wake wa ndoa na kwamba walitoka baa kunywa pombe na kwamba ugomvi huo ulianzia huko baa baada ya mwanamke huyo kukutwa na mumewe akimpa namba ya simu Mwanaume mwingine wakati mumewe walivyotoka kwenda msalani.
Nikamuliza kwa nini alifanya hivyo ili hali alikuwa na mume wako huki naye akiwa melewa alikili kosa hilo akidai ni sababu za ulevi huku akimtupia lawama lbirisi Shetani kwa kumpotosha.
Baada ya kusikia hivyo nikaondoka zangu huku jereha langu likiendelea kuvuja damu, kikubwa namshukuru Mungu kunipunguzia makali ya tatizo kama chupa hiyo ingepasuka kwenye jicho lingepasuka.
Nafarijika kwamba damu yangu nyingi kumwagika chini ya ardhi kwa kubeba msalaba wa mtu mwingine.
Juzi Octobar 23 nilikwenda Zanahati ya Kata ya Mji Mpya kuchoma sindano ya Kinga ya Tetenas na kwa sasa namshukuru Mungu naendelea vizuri”alimalizia kusema Shekidele.
Mikaa ya hivi karibuni Abdul ‘Bonge’ Tale Tale arifariki dunia jijini Dar es salaam alipokuwa akiwaamulia wanaume wawili waliokuwa wakipigana.
Hayati Abdul ‘Bonge’ Tale tale, ambaye ni Kaka wa damu wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini mashariki Mh Hamis Shabani Tale tale ‘Maarufu Babu Tale’ ambaye pia ni Meneja wa Msanii Maafuru Afrika Mwana Kigoma Tanzania Nassib Abdul ‘Diamund Platnumz’ alizikwa kijijini kwao Mkuyuni Matombo Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, huku shekidele akiwa miongoni mwa watu walishiriki mazishi hayo yaliyoongozwa na mastaa kibao akiwemo Diamond ‘Baba Tiffa’
No comments:
Post a Comment